SOMO: KUSUDI LA MUNGU LILICHELEWESHWA

JUMAPILI TAREHE 8.11.2015
SOMO: KUSUDI LA MUNGU LILICHELEWESHWA
SNP: PAUL JOSHUA
AYUBU 42:2 “Najua yakuwa waweza kufanya mambo yote, Na makusudi yako hayawezi kuzuilika”.
Mungu akikusudia jambo hakuna wa kuzuia bali laweza kucheleweshwa, kila aliyeokolea kuna kusudi la Mungu maana hujaokolewa ili upone tu bali kuna makusundi ya Mungu na yote ambayo BWANA amekusudia kwako lazima yatimie.
ISAYA 14:24, 26 “BWANA wa majeshi ameapa, akisema Hakika yangu kama vile nilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa na kama nilivyokusudia ndivyo itakavyotokea…. Hilo ndilo kusudid lililo kusudiwa duniani mwote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote”.
Kama Mungu amekusudia kutenda jambo juu ya Tanzania na familia yako hakuna wa kuzuia ni lazima kitimie, Mungu siyo mtu usimfananishe na wanadamu anasema yeye siyo mwanadamu hata aseme uongo wala siyo mwanadamu hata ajute, yeye ni Mungu jehova halinganishwi na chocho. Haijalishi unapitia nini leo kama Mungu amesema kitu juu yako ni lazima kitimie kama Mungu akisema utapita pale hata uone kuna jiwe linazuia utapita tu. Mungu akisema utapata mtoto hata kama ukae miaka mingi ahadi ya Mungu iko pale pale, hata kama wakuloge hutakufa ni lazima kusudi la BWANA litimie.
Wale wote ambao Mungu alikusudia kuwainu shetani alitangulia kuwafunga, katika biblia watu ambao walifanya mambo makubwa walikuwa wamefungwa. Tukiangalia Sara alikuwa amefungwa asipate mtoto shetani alijua kwenye tumbo hili kuna taifa la Israeli akaamua kumfunga. Shetani hana shida na wewe ana shida na kusudi la Mungu maana yeye anaangalia na kujua huyu mama Mungu anataka kumtumia. Hata kama wanakuloga wambie wanapoteza muda hawawezi kuzuia kusudi la BWANA ingawa wewe mwenyewe hujijui lakini una kitu cha ajabu maana BWANA ametuchagua sisi tuhubili habari njema dunia nziwa wasikie saa ya ufufuo na uzima vipofu waone matasa wazae katika jina la Yesu kristo.
Wewe Mungu amekuchagua ameona kitu ndani yako ndio maana shetani hakupi nafasi anajua akikupa nafasi familia yako imekombolewa unatakiwa kusonga mbele hufi leo wala kesho hadi kusudi la BWANA litimie. Unaweza kupewa na mtu ushauri mzuri lakini ukawa siyo kusudi la Mungu kama tunavyoona Sara alipomwambia mumewe Ibrahimu atembee na mjakazi wake ili apate mtoto, huu ulikuwa ni ushauri mzuri lakini ulikuwa siyo kusudi la Mungu. Lakini kusudi la BWANA lilipotimia Sara akapata mtoto nakutia moyo hata wewe hujachelewa Mungu anakwenda kutimiza kusudi lake haijalishi una umri gani BWANA hachelewi kutimiza ahadi yake. Tunapojifunza kwa Ayubu aliendelea kumtegemea BWANA pamoja na kupitia mateso makubwa alijua tu mtetezi wangu yupo kwa wakati wake atatimiza kusudi lake.
Kwenye vitu ambavyo unatakiwa kujifunza ni kwamba Mungu hachelewi wala hawahi bali Mungu anakwenda kuwashangaza adui zako watashangaa hawakutegemea upate mtoto ama uendeshe gari lakini watashuhudia wakiona Mungu amekubaliki na kusudi lake limitimia kwako.
1SAMWEL 1:1, 10, 20 Palikuwa na mtu mmoja wa Rma, msufi wan chi ya milima milima ya Efraimu jina lake akiitwa Elkana mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, mwefraimu. Naye alikuwa na wake wawili jinalake mmoja akiitwa Hana na jina lake wa pili aliitwa Penina naye huyo Penina alikuwa na watoto lakini Hana hakuwana watoto. Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka ili kuabudu na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika shilo na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi makuhani wa BWANA walikuwako huko….Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake akamwomba BWANA akalia sana, akaweka nadhiri akisema Ee BWANA wa majeshi ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako na kunikumbuka wala usinisahau mimi mjakazi wako na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume. Ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. Ikawa wakati ulipowadia Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanaume akamwita jina lake Samweli akisema kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.
