SOMO:
KUMWANGAMIZA
NYOKA NA UZAO
WAKE …na Pastor Paul Joshua
(KUMUUA NYOKA NAWATOTO WAKE WOTE)
Jumapili 17.08.2014
Mwanzo 3:1...
Hapo
tunamwona nyoka anaongea kumbe, si kila anayeongea si mwanadamu japo anasema
kama wanadamu.
Pia unaweza
kumuona mtu anasema na anatembea kama
mwanadamu kumbe ndani ni nyoka
Mathayo 3:7
Shetani/Nyoka
anaweza kuwa na uzao wake lakini kwa macho ya kawaida huwezi kujua chochote,
upo uzoa wa nyoka duniani unaoishi kama watu wa kawaida, na huyo nyoka amemeza mali nyingi za watu lakini
atazitapika.
Matendo 28:1-5
Nyoka
anaweza kujificha sehemu yoyote, anaweza kujificha kwenye ndoa yako, kazini
kwako, shuleni kwako hata kwenye biashara/mali zako, anaweza kuingia kwa siri.
Paulo alipowasha moto, kwaajili ya ule moto yule nyoka alitoka katika kuni
alizokuwa amekusanya Paulo; Tunaweza kumwangamiza nyoka
kwa kuuwasha moto wa Bwana Yesu katika maisha yetu.
Ufunuo wa Yohana 12:13-17
Nyoka
anaweza kutema mabaya ili usifanikiwe, anaweza kutengeza magumu katika maisha
yako ili uangamie.
Nyoka
anaweza kufanya vita katika maisha yako
-Mafarakano,
magonjwa, nyoka anaweza kuvii ngiza sehemu yoyote ya maisha ya mwanadamu.
Leo
tunang’oa mapando yote ambayo nyoka kayaingiza. Usimvumilie mzinzi,
msengenyaji, mtu wa kung’ang’ania madaraka, kujipandisha; washa moto ili waweze
kung’oka haraka sana.
Mbiguni
hakuna mzee wa kanisa wala potetial kwahiyo mwangalie sana mtu
anayeng’ang’ania madaraka au kupandishwa
cheo, hafai kabisa huyo ni nyoka! Mwashie moto haraka sana.
Nyoka
anaweza kuzonga-zonga kizazi cha mtu ili aweze kula mayai tumboni.
Ukitaka
samaki wakubwa nenda kwenye maji mengi, usiwaogope wachawi kwamaana shetani
ataleta vitisho vingi ili umwogope.