SOMO LA LEO_ TAREHE 8/3/2015_FUMBO
LA ROHONI: SNP PAUL JOSHUA
Ulimwengu wa roho ni bayana na
ulimwengu wa roho ni harisi, wachawi wanafanikiwa kuwaroga watu kwakuwa
wanawaroga wakiwa wamejificha. Unaweza ukaota ndoto kuwa unafukuzwa na mbwa
kumbe sio mbwa.
Ndio maana wachawi wanaweza kumtesa
mtu hata miaka kumi na asiwajue. Adui yako ukishamgundua tu umemmaliza. Leo
tunaziweka wazi sura za watesi wetu, tuwajue kwa maumbo yao hata kama watakuja
namaumbo tofauti au wamevaa sura za paka
au mbwa.
Yoshua 5:13 Yoshua alimuona Mungu kama mtu, mwanajeshi aliyevaa gwanda za
jeshi, huyu hakuwa malaika kwani biblia inatukataza kuwasujudia malaika, hivo
Yoshua aligundua kuwa Yule alikuwa ni Mungu ndio maana akapomoka kiuso uso hata
nchi akasujudu.
Marko 16:12 wakati Yesu alipofufuka
mariam Magdalena hakuweza kumtambua kwakuwa alikuwa amevaa sura nyingine, na
kwa maana hiyo mariam alizani anaongea na mtunza bustani. Mtu yeyote akiwa
katika roho anaweza kuvaa sura yoyote. Wachawi
wanauwezo wakuvaa umbo la mnyama yoyote au kitu chochote wanapokuwa rohoni.
Ufunuo 1:9-16 Yohana anamuelezea
Yesu namna alivyo muona,
Shetani anafanya kazi yakuwa funga
watu akiwa katika anina mbili,
1. Anaweza
kumfunga mtu asimtambue hata kama ni mme wako au mke wako.
2. Akija
anakuja na umbo tofauti yaani kama panya, mjusi, popo, nyoka n.k
Watu wanasema adui wa kwanza ni
Yule wanyumbani kwake, nakumbuka wanyumbani kwako hawezi kuja na maumbo yao
halisi. Unaona ni mbwa kabisa kumbe ni binadamu kabisa, hii ndio siraha ambayo
shetani anaitumia sana. Na watu wanamna hii huwezi kuwajuwa maana wanakuonesha
upendo wa ajabu , kwakuwa wanajua kuwa upendo huficha mambo. Unaona mtu
anakusaidia sana ukadhani anamapenzi na wewe, je unauhakika kuwa msaada huo ni
waki-Mungu? Msaada mwingine ni kwaajili ya kuficha ubaya ili wakumalizevizuri.
Hata Mungu anaweza kuvaa umbo
lolote kumsaidia mtu, Mungu alijigeuza na kuvaa umbo la kunguru wakati ule wa
Eliya mtishibi. Ukizingatia kunguru ni mroho sana wa nyama inawezekanaje
kunguru aifikishe nyama salama! Kwakuwa Mungu ni roho hivo anauwezo wakuvaa
sura yoyote.
Ufunuo 2:24
Ufunuo 13:11 joka lilivaa sura
mfano wa mwanakondoo
Ufunuo 16:13 roho tatu za uchafu
zinazofanana na vyura.
Fumbo la roho watu wengi hawalijui na wala hawaelewi
namna ulimwengu wa roho unavyofanya kazi na kwakuwa hawajui adui anawatesa.Leo
tunawavisha maumbo yao halisi adui zetu wote wanaokuja kwa maumbo
tofautitofauti, tutawatambua kwa sura zao natutawateketeza kwa damu ya
mwanakondoo.