SOMO:KIBALI KILICHO FUNIKWA.

JPILI TAREHE 20/3/2016
SNP: PAUL  JOSHUA
SOMO:KIBARI KILICHO FUNIKWA.
Kibari ni kama Pasport yako ya Maisha,Kwa maana nyingine Kibari ni Maisha ya mtu.(EZEKIEL28:15)Ulikuwa mkamilifu tangu siku ile ulipo umbwa kwa wingi wa uchuzi wako watu walikujaza Hapa andikohili hasa linamzungumzia Shetani ambae alikuwa ni malaika mzuri lakini baadae aliasi na kujulikana kama Kerubi afunikae.Kila mtu unaemwona Mungu alimpa kitu cha kipekee,na jinsi ulivyo wa kipekee ndivyo ndani yako ulivyo wa kipekee na Mungu alipomuumba mtu alimpa mtu Kibari, na ndio maana Wachawi na Waganga wakitaka kumchafua mtu huanza kufunika na kunyanganya kibari chako,Kibari ndio kila kitu kwenye Maisha kibari kinaweza kumpa mtu Kazi,Ndoa nzuri Mume na hata Mchumba anaefaa,Kiuchumi utafanikiwa na hata kiafya kila utakacho kifanya kinakubarika kwa kila mmoja.
(MWANZO 39:21)Lakini bwana akawa pamoja na Yusuphu na akampa Kibari mbale ya Mkuu wa Gereza,Yusuph alikuwa ni mtu ambae aliunzwa na ndugu zake na kuzingiziwa kumbaka mke wa mfalme ,Lakini Mungu katikati ya mateso ya Yusuphu Mungu alimpa kibari cha kukubarika mbele ya Mkuu wa Gereza Mungu alimueka mbali na Mateso akiwa Gerezani.
(MITHALI 8:35) Anionae mimi apata uzima nae atapata kibari mbele za bwana kumbe kuna kibari mbele za watu na kibari mbele za Bwana.(ZABURI 19:14) Maneno ya kinywa change na mawazo yangu yapate kibari mbele zako,hapa tunamuona Daudi akiomba kibari mbele za Bwana ili kila atakacho kifanya kipate kibari mbele za Bwana na mbele za Watu pia.
(1.SAMWELI 2:26) Na Yule mtoto Samweli kazidi kukua akapata kibari mbele za Bwana na mbele za Watu pia,samweli kabla hajawa Nabii yaani akiwa bado ni mtoto mdogo lakini Mungu alimpa kibari cha kukubarika yaani kila aliye muona Samweli alimsifia na kumuona wa tofauti sana na baadae kibari hicho kilimfanya akawa ni Nabii mkubwa katika Biblia. Katika maisha ili uende ni lazima uwe na kibari ndio maana unaweza ukamuona mtu anauza genge ya chakula na wako wengi lakini yeye ndio wa kwanza kumaliza chakula na unaweza kujiuliza kwa nini yeye lakini ni kwasabau mtu huyo anakibari cha Biashara na hata katika biashara ipo hivyo,Esta akapata Kibari mbele ya Mfalme na kuwaokoa wayahudi,Nami ni Maombi yangu mchana wa leo Mungu akupe neema ya Kuwa na Kibari cha kufanya chochote.Katika Biashara Mungu anakupa kibari yaani kila unachokianzisha kinakwenda na kinafanikiwa na  Kuna watu Mungu alimpa Kibari mbele za watu yaani unakubarika kwa kila mtu na kusikilizwa na wengine wanakibari cha uongozi  yani tangu akiwa  mdogo anakuwa ni kiongozi.Na kibari cha namna hii ndio kinachoweza kukufikisha kwenye hatima ya Maisha yako.Ni maombi yangu Mchana wa leo Mungu akupe kibari.Kibari kinafunika mapungufu yako yote hata kama ni kilema wa jicho Kibari kinaweza kufunika.Kibari kinamfanya mtu aliekuwa masikini anakuwa Tajiri,aliekuwa Tasa anazaa,Aliekuwa analala njaa anapata chakula,Aliekuwa chini kuinuka tena.Kibari mbele za watu kinamfanya mtu aliekuwa amedharaurika na mtu asiefaa kuinuliwa juu,Kibari kinaweza kusababisha watu wakukubari,kana mfanya mtu katikati ya wengi anachaguliwa yeye,kinamfanya alie choka na kukata tama anainuliwa na kuwa juu.Katika maisha ukikubariwa na watu tu unafanikiwa.Kibari mbele za watu humfanya mtu huyo watu wamtafute,humfanya aongoze wengine,Ndio maana hatima ya mtu ipo kwa mtu.
