SOMO: UZAO ULIOLAANIWA

“UZAO ULIOLAANIWA”
SNP-PAUL JOSHUA
JUMAPILI YA TAREHE 7/8/2016
Watu wengi wana mateso lakini mateso hayo asilimia kubwa yameanzia kwenye asili ya kwao, kuna wengine wana asili ya mwanza,kibondo, kigoma, kasulu, manyovu nk. Ukifuatilia mateso mengi ambayo unapitia kwenye familia kuna mtu ambaye alipitia matatizo hayo kwenye familia. Kama kuna mtu ana matatizo Fulani yanaweza kutembea kwenye familia kizazi hadi kizazi.
MWANZO 12:1 BWANA akamwambia Abrahamu, Toka wewe katika nchi yako na jamaa zako, na nyumba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. Nami nitakufanya kuwa Taifa kubwa na kukubariki na kulikuza jina lako nawe uwe Baraka. Nami nitawabariki wakubarikio naye akulaaniye nitamlaani, na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mungu anamtenga Ibrahimu na ndugu zake wote ili afanye agizo nay eye, Mungu alikuwa anaandaa mazingira ili Yesu azaliwe kwenye uzao wa Ibrahimu.
MATHAYO 1:1 Kitabu cha ukoo wa Yesu kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Mungu akitaka kukubariki cha kwanza ni lazima akutenge na mauzauza ya ukoo, akutenge na dhambi ndio maana Mungu akumtoa Ibrahimu ili aende kwenye nchi nyingine.
Mungu akaanza ukoo mpya wa Ibrahimu, ukoo uliojitenga na ukoo wenye wachawi, magonjwa, laana. Mungu anaweza kulikuza jina lako hata kama umezaliwa kijijini, utajulikana maeneo yote, kumbe jina linaweza kukuzwa ulianza chini kwenye magonjwa, ulianza kwenye shida lakini BWANA akilikuza jina utamaliza mwenye heshima; kama Mungu alivyolikuza jina la Ibrahimu leo hii linajulikana kwenye mataifa yote.
Mwanzo wako siyo mwisho wako, kuanza vibaya haimaanishi kwamba utamaliza vibaya, wale walio kuzalau watakushangaa umefanikiwaje na kila mmoja atasema huyu ni ndugu yangu, hata Yule aliyekuloga atasema ni ndugu yangu, hata Yule aliyekutema mate atasema huyu ni ndugu yangu kwa maana BWANA atalikuza jina lako.
Mungu Mungu alianzisha uzao mpya wa Ibrahimu na akaweka agano naye akimwambia mataifa yote watabarikiwa kupitia yeye.
Kumbe Baraka yaweza kutembea uzao hadi uzao na ikasambaa kwenye uzao wote, kama vile Baraka ya Ibrahimu ipo hadi leo tumebarikiwa.
Na laana inaweza kutembea uzao hadi uzao unajikuta unapitia mateso, na magonjwa, mikosi laana, balaa, umaskini; kumbe yametoka kwenye familia yenu. unaweza ukawa kuna shida unapita ambayo imetokea kweye ukoo na imekuwa ikitembea kizazi hadi kizazi.
Mtu anaweza kurithi tatizo, anakuwa anasumbuliwa na magonjwa ambayo yameanzia kwao, kuna mtu mwingine ni kweli ameokoka lakini kuna vitu vinamsumbua ambavyo vimeanzia kwenye ukoo.
Kuna watu wengine wana vitu ambavyo waliachiwa na wazee wao ambavyo vinawatesa kwenye maisha yao; kuna kitu ambacho hukipendi kwenye maisha yako lakini kimekuja kutoka kwenye familia yenu, na leo tunakivunja kwa jina la Yesu.
Kama Baraka zinaweza kutembea kizazi hadi kizazi, hivyo hivyo na laana nazo zinaweza kutembea kizazi hadi kizazi. Kuna wengine wanajikuta wana roho za kuolewa na kuachika, shida inakuwa siyo wewe wala shida siyo mwanaume ila shida inakuwa imeanzia kwenye familia. Unaweza kurithi matatizo, magonjwa, laana, umaskini, roho ya kuoa na kuacha ambayo ukifuatilia inakuwa ilianzia kwa babu.
Kuna wengine wanajikuta wana roho ya kutokusoma maana mizimu inasema kwenye ukoo huu hakuna aliyesoma wewe unataka usome unaenda wapi; lakini leo nakutangazia familia yenu itakuwa wa kwanza kusoma shule. Watu mnakuwa mnaakili darasani lakini mnaishia njiani, mnatamani kusonga mbele lakini unashindwa shida inakuwa siyo wewe ila umezaliwa kwenye ukoo tata. Kazi inakuwa ni kutoka kuiponyoka mizimu na mashetani, na ukifanikiwa kutoka umefanikiwa.
Kuna wengine kwao kuna roho ya kifo, wanakuwa kila mwaka ni lazima wazike mtu ingawa wengine wanakuwa wameokoka. Huyo anakuwa ni shetani ambaye alikabidhiwa ukoo kwa masharti kila mwaka apewe mtu.
Kuna kitu ambacho familia imekwisha kukipokea kutoka kwenye familia, ambacho ni roho tayari wameshaipokea itakayotesa familia kwakuwa ni urithi kutoka kwenye ukoo.
Kwenye familia kunakuwa hakuna aliyefanikiwa sasa wewe unapojaribu kupiga hatua mizimu inakushikilia na kukurudisha nyuma kwa sababu kwenye ukoo wenu hakuna aliyefanikiwa, hakuna aliyejenga nyumba, hakuna aliyenunua hata Tv, hakuna hata aliyesoma shule, wala hakuna aliyewahi kuwa mchungaji.
Kuna familia zingine kuna wakala wa shetani ambaye anafanya biashara inakuwa kila anayezaliwa kwenye familia anauzwa kwa wachawi, mtu ambaye amezaliwa ana kitu anauzwa, anauza matumba ya uzazi anafanya biashara ya kuuza watu.
Yale ambayo unapita leo na wanao watapitia kama usipovunja na kuharibu.
ISAYA 57:3 Lakini ninyi karibuni hapa, enyi wana wa mwanamkwe mchawi, uzao wa mzinzi na kahaba.
Huu ni uzao ambao kuanzia babu alikuwa mzinzi, na hii inakuwa ni roho inatembea kwenye familia inatembea hadi kwenye familia. Ama familia hii inakuwa kuanzia bibi alikkuwa kahaba sasa roho hii inaendelea kwenye familia kwa wajukuu hadi kwa vitukuu. Ama uzao mwingine ni wa wachawi maana yake babu anapokaribia kufa anamchagua mtu wa kumrithisha uchawi wake.
Leo ni siku ya kuwafungua wote ambao wamefungwa na mizimu ya familia wamekuwa na magonjwa ya kurithi, laana za ukoo na mikosi, tunavunja kila balaa zilizotoka kwenye familia kwa jina la Yesu.
LikeShow more reactions