SOMO LA LEO
14/12/2014_MITEGO YA WACHAWI_ PAUL JOSHUA MCHUNGAJI KIONGOZI.
ZABURI 10:8-10
ZABURI 64:5
Wachawi wana mitego
yao, nao huandaa mitego ya kila aina, wanatafuta wapi unapenda kutembelea, kula
nk, usimwamini kila mtu, mtu unayemuona mchana unafurahi naye huyo ndio adui
yako anakuwinda usiku.
Wachawi wanakaa vikao usiku wakijadili namna ya kumtendea
mtu au kumshika. Wachawi wanaweza kutega mitego kwenye nguo, maji ,chakula, ndio maana muheshimiwa
alipokuwa anatoa repot ya escrow alikuja na maji yake mwenyewe kwa sababu aliogopa
kuwekewa mitego.
Mtego unaotegwa lazima umpate mtu aliyekusudiwa na sio kwa
kila mtu, ndio maana unawza mkala chakula watu wengi lakini mtego ukamnasa mtu
mmoja, mtu unaweza kumuona mwema yaani amevaa ngozi ya kondoo lakini ni bingwa
wa kutega mitego. Ndio maana unatakiwa uwe makini maana unategwa na ukitegwa
unavutwa kwenye nyavu. Watu wengi wameuliwa maana hawajui wametegwaje.
2 Wafalme 4:38
Maeneo ambayo watu hutegwa sana ni kwenye chakula, na
wachawi hutumia shida au udhaifu wa mtu ili kumtega, kwa mfano wakijua wewe ni
mdhaifu kwa mabinti wanakutega,au kama ni chakula.
Angalia sana mtu asiujue udhaifu wako maana anaweza kuutumia
udhaifu wako kukutega.
Kuwa makini sana usipende kula ovyoovyo, wakina mama nanyi
muwe makini angalia sana juu ya nani anakusuka, nani anakutengeneza nywele
maana si kila mtu ni mwema kwako, wengina wanakuotea ili kukuangamiza.
Uwe makini sana. Adui
yako anataka kukushik au kukunasa na hawezi kukushika bila kukuwinda na
kukukamata kwanza.
Yeremia 5:26
Adui zako wanajadili juu ya namna gani kukupata au
kukuwinda, wanajishauri juu ya nini unapenda kufanya, kula,kunywa nk.
Zaburi 91:3 maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, na katika
tauni iharibuyo.
Adui zako wanakuwinda wakiwa wameweka mitego, mtu
anayekutega au kukuwinda, lazima awe
anakujua vizuri. Adui zako hawawezi kukupata kama hawakujui vizuri, ndio maana
kuna ramani na michoro ya wachawi ili kujua namna ya kukuangamiza. Ndio maana
kwenye kundi la wachawi na adui zako lazima awepo mtu anayekujua vzr
wakuwaongoza , ndio maana bila Yuda mafarisayo wasingemshika Yesu.
LEO TUNAKWENDA KUMPIGA YULE ANAYEONGOZA ADUI ZAKO ILI
USHIKWE, KABLA HUJASHIKWA WEWE ASHIKWE YEYE KWA JINA KA YESU. TUNATANGAZA WALE
WALIOTUMWA KUPELELEZA KANISA, NDOA ,HUDUMA NK. TUNAWAANGAMIZA NA KUWATEKETEZA KWA
JINA LA YESU.
Kuna mtu anakupeleleza, usipende kumwambia kila mtu matatizo
yako ya maisha yako maana huwezi mjua unayemwambia , inawezekana unayemwambia
ni mpelelezi, unapomwambia anapata mwanya wa kukuangamiza.SIO KILA
ANAYEKUCHEKEA ANAKUPENDA.
Usimwambie kila mtu mambo yako maana hauujui moyo wake, moyo
wa mtu anaujua Mungu peke yake, kwa mfano Delila alikuwa mzuri kwa nje lakini
alikuwa mbaya noyoni.
KUMBUKA UNAVYOOMBA SANA UNAWASUMBUA WACHAWI, HIVYO
WANAKUWINDA ILI WAKUKAMATE, NDIO MAANA UKIONA UMEPOA UJUE MTAANI KWAKO WACHAWI
WANAAMANI.
UKIONA SPEEDE YAKO YAKUMTAFUTA MUNGU, YAKUPIGA MAJESHI
IMEPUNGUA ,UJUE UMEPOZWA.
Sio kila mtu anayeongea mambo mazuri au maneno matamu anakupenda,
elewa ya kuwa anakusogeza ili akumalize.
Dada mmoja aliololewa kwa sababu alimuona mwanaume ana
gari(anaufunguo wa gari) sasa haoni gari wala funguo ila anaona kichapo.
Elewa kuwa bado unatafutwa, wale adui zako wa mwaka jana
bado wapo hawajafa ila ulimshinda nguvu, na anatamani akushike tena, akuue lakini
neema ya Mungu imekufunika.
BARIKIWA