SOMO LA LEO 21.12.2014: UMEANGUKA UMEANGUKA EWE BABELI!_PAUL
JOSHUA_MCHUNGAJI KIONGOZI
Bustani ya edeni ilikuwa babeli ambapo sasaivi panajulikana
kama Iraq
Mwanzo 2:7-15
Hapo awali hapakuwa na bustani wakati Adam anaumbwa, lakini Mungu alipanda bustani
nzuri pembeni ya edeni, bustani haikuwa ndani ya Eden ila ilikuwa pembeni ya
Eden,nakulikuwa na mito ambayo
ilimwagilia bustani hiyo,
Kuna vitu ambavyo shetani amevificha baada ya Adamu na Eva
kuanguka akajimilikisha utajiri wote na kwahuo waganga wa kienyeji na wasoma
nyota wanawapatia wateja wao maana shetani hana kitu wala hajawahi kuumba,hivyo
anatumia mali alizojimilikisha pale edeni kudanganyia watakatifu wa Baba, hapo
alijaribu kumdanganyia hata Yesu yakuwa akimuabudu atampa milki zote lakini
kiuhalisia hana chochote ila aliiba/alijimilikisha mali zote pale Edeni.
Nchi zote za kiarabu zilikuwa nchi za kikristo kam vile Iran,
Iraq n.k lakini sasa hivi zimekuwa nchi za kiislamu maana babeli huyu
kajimilikisha. Ndio maana utaona majini yote asili yake ni uarabuni maana ndiko
mwanamke huyu kahaba anaachilia roho kutetketeza watoto wa Yesu
Bustani ya edeni hii ndio ilikuwa imejengwa babeli ambapo
leo inajulikana kama Iraq
Ufunuo 17:1-6
Huyu mama kahaba kanywa damu za watakatifu na mashahidi wa Yesu mpaka kalewa ,mama huyu haangalii mtume wala mwinjilisti wala nani; ukikaa
vibaya huyu mama anakumaliza,vilevile huyu
mama anakazi ya kushindana na kanisa, anatuma na anaachilia roho ambazo zinaangusha
watumishi wengi wa YESU. Ndio maana watumishi wengi wameanguka kwa uzinzi na
sio wizi,wala ulevi maana mama huyu ameachilia roho za ukahaba ambazo
zinawafuatilia watakatifu wa BWANA na mashahidi wa Yesu yaani wachungaji ,
wainjilissti , mitume,
Ufunuo 18:1-12
Yohana aliendelea kuoneshwa maono. Alioneshwa babeli
anaanguka chini, mamahuyu ameangusha wafanyabiashara wa nchi, maraisi, na
wafanya biashara. Wananchi wamepata utajiri kwa nguvu za kiburi chake.
Yeremia 50:24-25.
Huyu mama amekunywa damu za watakatifu na Mungu ameamua kumtega, naye anashida na
wakristo, huyu mama anashindana na BWANA ,anashindana na Mungu wetu,ameshiba
damu ya watakatifu na anakiburi sana
Ufunuo 18:15
Mama huyu alichukua utajiri wote katika bustani ya
edeni ambao Adam alipewa na Mungu na
ndio huo anawagawia wafanyabiashara wanchi,kila aliyefanikiwa elewa kuwa kuna
nguvu ya rohoni inayomfanya asonge mbele ,kama sio Mungu basi ya shetani(mganga
wakienyeji) ndio maana kila unayemuona kastawi kwa hali yoyote ile anaye ambaye
anamtegemea katika ustawi huo.
Ufunuo 17:18 mwanamke huyu unayemuona ni mji ule mkubwa wenye
ufalme juu ya wafalme wanchi, mama huyu ndiye anayeongoza wafalme wa
nchi(maraisi) ni hatari sana kuwa na mfalme asiyenaYesu (aliyeokoka) maana kwa
namna yoyote huyu mama lazima amtumikishe kwakuwa yeye ni mfalme juu ya falme,
na wafalme wote hufanya mambo kwakuongozwa na mama huyu kahaba.
Zaburi 2:2-3 wafalme wa dunia wanajipanga , na wakuu
wanafanya shauri pamoja , juu ya bwana na juu ya masihi wake. Natuvipasue
vifungo vyao, na kuzitupa mbali nasi kamba zao.
A M E E N ! ! !