Kuna watu wanapitia matatizo lakini hawajui ni kwanini lakini tatizo ni kwa sababau wewe ni chaguo la BWANA na kuna kusudi ambalo Mungu amelipanga juu ya maisha yako.
MATENDO YA MITUME 27:24-25 Akaniambia, usiogope Puulo huna budi kusimama mbele ya kaisari tena BWANA amekupa watu wote wanaosafiri. Basi wanaume changamkeni kwa sababu namwamini Mungu ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.
Ukitembea na mtu ambaye ni kusudi la BWANA hautazama kwa jina la Yesu shetani anaweza kukuzungusha ukapitia shida mbali mbali lakini Mungu anakwenda kutimiza kusudi lake.
YONA 1:1-4,  Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai kusema ondoka uende Ninawi mji ule mkubwa ukapige kelele juu yake kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi apate kujiepusha na uso wa BWANA akatelemka hata Yafa akaona merikebu inayokwenda Tarshishi basi akatoa nauli akapanda merikebu aende pamoja noao Tarshishi ajiepushe na uso wa BWANA. Lakini BWANA alituma upepo mkuu baharini ikawa tufani kubwa baharini hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika…… wakapiga kura na kura ikamwangukia Yona ndipo wakamtupa baharini na akamezwa na samaki Akaka kwa siku tatu huku akiwa anaomba ndani ya tumbo la samaki akitubu mbele za Mungu.
Kile ambacho BWANA amepanga akutendee lazima kitimie, kile ambacho BWANA amepanga akitimize juu ya maisha yako ni lazima kitimie kwa jina la Yesu. Unaweza ukapitia mambo magumu katika maisha yako lakini mwisho wake kusudi la BWANA litatimia. Jifunze kutokukimbia kazi ya BWANA yakupasa kutimiza yote ambayo BWANA amekuamuru uyatende kwaajili ya utukufu wa jina lake. Kuna sehemu ambapo shetani anakuchelewesha kwenye maisha yako lakini shetani kwenye ulimwengu wa roho anapambana kuhakikisha anakukatisha taamaa ili ushangae mbona BWANA ameniahidi kupata mtoto lakini hadi leo sijapata, kuna watu ambao wamepangiwa vitu vifanyike katika maisha yako unapitia mashimo mengi kuna kitu ambacho shetani amekiona kwamba wakikuachia hakika kama akikuachia ufanikiwe ni lazima familia yenu ifanikiwe.
Mungu huwa anachagua mtu mmoja katika familia ambaye Mungu alimchagua tangu tumboni mwa mama yake anaweka kusudi lake na kupitia huyo wengine wapate neema na kufunguliwa, katika familia Baraka huwa zinabebwa na mtu mmoja Mungu anaweka neema ya wokovu anamfanya kuwa Baraka kwenye familia hata kwa ndugu kwenye mkoa hata katika nchi. Shetani sasa anaona tangu akiwa mdogo anapitia misukosuko mingi anaweza asisome anaweza akakaa gerezani au akawa mlevi hayo yote shetani anayafanya ili kusudi la BWANA lisitimie. Shetani anakuwa ameona huyu mtoto amewekwa ili kuwa msaada wa familia anamfanya mtoto huyo adharaulike katika familia anamuwahi mapema na kumfunga. Leo hii watu wanakuita masikini lakini Mungu anasema wewe ni tajiri, walimwita Yesu amechanganyikiwa lakini Mungu alimwita ni mwokozi wa ulimwengu, watu wanakuita ni tasa lakini Mungu anakuita wewe ni Mama wa mataifa Mungu ana kazi na wewe ndio maana hajaruhusu ufe mapema anatamani watu wamtukuze kupitia wewe ndio maana kama kulogwa ulilogwa sana lakini ulitoka salama, saa zingine mama alikusudia kutoa mimba Mungu akasema huyu nina kazi na yeye. Shetani anaweza kuruhusiwa auguse mwili wako lakini siyo roho yako. Mungu anataka akurudishe kwenye hatima ya maisha yako kwa jina la Yesu kristo.
Kuna ndoto nzuri ambazo Mungu alisema na wewe au kuna vitu ambavyo Mungu alisema na wewe ni lazima vitimie kwa jina la Yesu. Kila aliyeokolewa kuna sehemu Mungu anakupeleka usijali kama unapitia shinda mbali mbali umeanza ukiwa mgonjwa japokuwa mwanzo wako umekuwa wa matese, mwanzo wako umekuwa wa kilio lakini adui zako watakusheshimu maana BWANA ameweka kitu ndani yako.