SOMO: KITI CHA ENZI CHA SHETANI

SOMO LA LEO_TAREHE 26 / 7 / 2015_KUBOMOA KITI CHA ENZI: SNP PAUL JOSHUA
Kila anayeongoza watu kuna kiti chake ambacho anakalia. Ukienda sehemu yoyote… kila mtawala wa mwilini na mtawala wa rohoni anakiti chake cha katika utawala wake. Hata Mungu wetu amekaa katika kiti chake cha enzi
Ufunuo 7: 9-12
Baada ya hapo tutaona kuwa kuna watu wamekalia viti vya enzi  na wanatawala eneo hilo. Tukifanya kwa mapenzi yetu tutashangaa mtawala huyo atatutawala mpaka nyumba na mifugo wetu.
2 Samweli 3:9
Huwezi kufanikiwa sehemu mpaka umpige anayetawala eneo hilo. Huwezi kufanya biashara sehemu mpaka umpige mtawala wa eneo hilo.
Kiti ni maisha kitikinakupa utawala wa eneo hilo pamoja na kila kitu na mali. Mtawala akisema hakuna mnakuwa hamna ujanja.
Familia zote zaweza kulia njaa,elimu mbaya, madawa hayatoshi lakini mtawala hana tatizo hilo wala shida hiyo.
Zaburi 11: 4
Kumbe Mungu naye anakopoe, ana macho. Tena anakiti na anatawala. Ukitaka kutawala wewe pasua kiti cha utawala, ukipasua atakaa chini na akikaa chini maana yake mtawala.
Ufunuo 2:13
Unaweza kukaa sehume yoyote kwaamani na furaha kama  utafanikiwa kumpiga mtawala. Ndio maana kila sehemu zinatofautiana maana watawala wanatofautiana. Mambo ya kigoma yanatofautiana na mambo ya mwanza maana sehemu hizi zina viti vya enzi tofauti katika ulimwengu wa roho
Maeneo ambayo shetani ameweka kiti chake cha enzi
Anga , angani kuna kiti cha enzi cha shetani, anatawala lakini pia elewa kuwa shetani anaitwa mfalme wa anga.
Unajua sio kwamba watu hawaombi ila wanaomba kwa kukosa maarifa ya vita vya rohoni
Daniel, Mungu anasema kila aombaye hupewa lakini mbona hatupati? Je Mungu ni muongo? Mungu amekwaisha kujibu bali yupo mkuu wa anga azuiae.
Kuna mbingu ya kwanza ya pili nay a tatu,ili maombi yako yapenye ni lazima uwe rohoni sana
Kiti cha enzi cha baharini
Kiti cha enzi katika nchi

Matendo16:16
Anayetawala nchi ana utawala wake anaouongoza
Kiti cha enzi ndicho kinachochagua upate pesa au mafanikio, huwezi kumiliki bila kumpiga mkuu wa anga
Paul alihubiri sana lakini alikuwa hajagusa kiti cha enzi cha shetani, unaweza ukaomba sana hujajibiwa, kuna sehemu moja tu ukigusa ambayo ndiyo kiti cha enzi, ukigusa tu , unafanikiwa. Unapoomba hakikisha unaomba mpaka uhuse kiti cha enzi.
  Sio kila kitu ni cha kutii na sio mamlaka ni yakutii lakini maana anaweza akasema mkubwa au mwenye mamlaka  maana unaweza kujikuta  unatii yasiyo mapenzi ya Mungu, kwani shetani anaweza kumtumia mtu yeyote katika ukoo au nchi au familia ili kupitisha mawazo yake au matakwa yake. Hivyo sio kila mamlaka ni yak utii , chunguza kwanza ni kiti kipi cha enzi kinachoongoza ndani ya mamlaka.