JUMAPILI TAREHE 24/4/2016
SNP: PAUL JOSHUA
SOMO: NYOKA AZUIAE.
Katika wanyama wanaogopeka
na wanadamu wa kwanza ni nyoka,na Nyoka huyu ni mjanja kuliko wanyama wote. na
anaweza kuyatesa maisha yako bila wewe kujua.
(MWANZO 3:1) Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote alio wafanya Bwana Mungu,Akamwambia
mwanamke Ati hivi ndivyo alivyosema Mungu msile matunda yote ya bustani? Nae mwanamke
nyoka anamdanganya na kuingia dhambini.Huyu nyoka alimdanganya mwanamke nae
akala matunda ambayo Mungu aliwaambia wasiyale na kufanikiwa kuwadanganya,na
baada ya kula ndipo dhambi ilipoingia kwa mwanadamu na ndipo matatizo yakaanza
kwa mwanadamu tabu na shida hata sasa tunayapitia haya tunayo yapitia
sasa,Lakini leo kwa damu ya Yesu leo tunawashinda na huyu Nyoka wa maisha yako
tunamkata kichwa kwa jina la Yesu.Kumbe nyoka anaweza kumdanyanga Mtu.
(UFUNUO 12:13) Na Yule joka alipoona ametupwa katika nchi,alimudhi
mwanamke aliye mzaa yule mtoto mwanamume mwanamkeakapewa mabawa kama tai wakati
anaruka Yule Nyoka akatema mto na kumeza Yule Mweanamke kumbe tunaona si kila
mto unauona ni mto wa kawaida mingine ni mito ya kishetani na ndio maana
utasikia mto Fulani kila mwaka watu wanakufana kuzama kumbe ni Joka anaemeza
watu wa Mungu. Nyoka alipotupwa duniani akaanza kufanya vita na uzao wa
mwanamke na wale wazishikao amri za Mungu,Lakini tumepewa amri ya kukanyaga
Nyoka na Ng’e na wakuu wote wa giza,na hata hivyo tunayaweza mambo yote katika
yeye atutiae nguvu,hivyo hatuta ogopa,Nyoka huyu anaweza kufanya vita na kazi
yako,Biashara yako,ndoa yako na maisha yako kwa ujumla
(YOHANA 13:11) Kiaha nikaona myama mwingine akipanda juu katika nchi nae alikuwa na
pembi mbili kama mfano wa mwana kondoo lakini sauti yake ni kama Joka,kumbe
nyoka anaweza kujibadilisha na kuvaa sura ya mtumishi wa Mungu,anaweza kuvaa
sura ya utakatifu ilimkutimiza mapenzi yake,lakini leo tunamshinda katika jina
la Yesu.Lengo la huyu ni kuwavuta na kuwakusanya watu wa Mungu ili wamsujudie
Mnyama.
(UFUNUO 6:12) Na huyo wa sita alikimimina kichwa chache juu ya mto flati,nikaona
Roho tatu za mashetani zinazofanana na Vyula.Yohana akaona roho za mashetani
zikitoka kwa Yule joka na hizo ndizo Roho zitokazo kwa shetani zitendazo kazi
katika ulimwengu wa giza na kuleta shida na matatizo kwa watu wa Mungu.Lakini
leo tunazishinda kwa damu ya Yesu kabla hajaachama.Nyoka huyu ni nyoka ambae
amefunga maisha ya wengi.
(AYUBU 20:15) Amemeza mali nae atayatapika tena na Mungu atayatoa tumboni
mwake,kumbe Joka huyu anaweza kumeza mali,kazi,watoto,ndoa,mume wako na kila
kitu cha maisha yako.Na nyoka huyu anawatoto wake na hutenda kazi kama mama yao
na Nyoka huyu huweza kuvaa umbo na sura ya mtu yeyote na kutenda kazi laini
maandiko yanasema watashindana nasi lakini hawatashinda.Nyoka huyu kazi yakeni
kuchinja na kuharibu huduma na kazi ya
Mungu kiujumla,Nyoka huyu anaweza kuzuia
na kuharibu kabisa mipango yako ya kimaisha anaweza kukufunga usizae ,usipate
kazi ,usioe wa kuolewa,lakini leo tunamshinda kwa damu ya Yesuna tutakata
kichwa chake kabisa ili sisi tuwe huru na si kila binadamu unaemuona kwamba ni
binadamu wengine si binadamu wa kawaida bali ni pepo ndani ya mtu.Usiogope mtu
wa mungu walioupande wetu ni wengi kuliko walio upande wao nae atatusaidia na
kumshinda adui huyu anaeharibu maisha ya watu wamungu.