JPILI TAREHE 1/5/2016
SNP:PAUL JOSHUA
SOMO:TAA ILIYOZIMISHWA.
ZABURI
18:28 "Kwa kuwa wewe
unawasha taa yangu,Bwana wangu aniangazia giza langu.Huyu ni Daudi anasema
maneno haya na kumfurahia Mungu,Taa hii ni taa ya Rohoni ambayo taa hiyo
hukuangazia hatima ya maisha yako na pale unapokosa njia, Taa hii hukuangazia
njia".
MITHALI 20:20
"Amlaanie Babaye au
Mamae taa yake itazimika katika giza kuu,unapokuwa unamjibu baba yako ama mama
yako mzazi ulimwengu wa Roho ile taa mbayo mungu alikuwekea Mungu huiondoa na
Taa likizimika hakuna Maisha".
MITHALI
13:9 "Nuru ya
mwenye haki inang’aa gizani bali taa ya mtu mbaya itazimika.Kumbe taa ya mtu
inaweza kuzimika.Wachawi ama waganga huangalia ni nani mwenye taa na kutafuta
kuizima ili giza liingie na ndio maana kuna familia zingine walianza vizjuri
kiuchumi lakini baadae mambo yakaharibika ni kwa sababu taa ya familia hiyo
ilizimimwa na kuyaharibu maisha ya watu hawa kabisa"
2.SAMWELI
21:15 Basi kulikuwa
anavita kati ya Wafirist na Waislaeli; Daudi akashuka mpaka Gobu na watumishi
wake pamoja naye alipigana na Wafirist naye Daudi akaishiwa nguvu. naye
Ishi-benobu aliyekuwa mmojawapo wa warefai, ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa
shekeli mia tatu za shaba kwa uzani naye amejifungia upanga mpaya alijaribu
kumuua Daudi. Efueli akaanza kumtafuta Daudi ili amuue kwa sababu walijua Daudi
ndio aketaa ya Israeli,hata katika maisha tuliyonayo kuna watu wanakaa kwa
ajili ya kutafuta ni nani nguzo ya familia anae funga na kuomba lwa ajili ya
familia huyo ndie anaetafutwa ili wamuangamize,Lakini leo kwa jina la Yesu
tunazima mataa ya kichawi na waganga wa kienyeji ili tusonge mbele katika jina
la Yesu. Ukiona giza kwenye Ndoa yako,Masomo yako,Kazini hata katika biashara
yako kwako ujue taa imezimika.Lakini leo kwa damu ya Yesu tunaziwasha tena taa
zetu kwa jina la Yesu. Neno la Mungu ni taa ya miguu yetu na neno la Mungu
tunaliamuru leo liwe taa kwenye ndoa,kazi,biashara na hata katika masomo
yako.Kuna watu ambao walizimiwa taa zao tangu wakiwa ni wadogo na ndio maana
wanapitia kwenye mazingira magumu katika maisha yao na kuwa watu wa huzuni muda
wote na kuikosa furaha ya Maisha,Lakini leo tunakwenda kuiwasha taa hizo tena
na watu waanze kukuona tena na hakuna atakae zuia.Wachawi,waganga na wasoma
nyota wanakazi ya kuwaingiza watu kwenye gizana hapa ndipo maisha ya wengi
yaliharibika.
ISAYA 60:1 "Ondoka uangaze kwakuwa nuru yako imekuja,
na utukufu wa Bwana umekuzukia".
Ukiwa ndani ya Giza huwezi kuonekana,kabla hujalaumu watu jiulize taa
yangu inawaka au imezimika,ili uanze kushughurika na taa ili giza liondoke,Giza
ni mateso,shida,balaa ,nuksi,kulogwa,na mateso ya kila namna lakini leo Mungu
anakwenda kututoa kwenye giza hilo na mataifa wataijilia Nuru yako na Wafalme
watakuja kwako na kuifuata Nuru yako.Kuna baadhi ya vitu unashindwa kuvipata
kwa sababu taa yako haijawaka.Lkini mungu anasema ni kweli walikuzimia taa
lalkini leo Ta iliyozimwa inawaka tena,Taa ikiwaka ndoa yakoitastawi tena,taa
ikiwaka watu wanaanza kukuona na kwenye maisha yako kuonekana tena.Wachawi
wanakazi ya kuwakusanya watu na kuwaweka kwenye giza nene na la ajabu na
hawaoni ninaniatakae wasaidia,Lakini leo kwa jina la Yesu taa zao zinawaka tena
na giza litaondoka maishani mwako.
ISAYA 60:4 "Inua macho yako utazame pande zote wote
wanakusanyana wanakujia wewe wana wako wanakuja kutoka mbali na binti zako
watabebwa nyongani".
kumbe taa
ikiwaka unapata kibari na kuonekana mbele zawatu na Maisha huanza kukufuata
wewe,na utajiri wa mataifa utakuijilia wewe wataleta Dhahabu na uvumba,makundi
ya kelali watakufuata nanmi nitaitukuza nyumba ya Utukufu wangu,Taa ikiwa
utaanza kuonekana,hata mbele za watu utaonekna.
ISAYA 60:10 "Na wageni watajenga kuta zako na wafalme
wao watakuhudumu, maana katika ghadhabu yangu nalikupiga. lakini katika
upendeleo wangu nimekurehemu".
ZABURI
119:105 "Neno lako ni
Taa ya miguu yangu,na mwanga wa njia yangu,Neno la Mungu ni Taa na Mwanga mungu
akilituma humulika maisha yako".
2.SAMWELI
22:29 "Kwakuwa wewe
hu taa yangu na Bwana ataniangazia giza langu". kwenye giza Mungu anakuwa
ni taa kwa jina la Yesu,na leo tunaliondoa giza kwenye maisha yetu na kuwa huru
kabisa.