kibari kwenye ndoa,ukiona mwanamume anampiga mangumi mke wake ujue kuna kitu kilikuwepo ambacho kwa wakati huo hakipo,Wachawi wakitaka kufunja Ndoa kwanza huanza kuondoa kibari mbele za mume wako,na michezo hio inafanyika sana na wachawi yaani kile ambacho alikupendea Mume wako hakioni tena na hatimae Ndoa kuvunjika.Kibari ni kama Pasport ya maisha yako na kibari hicho kinaweza kikachafuliwa,na hata kufunikwa yaani kile ambacho ulikuwa nachokinaweza kufunikwa. ESTA 7:8)Kisha Mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali ya karamu ya Divai,wakamchukua hamani wakamfunika kitambaa Cheusi wakamfunika  wakamuua,Kumbe kibari cha mtu kinaweza kufunikwa Wchawi wanaweza kufunika chochote,kufunika kazi,kufunika tumbo la uzazi,kufunika fedha na kufunika cheo kazini.Ukiwa na kibari watu wanaanza kukuona tangu ukiwa mdogo na kufunga kibari ambacho Mungu alikiweka ndani yako.Kibari ndio Maisha ya Mtu.
Dalili tano za Mtu aliechafuliwa Kibari chake.
Utahisi kama una buibui Usoni,u utahisi kama kuna vitu vinatembea tembeaUsoni,ujue uso wako umechafuliwa umepakwa Mavi ama ngozi ya mnyama. Kuota mapele au chunusi yasiyo isha.
Utahisi mikono inajasho au inauma bila sababu,Utahisi miguu yako inawasha ama miguu mizito ama inawaka moto,ujue hutakiwi kwenda sehemu yoyote.Kila sehemu ukienda unagombana na watu,au watu wanakusingizia kila kitu hata kama hujafanya wewe,kila sehemu unaonekana ni mbaya.Hata kwenye ndoa yako hata ukifanya vizuri kwa mume wako anaona bado hufai na si kitu kwa mume wako.Lakini mchana wa leo Mungu anarudisha kibari chako na kila alie kuchafua atakutafuta sasa na kuja kumuulizia Mungu wako,Kwa maana bwana atatupigania na si tutanyamanza kimya,maana Bwana ni mtu wa Vita na Bwana ndio Jina lake.IU


UFUFUO NA UZIMA KIGOMA
JPILI TAREHE 13/3/2016
SNP:PAUL JOSHUA
SOMO:ALINYANG’ANYWA TOKEA NDOTONI.
Kila jambo huwa linaanzia moyoni,na lengo la somo hili ni kurudisha vyote vilivyochukuliwa katika maisha yako,Kwa sababu maandiko yanasema Mpendwa naomba ufanikiwe katika mambo yako yote.Lakini tunaona vitu vingi hatuna kwa sababu tulikwisha nyanganywa katika ulimwengu wa Roho.Ulimwengu wa roho kuna viumbe viwili ambao ni Mlaika wa Mwili na Malaika wa Nuru,Malaika wa Nuru ni mwanga wa maisha yetu ambao wanakazi ya kuhakikisha tunafanikiwa katika maisha yetu,katika Ndoa,Kazini,Kibiashara na katika sehemu zote za Maisha yetu.Lakini malaika wa Giza hawa ni maajenti wa sheteni ambao kazi yao ni kutengua yale makusudi ya mungu juu ya Maisha yetu,Hapendi kuona ukiwa na amani katika Ndoa yako,katika biashara na katika Familia,Malengo yao huwa ni kupindisha makusudi ya Mungu aliyopanga juu ya Maisha,Lakini leo kwa jina la Yesu tunawanyang’anya Baraka zetu kwa jina la Yesu.
