SOMO LA LEO_TAREHE 15/3/2015_NATUVUKE TWENDE NG’AMBO:SNP PAUL JOSHUA.



SOMO LA LEO_TAREHE 15/3/2015_NATUVUKE TWENDE NG’AMBO:SNP PAUL JOSHUA.
Maisha ya mtu yanaanza na zero na baada ya hapo Mungu anakuinua. Kila aliyefanikiwa ameanza na sifuri na baada ya hapo anaingia 1,2,3 mpaka mamia, kuhama pointi moja kwenda sehemu nyingine yahitaji kupambana.
Kuna watu wengi wameishia kwenye mbili au tatu ya maisha na wachawi wamembana ili asihame, wachawi walikubanana ukikaa hatua moja na adui yako hatakuheshimu, lazima uvuke ng’ambo adui yako akuheshimu, lazima uwe juu ya adui zako ili wakuheshimu.
Leo Yesu anasema lazima tuvuke twende ng’ambo ya maisha yetu
Yohana 6:15 -18
Wanafunzi walipoanza kuvuka upepo ukaanza na mawimbi yakaanza, kabla ya hapo hapakuwa na upepo na hali ilikuwa shwari, kabla hujaanza kuinuliwa hali inakuwa shwari lakini unapoanza kuinuliwa hali inachafuka
Luka 8:23 Kila Yesu alipotaka kuvuka upepo ulikuwa unavuma.ukiona misukosuko Imeinuka ujue unataka kuvuka, ukiona shwari ujue si shwari hivo jitahidi upate changamoto  ili wakurahisishie safari yako,adui wakiinuka kama ulikuwa huombi utaanza kuomba , kufunga, kunena kwa lugha na kumtafuta Mungu.chura anamwendo wa pole pole lakini ukiamua kumpiga teke unamsogeza kwenye hatima yake japo atakuwa na maumivu, wanakuchezea sana lakini ndio wanakusukuma kwenye hatima yako . kama huna mtu wakukusogeza mbele basi  mtafute, kama huna adui wakukuonea wivu ili akuseme nakukufanya ukazane kusogea kwenye hatima yako basi hakikisha unafanya jambo ambalo litainua watu watakao kusukuma na kusonga mbele.
Kila mtu akianza kuvuka lazima vikwazo viinuke, hata kazini kwako utapata matatizo ,utasemwa, utachongewa, na kila aina yavikwazo utawekewa. Ukiona hivo ujue umeanza kuvuka hivo weka bidii katika kupambana maana adui zako wanafanya juhudi kuhakikisha huvuki.
Ifikie hatua adui zako wabaki chini yako, kataa kubaki level/ nafasi  moja na adui yako. Usipende kumsema mtu,mtu akikusema wewe timua vumbi.
Kuna watu wana neema ya kuvuka lakini wameshikiliwa na wachawi , au kwenye ukoo kuna kigagula anawazuia wasivuke,kila ukitaka kuvuka unakwama.
1 wakorintho 16:9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana na wako wengi wanipingao. Kama una mlango mkubwa wakufaa sana kwanini huvuki? Huvuki kwasababu wapo wengi wakupingao.
Isaya 60:11- - , Kila mtu ana mlango wake, kazi ya malango ni kukuletea utajiri wa mataifa na kukuingizia Baraka , sasa wapingao hujiinua na kupinga malango yako.
Kuna malaika wa nuru na malaika wa giza na kazi zao nikusababisha mabaya au mazuri yakutokee. Malaika wagiza wanasababisha watu wateseke , waugue , wafukuzwe kazi,. Unateseka lakini hujui kwanini, kwasababu anayekusababishia kajificha kwenye kona iitwayo ulimwengu wa roho.
BARIKIWA.