SOMO:ROHO YA KUKATALIWA _ SNP Paul.Joshua



SOMO LA LEO 31.08.2014
 ROHO YA KUKATALIWA na SNP Paul Joshua

Utangulizi:

Jambo la kwanza linalomfanya mtu afanikiwe kwenye maisha, ni kukubalika kila sehemu. Na jamii ikisema kama hatakiwi huyu, huwezi kwenda kokote.” Ukimwona mtu kaolewa, kwanza alikubalika”
Esta alikuwa ni binti mdogo tena yatima asiye na baba wala mama wala hukujiremba, lakini ndiye alikubalika machoni pa Mfalme Modekai tena alikuwa na kibali kutoka kwa Bwana,alikubalika kwa kila aliyemuona.
Kuna watu ambao wananyota nzuri lakini wachawi wamewawekea roho ya kukataliwa kwa kila atakaye muona aseme cha nini hiki nacho; kazini kwako, masomoni, h ata mume wako wa ndoa asikupende kwakuwa nyota yako imekwisha kufnikwa.
Ø Isaya 53:1
Kuna uwezekano watu kukudharau na kukataliwa hata wasikupende
Katika ndoa au familia walio wengi huanza vizuri ila shetani hutaka kusambartisha upendo/amani ya watu hao kwa kuwaingizia roho ya kukataliwa yaani kwa kila mmoja amwone mwenzake kana kwamba si chochote. Mfano kwa wanandoa mke au mume huanza kujuta kwanini aliolewa/alioa na mtu kama huyu ambapomwanzo mlipendana vizuri; hali hiyo ni shetani kawaigizia roho ya kukataliwa kwenye ndoa yako.
Ø Ezekieli 16: 1
Shetani ameanza kuwashika watu tangu wakiwa wadogo, ukubwani ni matokeo tu. Yawezekana kabisa kipindi cha ujauzito wako, baba yako alikana mimba (alikukataa) tangu ukiwa tumboni hivyo mama akaingiwa na uchungu na kuanza kuchukia ujauzito alionao. Kinachotokea hapo ni roho ya kukataliwa inakuja kwako maana baada ya baba yako kukukataa, mama yako pia alikukataa.
Hata baada ya kuzaliwa mama anaweza kukukataa na kukuacha mtaroni kwakuwa aliyempa ujauzito huo, kakataa kuhudumia mtoto.
Baba au mama kama mwanao humpendi, unamchimbia shimo mwanao. Kwa hiyo, kama unajua unamtoto mahali Fulani ulizaa na mtu kasha umkana, leo mtafute  kwa Jina la Yesu.

Ø Kupenda kukaa peke yako  ni dalili moja wapo ya mtu mwenye roho ya kukataliwa.

Leo hata kama watu wamekukataa, jifunze kumngoja BWANA kwani waliokukataa ni watu na siyo BWANA.
Mama usimkatae mwanao kwa kuwa mume wako kaukana ujauzito;  Tulia na BWANA kwani aliyemkana ni mwanadamu na si BWANA.
Pia mabinti mnaosoma, tulieni katika masomo yenu msijihusishe kabisa na uzinzi kwani endapo utapata ujauzito ni vigumu baba wa mtoto kukiri kama ni ujauziti wake kwa kuogopa atachukuliwa hatua za kisheria; Nawe utataka kuutoa ujauzito huo kwa kuogopa wazazi na jamii kwamba utaonekanaje.
Acha dhambi, subiri wakati wa BWANA.

Pengine leo maisha ya mwanao ni magumu na yamekuwa ya kutangatanga siku zote kwasababu ulimkataa kwa kutaka kutoa mimba , maana yake ulitaka kumuua tangu akiwa tumboni.

Dalili za mtu mwenye roho ya kukataliwa:-
Ø Kudharauliwa na watu
Ø Kutojikubali (kutojiamini)
Ø Kutokubalika kila sehemu (kukosa msaada wowote)
Ø Mtu wa huzuni_ mara nyingi hupenda kukaa peke yake. (kuwa na mawazo ya kujiua)

Leo kila roho ya kukataliwa iliyowekwa kwenye maisha ya watu inang’oka kwa Jina la Yesu.
Jifunze kuwakubali watu, penda kuwasifia wenzako; pia anza kujiamini, jikubali, ili uishinde roho ya kukataliwa kwenye maisha yako.
Ukitaka Mungu akubariki, jifunze kuwabariki wenzako nawe Mungu atakubariki. Mwambie Yesu nimekufuata wewe nisiabike milele.