SOMO LA LEO_TAREHE 15/3/2015_NATUVUKE TWENDE NG’AMBO:SNP
PAUL JOSHUA.
Maisha ya mtu yanaanza na zero na baada ya hapo Mungu
anakuinua. Kila aliyefanikiwa ameanza na sifuri na baada ya hapo anaingia 1,2,3
mpaka mamia, kuhama pointi moja kwenda sehemu nyingine yahitaji kupambana.
Kuna watu wengi wameishia kwenye mbili au tatu ya maisha na
wachawi wamembana ili asihame, wachawi walikubanana ukikaa hatua moja na adui
yako hatakuheshimu, lazima uvuke ng’ambo adui yako akuheshimu, lazima uwe juu
ya adui zako ili wakuheshimu.
Leo Yesu anasema lazima tuvuke twende ng’ambo ya maisha yetu
Yohana 6:15 -18
Wanafunzi walipoanza kuvuka upepo ukaanza na mawimbi
yakaanza, kabla ya hapo hapakuwa na upepo na hali ilikuwa shwari, kabla
hujaanza kuinuliwa hali inakuwa shwari lakini unapoanza kuinuliwa hali
inachafuka
Luka 8:23 Kila Yesu alipotaka kuvuka upepo ulikuwa unavuma.ukiona
misukosuko Imeinuka ujue unataka kuvuka, ukiona shwari ujue si shwari hivo
jitahidi upate changamoto ili
wakurahisishie safari yako,adui wakiinuka kama ulikuwa huombi utaanza kuomba ,
kufunga, kunena kwa lugha na kumtafuta Mungu.chura anamwendo wa pole pole
lakini ukiamua kumpiga teke unamsogeza kwenye hatima yake japo atakuwa na
maumivu, wanakuchezea sana lakini ndio wanakusukuma kwenye hatima yako . kama
huna mtu wakukusogeza mbele basi mtafute,
kama huna adui wakukuonea wivu ili akuseme nakukufanya ukazane kusogea kwenye
hatima yako basi hakikisha unafanya jambo ambalo litainua watu watakao kusukuma
na kusonga mbele.
Kila mtu akianza kuvuka lazima vikwazo viinuke, hata kazini
kwako utapata matatizo ,utasemwa, utachongewa, na kila aina yavikwazo
utawekewa. Ukiona hivo ujue umeanza kuvuka hivo weka bidii katika kupambana
maana adui zako wanafanya juhudi kuhakikisha huvuki.
Ifikie hatua adui zako wabaki chini yako, kataa kubaki
level/ nafasi moja na adui yako. Usipende
kumsema mtu,mtu akikusema wewe timua vumbi.
Kuna watu wana neema ya kuvuka lakini wameshikiliwa na
wachawi , au kwenye ukoo kuna kigagula anawazuia wasivuke,kila ukitaka kuvuka
unakwama.
1 wakorintho 16:9 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa
kufaa sana na wako wengi wanipingao. Kama una mlango mkubwa wakufaa sana
kwanini huvuki? Huvuki kwasababu wapo wengi wakupingao.
Isaya 60:11- - , Kila mtu ana mlango wake, kazi ya malango
ni kukuletea utajiri wa mataifa na kukuingizia Baraka , sasa wapingao hujiinua
na kupinga malango yako.
Kuna malaika wa nuru na malaika wa giza na kazi zao
nikusababisha mabaya au mazuri yakutokee. Malaika wagiza wanasababisha watu
wateseke , waugue , wafukuzwe kazi,. Unateseka lakini hujui kwanini, kwasababu
anayekusababishia kajificha kwenye kona iitwayo ulimwengu wa roho.
BARIKIWA.