KESHO ILYOPINDISHWA

UFUFUO NA UZIMA KIGOMA

JUMAPILI TAR 15/5/2016
SOMO: KESHO ILIYOPINDISHWA
SNP: PAUL JOSHUA
Mungu anapomuumba mtu anampa mwanzo wake na mwisho wake. Anampa aanzie maisha ya chini lakini hatima yake iwe maisha mazuri anaweza akaanza na nyumba ya udongo hatima yake akamiliki gorofani, anaweza akaanzia kwenye magonjwa lakini kesho yake ni uzima, anaweza akawa masikini lakini hatima yake ni kumiliki utajili. Lakini shetani huwa anaweza kuiona kesho au hatima ya mtu na aakamua kuipindisha ili kesho yake ambayo anatakiwa amiliki isitimie, lakini lleo tunawatangazia wachawi wote tunawashinda kwa damu ya mwana kondoo.

WARUMI 8:29-30 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua  tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi; na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita na wale aliowaita akawahesabia haki na hao aliowahesabia haki akawatukuza.
Mungu alikuchagua tangu mbinguni uwe mtu fulani, uwe mchungaji, uwe tajiri, uwe na ndoa nzuri uwe na maisha mazuri; Mungu alikuchagua tangu asili, lakini shetani anapambana na kile ambacho Mungu alikipanga juu ya maisha yako. Shetani anaangalia mtu huyu amezaliwa lakini miaka hamsini au thelasini ijayo mbele atakuwa mtu Fulani;  ni kweli amezaliwa kijijini lakini mwisho wake ni kuishi marekani hakikisheni mnapindisha maisha yake aishie kwenye magonjwa. 

Wanasoma nyota yako na kujua Mungu amekupangia nini ni kweli ana kasi ya kumtumikia Mungu, hakikisheni mnamfunga; Lakini leo tunawatangazia wachawi wote kwamba tumepewa nguvu ya kushinda kwa jina la Yesu. Tunaye Yesu ambaye alishinda kifo na mauti, yawezekana ulianza kwa huzuni lakini utamaliza kwa kucheka hata Yesu alizaliwa kwenye nyumba ya fundi selemara lakini akaishia kuwa mfalme wa wafalme. Mungu huwa anaiandaa kesho ya mtu, na anapokuokoa lengo la kwanza la Mungu ni kumpeleka kwenye hatima ya maisha mazuri, hata kama ameanza vibaya lakini atamaliza vizuri kwa jina la Yesu.

AYUBU 8:5-7 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, na kumsihi huyo mwenyezi ukiwa wewe u safi na mwelekevu; hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako na kufanya makazi ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
Hata kama umeanza vibaya mwanzo wako umekuwa sio mzuri lakini BWANA anakuja kufanya makazi kufanikisha haki yako na hatima yako inaongezwa, kesho yako inakwenda kufanikiwa ule uchawi ulifanywa ju yako ili kupindisha kesho yako ili wakuingize kwenye huzuni tunaubomoa kwa jina la Yesu.

MATHAYO 2:1-2 Yesu alipozaliwa katika Bethlelehemu ya uyahudi, zamani za mfalme Herode tazama mamajusi wa mashariki walifika yerusalemu wakisema. Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa wayahudi? Kwa maana tuliona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumsujudia.
Mamajusi hawakupigiwa simu bali waliiona nyota ya Yesu wakajua kuwa huyu ni mfalme amezaliwa; wakaenda kumsujudia akiwa bado mchanga fedha zikaanza kuja, dhahabu zikaanza kuja, zawadi zikaanza kuja kumbe nyota iking’aa fedha zinakuja, zawadi zinakuja, dhahabu zinakuja nyota yako ing’ae leo kwa jina la Yesu.
Nyota ya Yesu ikaonekana akiwa mchanga, ingawa alizaliwa kwenye holi la ng’ombe lakini hatima yake akaishia kuwa mfalme; hata wewe usikate tama kwenye maisha yako nyota yako inangaa tena haijalishi umepitia nini kwenye maisha yako ingawa ulisoma shule bila hata viatu, au hata shule hujasoma lakini Mungu anakuinua tena kwa jina la Yesu.

Tunawatangazia adui zako ipo njia nyingine hata kama ulifeli mtihani, ipo njia nyingine hata kama hujasoma sana ipo njia nyingene ambayo haihitaji uwe umesoma sana bali inamhitaji roho mtakatifu. Yesu yupo kwaajili yako usivunjike moyo mwambie Yesu akuonyeshe njia ya kupita; yawezekana mchumba wako ulimsubili kwa muda wa miaka mingi lakini sasa amekwambia amepata mwingine, usiwe na wasiwasi mtazame Yesu. kila jambo lina kusudi la Mungu hata kama unapitia mateso ingawa Ayubu alipitia mateso lakini hakupenda apitie mateso, ndani ya mateso ya Ayubu kulikuwa na kusudi la Mungu.
Heri wewe unayekula ugali kwa tembele kila siku lakini nyumba yako ina amani kuliko nyumba ambayo wanakula pilau na kuku kila siku siku lakini nyumbani ni ngumi kila siku.

Kuna watu wengine wamepindishwa kona, wanajikuta wanafanya kazi ambayo siyo ya kwao mtu anajikuta alipanga awe Rubani lakini anaishia kuwa mama wa nyumbani, alitakiwa awe mbunge lakini anaishia  kuwa mpiga bodaboda na shetani amepindisha maisha ya watu kwa sababu aliona nyota zao. Wachawi wapo wanaweza kumloga mtu asisome shule, asizae watoto, asipate kazi wanapindisha kesho ya mtu na anajikuta anaishia kufanya kazi ambayo haipendi.
Kuna watu wengine kesho yao ilipindishwa kwa namna ya kupewa uchawi wakiwa wadogo au wakubwa, wengine wamejikuta wanaitwa wachawi ingawa hawalogi, wengine kuna kitu ambacho walipewa nyumbani kwenu yawezekana madawa, mahirizi yamebaki yanakutesa kwenye masha yako na mwisho wake yatakumaliza mwenyewe; kesho inakuwa imepindishwa hauwezi kufikia malengo ambayo Mungu aliyapanga kwenye maisha yako. Watoto wengine hatima ya maisha yao imepindishwa walitakiwa wawe shule lakini wanaishia kuloga, wengine walitakiwa wasonge mbele kwenye maisha yao yakini wanaishia kuloga.
Kuna mwingine alitakiwa awe muimbaji lakini kesho yake imepindishe, mwinginge alitakiwa afanye biashara kesho yake imepindishwa anajikuta anapitia maisha magumu ni kwa sababu wachawi waliona kesho yako, waliona hatima ya maisha yake wakaamua kuipindisha, lakini leo tunaangusha falme zao kwa jina la Yesu.