JUMAPILI TAREHE 15.11.2015
SOMO: KUVUNJA ROHO YA MAUTI
SNP: PAUL JOSHUA
Mauti ni roho inayosikia inayoongea inaweza kukaa sehemu yeyote au kutumwa sehemu yeyote.
UFUNUO WA YOHANA 6:8 “Nikaona na tazama farasi wa rangi ya kijivu jivu na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa , mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni kwa hayawani wa nchi”.
Kila jambo unaloliona katika maisha yako kuna sehemu limetokea
ZABURI 27:1-4 “BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu nimhofu nani? Watenda mabaya waliponikaribia wanile nyama yangu, watesi wangu na adui zangu walijikwaa wakaanguka. Jeshi lijapojipanga kupigana nami moyo wangu hautaogopa, vita vijaponitokea hata hapo nitatumaini. Neno moja nimelitaka kwa BWANA nalo ndilo nitakalolitafuta nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa BWANA na kutafakari hekaluni mwake”.
Royo ya mauti inasimamiwa na jini Makata na waganga wachawi wanalitumia kwaajili ya kuua watu na hii ndiyo siraha kubwa ya shetani lakini; Yesu alishinda kifo na mauti na mchana wa leo Yesu kristo aliye hai anakwenda kushinda tena. Walimsurubisha, wakamchoma mikuku wakamzika kaburini lakini siku ya tatu lile jiwe likatoka mlangoni kristo akafufuka na kushinda kifo na mauti.
Toa wazo kwamba kuna mchawi mmoja anakutafuta tambua kwamba kuna kikundi cha wachawi wamekusanyana wana vita na ndoa yako; ndio maana Daudi anasema Jeshi lijapojipanga kupigana nami moyo wangu hautaogopa. Tambua kwamba hupambani na adui au mchawi, mganga mmoja bali ni jeshi lakini BWANA anasema watapambana lakini hawatashinda.
ZABURI 116:3 “Kamba za mauti zilinizunguka , shida za kuzimu zilinipata naliona taabu na huzuni”.
Daudi anasema kamba za mauti zilimzunguka maana unaona kila sehemu umezungukwa unaona kamba za kifo unatibu ugonjwa mwaka mzima unaambiwa muda wowote unaweza kufa zinaweza zikawa kamba za ukimwi, kansa,kisukari madonda ya tumbo, lakini mchana wa leo tunazikata kamba zote zilizokuzunguka kwa jina la Yesu. Ukifungwa na kamba hizi za kuzima matatizo na shida hayaiishi kwako maana umefungwa na kamba na mauti na shida zinaanza zkuja. Unateseka hadi unasema bora nife tu maisha magumu huna hata hela kumbe zinakuwa ni kamba za mauti na kuzimu zimekufunga.
Mtu anaweza kuzungukwa na kamba pamoja na mitego ya mauti inakuwa imetegwa kwaajili yake, lakini Bwana amesema atatuokoa na mtego wa mwindaji.
ZABURI 18:4-5 “Kamba za mauti zilinizunguka mafuriko ya uovu yakanitia hofu, kamba za kuzimu zilinizunguka mitego ya mauti ikanikabili”.
2SAMWELI 22:6 “Kamba za kuzimu zilinizunguka mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimlilia BWANA, naama nikamlalamikia Mungu wangu”.
Roho ya mauti ambayo inasimamiwa na jini makata anaweza kutumwa na kukaa kwenye moyo mtu na kusababisha presha ya kupanda au kushuka na jini huyo anaambiwa akubane moyo hadi mtu anakosa hewa na anakufa. Lakini Mungu wetu anaweza hakuna jambo gumu la kumshinda BWANA na mchana wa leo tunakwenda kushinda kwa jina la Yesu.
Hili jini laweza kukaa kwenye damu na kunyonya damu na kuambiwa hakikisha kila akipima aambiwe ameasilika ana Ukimwi, kumbe kuna wachawi wametengeneza ugonjwa. Wachawi wanaweza kutengeneza ugonjwa au tatizo na kumtumia mtu ili yampate, Roho ya mauti pia yaweza kutegwa barabarani inaambiwa nenda kakae barabarani msubilie anakuja na uidondoshe gari mtaloni.
Roho ya mauti inaweza kutegwa kwenye chakula ndio maana usipende kula hovyo hovyo kwa watu kila unachopewa unakula tu unaambiwa chukua mpendwa, tena cha kutegwa ni kitamu kweli kweli ndio maana uwe makini na chochote unachokula. Kabla haujala kitu chochote kwanza kitakase hata kimoyo moyo sema nakitakasa kwa damu ya Yesu.
Roho ya mauti inaweza kumwita mtu ni roho huyu na hata tunaposema anasikia anakwambia chukua gari kimbiza gari unajikuta unadondoka mtaloni, wachawi wanatumia roho ya mauti ili waweze kula nyama za watu.
Ukiona mwanao anaugua magonjwa yasiyopona unajikuta anakonda tu jua kwamba ana roho ya mauti maana wachawi wanapenda kula nyama za watoto na wanaweza wakakubadilishia mtoto wakakupa mdoli. Kama kwenye familia yenu kuna mchawi na anatakiwa kila mwezi atoe sadaka na anaangalia amtoe nani anaamua kutuma roho ya mauti.
Utajuaje kama roho ya mauti inakufuata. Utaanza kuwaza kufa tu unaiingiziwa hofu ya mauti, unawaza huna hela ni bora ufe tu. Ukiona unalala lakini moyo wako unakaa una mashaka mashaka amka uombe. Unapoota usiku kwamba kuna nyoka amekugonga hiyo ni roho ya mauti inakuwa ni sumu imeingizwa kwenye mwili wako.
ZABURI 55:4 “Moyo wangu unaumia ndani yangu, na hofu za mauti zimeniangukia. Hofu na tetemeko limenijia na hofu kubwa imenifunikiza”.
Mauti na kuzimu ni mtu na rafiki yake, mauti ikishachukua inampa kuzimu ndio maana kuna watu wamefichwa ziwa Tanganyika, maana mauti ikiingia kuzimu inakuwa na nguvu.