JUMAPILI TAREHE 11 OCTOBA, 2015
SOMO: KUMTAMBUA JINI ALIYEVAA UMBO LA BINADAMU.
SNP: PAUL JOSHUA

Ufunuo 12:7-12 “Kulikuwa na vita mbinguni, Michael na malaika zake wakapigana na Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake nao hawakushinda wala mahali pao hapakuoneakana tena mbinguni; Yule joka akatupwa Yule mkubwa nyoka wa zamani. Aitwae ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote akutupwa hata nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema sasa kumekuwa wokovu na nguvu ya ufalme wa Mungu wetu na mamlaka ya kristo wake, kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakie mbele za Mungu wetu mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo na kwa neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. kwahiyo shangilieni enyi mbingu nanyi mkaao humo ole wan chi na bahari kwa maana Yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu”.
Shetani ni roho, Mungu naye ni roho, malaika wa giza na malaika wa nuru nao no roho. Na sifa ya roho huweza kuvaaa umbo lolote. Unatakiwa ujue ya kuwa unapopambana sana katika umbo la rohoni huwa anahama katika umbo la rohoni na kuja katika umbo la mwilini, yaani anavaa mwili na kutenda kazi akiwa na mwili, na anauwezo wa kuvaa umbo lolote. Anaweza kuwa mdudu, mnyama, binadamu ama ndege.
Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwa na neno… naye neno huyu akafanyika mwili akakaa kwetu, alikuja kwake wala walio wake hawakumpokea bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu ndio wale waliaminio jina lake”.
huyo mwanzao alikuwa kwa Mungu na vitu vyote vilifanyika katika yeye hakuna kitu ambacho kilifanyika bila yeye. Ndani ni neno lakini nje ni mwili. Neno la weza kuvaachochote. Neno laweza kuvaa uponyaji, pesa.
Tunaona ya kuwa hapo mwanzo kulikuwa na neno, huyu alikuwa ni neno na wala hakuwa na umbo lolote. Hivo akachukua mwili akazaliwa na Mariam, kumbe sio kila anayezaliwa ni mtu. Huyu alikuwa mtoto lakini kumbe hakuwa mtu. Hivo tambua ya kuwa si kila unayemuona ni mtu wa kawaida. Kuna wengine wametoka mbinguni na wengine wametoka kuzimu.  Hivo lazima wale wa shimoni tuwarudishe shimoni. Uzao wa shimoni umejichanganya na uzao wa mbinguni, hivyo lazima tufanye kazi ya kutenga wa mbinguni na wa shimoni.

Sio kila anayezaliwa na mwanadamu ni binadamu, Kuna watu wametoka mbinguni kuja kuifanya kazi ya BWANA kama vile Yesu kristo alipozaliwa alikuwa siyo mwanadamu wa kawaida lakini alikuwa amekuja ili kufanya kazi ya BWANA. Hivyo ni vizuri utambue ya kuwa tumechanganyika, kuna wati wa mbinguni na wengine ni wa kuzimu. Yesu alikuja kwao walio wake nao hawakumjua kwakuwa alivaa mwili hivyo wakamuona ni mtu wakawaida kabisa, hawakumtambua ya kuwa yeye ndiye mkombozi wa ulimwengu.
Mwanzo 18:1-5 BWANA akamtokea Ibrahimu katika mialoni ya mamre alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona na tazama watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema akainama mpaka nchi. Akasema BWANA wangu kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yalete basi maji kidogo mkanawe miguu mkapumnzike chini ya mti huu name nitaleta chakula kidogo mkaburudishe moyo mwendelee iwapo mmemjia mtumishi wenu, wakasema haya fanya kama ulivyosema.
Kuna watu wanatembea au wengine umefanya nao biashara nao lakini hawakuwa watu. Tunaona ya kuwa wale watu walikula kwa Ibrahimu, sio kila anayetembea au anayekula ni mtu wengine sio watu wanaweza wakawa wamevaa sura tu. Kumbe Mungu anaweza kuvaa sura ya binadamu, Mungu anaweza kuvaa umbo lolote ndio maana anamajina mengi. Anaitwa moto kwakuwa anaweza kuwa moto, anaitwa maji kwakuwa anaweza kuwa maji, anaitwa jiwe kuu la pembeni kwakuwa anaweza kuwa jiwe, anaitwa simba kwa kuwa anaweza kuwa simba. Mungu anaweza kuvaa umbo lolote analotaka, unaweza ukawa rafiki na mtu kumbe ni Mungu, ukaishi naye kumbe ni Mungu na baada ya muda humuoni.
Mwanzo 32:1-2 Yakobo akashika njia yake na malaika wa Mungu wakakutana naye,  Naye Yakobo alipowaona alisema hili ni jeshi la Mungu akaita mahali pale mahanaimu
Yakobo aliwaona malaika sio rohoni bali mwilini. Aliliona jeshi, ndio maana usiogope maana kunaulinzi mkubwa kwaajili yako. Malaika wa Mungu wanaweza kuvaa umbo lolote ili kufanya kazi yake.

Yoshua 5:13-15 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa yeriko akavua macho yake akaangalia na tazama mtu mume amesimama kumkabiri mbele yake naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake. Yoshua akamwendea akamwambia je wewe u upande wetu au upande wa adui zetu? Akasema la lakini nimekuja sasa nili amiri jeshi wa jeshi la BWANA Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi naye akasujudu akamwuliza BWANA wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la BWANA akamwambia Yoshua vua vitu vyako miguuni mwako kwa maana mahali hapo usimamapo ni patakatifu Yoshua akafanya hivyo.
Yoshua alimuona mtu naye akamuuliza ya kuwa yu upande wao ama la! Naye akamwambia yakuwa yeye ni amili jeshi wa jeshi la BWANA. Yule haukwa mtu wa kawaida , bali ni Mungu aliyekuja kama binadamu ili aifanye kazi yake.
Kuna jeshi kutoka mbinguni limevaa sura ya binadamu na kuna jeshi kutoka kuzimu limetoka kuzimu, yote yanaipigania dunia. Shetani katuma watu wake na Mungu katuma watu wake.
Tuangalie juu ya somo letu. Vifungo vingi vinatokana na majini.Majini nayo yanaweza kuvaa maumbo yoyote na yakafanya kazi. Hivo wanaweza kuvaa umbo la binadamu na ukaishi nao kabuisa. Wanaweza kuzaa ama kuzalisha. Mashetani hawa wanaweza kuoa kabisa na wakawa na familia zao. Na hawa ndio wezi wa nyota za watu. Kila mwenye kitu kikubwa majini yalimuingia. Na hawa ndio wanatumika sana na waganga wa kienyeji, unaambiwa ukitaka utajiri tutakupa jinni fulanihawa majini hawana kitu isipokuwa wanatumia nyota za watu.
Mambo ya walawi 17:7 Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao kizazi baada ya kizazi.
Hawa ndugu walitoa sadaka kwa majini na kufanya uasherati nao na kuna wengine wamejikuta wamefanya uasherati na majini bila kujua wanajikuta wameungamanishwa na roho za majini. Wengine wamezaa na mashetani na wako kuzimu wamekuwa malikia wa kuzimu. Kuna kitu ambacho shetani anajiandaa kufanya kwako akiwa amevaa sura ya mtu ili uje useme ni mtu Fulani maana anatenda kazi akiwa amevaa sura ya mwanadamu ana sura kama ya rafiki. Majini na mashetani wanaweza wakaja kwako wakiwa wamevaa sura za watu na wanaanza kukuharibia maisha yako