(WAEFESO 1:3)Atukunzwe Mungu wa Baba wa bwana wetu  Yesu christo aliyetubarikikwa Baraka zote.Maana yake ulimwengu wa Roho kuna kila kitu,ndio maana leo tunamwambia Shetani aziachie Baraka zetu.Mambo yanaanzia ulimwengu wa Roho,Ndoto ni bayana na mambo utakayo yaishi kesho.Mungu humbariki mtu kupitia kwenye Ndoto.(2MAMBO YA NYAKATI 1:7)Usiku ule Mungu akamtokea usiku akamwambia Omba utakalo nikupe,kumbe mtu unaweza kupokea Baraka zako ukiwa umelala,Sulemani akamwabia Naomba Hekima na Maarifa ambapo kupitia hivyo vitakupatia Mali na Utajiri.Suremani akapata hekima na ufahamu kupitia kwenye Ndoto,kabla hujaanza kupokea mwilini huwa unaanza kupokea kwenye ndoto.
(MWANZO28:10)Yakobo akatoka Beer-sheba kwenda Harani akafika mahali Fulani usiku akalala usingizi palepale ndipo Mungu akamwambia Yakobo nchi hii uliyolala nimekupa wewe.Hapa unaweza kuona mafanikio tuliyonayo huanzia ndotoni,Na ndio maana wachawi wanacheza na Ndoto zetu unaweza kuota kitu kizuri lakini unasahau,kwa sababu wanajua hayo ndio maisha yako,sheteni anaweza kukunyanganya Ndoa yako,Kazi,na hata uchumi wako na chochote kizuri  kupitia kwenye Ndoto.Kila kitu huanzia Ndotoni,Hata Baraka za Mungu huanzia Ndotoni.Kuna mashetani na mapepo ambayo wanakazi ya kuwanyang’anya watu Fedha,na ndio maana unaweza kumuona mtu anatafuta maisha lakini hafanikiwi kimaisha ni kwa sababu kuna mashetani yanafatilia maisha yake.Mabaya unayoyapitia leo yalianzia ulimwengu wa Roho kwa kupitia Ndotoni,hata mazuri pia huanzia vivyo hivyo ndotoni.(MWANZO 40:1)Kitabu hiki cha Mwanzo kinatuonesha watu walioota ndoto iliyowachanganya sana na hawakuijua nini maana yake ndipo walipoenda kwa Yusuph ndipo yusuph akawapa maana yake kwamba atakuwa Mfalme baada ya sikutatu na ndivyo ilivyokuwa.Kumbe ndoto inaweza kumpeleka mtu kwenye hatima ya Maisha yako.haijarishi unapitia yapi sasa lakini unachotaka kufahamu ni kwamba Ndoto yako ni lazima itimie.
(MWANZO 40:16)Huyu aliota ndoto kabeba Nyung’o yenye Vyakula vyote vya Mfalme lakini akawaona Ndege wakaja kula kile chakula,Ndoto ile ilimchanganya sana ndipo alipoenda kwa yusuph akamwambia maana ya ndoto hii ni kwamba Baada ya siku tatu Mfalme atakiondoa kichwa chako na ndege wataila Nyama yako,Ndipo baada ya siku tatu zile kufika mfalme akafanya vile vile kama alivyoota.Kumbe matatizo ya mtu yanaweza kuanzia kwenye Ndoto.Ndio maana leo tunabadirisha yale mabaya yote uliyoota kwenye Ndoto,ili kuyaharibu  Maisha yako.wachawi  hucheza na ndoto za watu ama kumfanya asiote,kumfanya azisahau ndoto zako,ama kukufanya uzipuuzie hiyo yote ni mipango ya ibirisi na wachawi kwa sababu wanajua ndio kuna maisha ya Mtu.Wachawi wanaweza kumnyang’anya mtu chochote kwenye Ndoto,Kabla hujaanza kupoteza mwilini kwanza hupoteza Rohoni.Na kile unachokiota leo ndicho utakacho kiishi kesho.Lakini leo kwa Damu ya Yesu tunavunja kila Ndoto mbaya ulioota na kuifikia ile hatima ya Maisha yako.