SOMO LA JUMAPILI-TAREHE 22/2/2015_KUNA KUINUKA TENA: SNP PAUL JOSHUA
Ayubu 22:28 nawe ukikusudia neno litathibitika kwako, na mwanga
utaziangazia njia zako, hapo watakapo kuangusha utasema kunakuinuka
tena, naye mnyenyekevu Mungu atamuokoa.
Ayubu anasema hivo kwa maana
anajua kuwa kuna kuinuka tena, Ayubu alianguka lakini Mungu alimuinua
tena. Ni kweli kuna kuanguka lakini utainuka tena.
Inawezekana umeteleza , katika ulimwengu wa roho wamekuwekea utelezi,
Kila unayemuona amepanda amepandishwa,
Ndani ya moyo wako unakitu ambacho Munguamekupa kitakachokupandisha juu, lakini wapo wasukumao wanaotaka kukuangusha chini.
Zaburi 118:13 ulinisukuma sana ili nianguke lakini bwana alinisaidia,
wanasukuma ndoa yako, elimu yako maisha yako, wengi wanasema muacheni tu
tuone, kazi sio kuanza kitu lakini skazi ni kumaliza kitu, mtu anaanza
kufuga kuku ukaja ugonjwa ukakuangusha na kukurudisha nyuma, wewe unaona
kama ugonjwa kumbe nyuma kuna mkono wa shetani.
Kila sehemu wapo waangushao, inawezekena shangazi, babu, mjomba lakini waambie utainuka tena.
Mtoto wako aliyeacha masomo angekusaidia, hakuna mtu anayechukia masomo
ila unanuiziwa roho ya kuacha, hakuna mtu anayechukia mambo magumu ila
ananuiziwa roho ya kuacha na anapokuja kutaharuki muda ulishakwenda ndio
maana majuto ni mjukuu.
Kila unapojenga wapo wanaobomoa, mbomoaji hatoki mbali bali anatoka ndani ya familia yako
Mika 4:6… nitamkusanya yeye achechemeaye name nitamrudisha yeye aliyefukuzwa…nay eye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu
Matendo 15:16 .. nitajenga tena maanguko yake nami nitaisimamisha,
anaposema atajenga tena maana yake kulikuwepo kitu lakini kilibomolewa.
Inawezekana ukainuka tena, muamini Mungu. Mungu anasema kwakuwa ulikuwa
wa thamani na mwenye kuheshimiwa nitaleta watu kwaajili ya maisha yako.
Aliyekuangusha ni mwanadamu lakini anayekuinua ni Mungu, wao walitumia
madawa ya kienyeji ukaanguka chini, wakachijna Ng’ombe na kuku
wakakuangusha chini lakini Yesu alimwaga damu msalabani ili tuinuke
tena.
Inawezekana familia yako imeanguka lakini Mungu amekuchagua
wewe akuinue tena , endapo utasimama vizuri na Mungu Mungu atakutumia
wewe kukuinua tena.
Kila tukio kwenye maisha yako linalotokea kuna
sehemu linatokea na muhusika anayetengeneza yupo, kila tukio baya kwenye
maisha yako ni ngazi ya kushuka chini na kila tukio zuri kwenye maisha
yako ni ngazi yakupandia. Kuna watengenezaji wa matukio mazuri lakini
kuna watengenezaji wa matukio mabaya. Kila anayekuombea kwa Mungu
anakutengenezea matukio mazuri na kila anayekuloga anakutengenezea
matukio mabaya.