SOMO LA LEO
TAREHE 7/12/2014: LAANA YA
WACHAWI _SNP PAUL JOSHUA.
Laana ni mabaya yote ;
( balaa, mikosi, nuksi, shida, njaa, magonjwa,kushindwa, n.k)
1Samweli 17:43
Wakati mwingine Yule amabye anatukana familia yako au ndoa yako, ni kwa sababu ameona hakuna awezaye kuinuka
na kumpinga.
Goliati aliweza kutukana majeshi ya Bwana kanzia asubuhi
mpaka jioni kwa muda wa siku 40, akijiamini kuwa hakuna awezaye kumpinga. Ila
kijana mmoja mdogo Daudi, alisema mimi naweza kupigana naye kwani yeye ni nani
hata ayatukane majeshi ya Bwana?
Daudi alipoanza kusogelea Goliat , alimdharau; akisema wewe?!
Kwani mimi ni mbwa hata uniijie na fimbo? Mfilisiti akaanza kumlaani
Daudi kwa miungu yake. Mfilisti akamwambia Daudi njoo kwangu nyama yako
nitawapa ndege wa anagani na wanyama wa mwituni. Daudi akamwanbia Yule mfilisti wewe unajia na
upanga, na fumo na mkuki, bali mimi nina kujia kwa jina la BWANA wa majeshi,
Mungu wa majeshi wa Israeli uliowatukana. Siku hii ya leo Mungu atakuua mkononi
mwangu, name nitakupiga na kukuondolea kichwa chako, name leo nitawapa ndege wa
angani na wanyama wan chi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia
nzima wajue yakuwa yuko Mungu katika Israeli.
Leo adui zako wajue
yakuwa yuko Mungu katika ndoa yako, yuko Mungu katika masomo yako, yuko Mungu
katika biashara yako, yuko Mungu katika maisha yako, yuko Mungu katika nyumba
yako, wajue haokoi kwa upanga wala mkuki, kwamaana vita si vyetu bali ni vya
BWANA, naye atawatia adui zetu mikononi mwetu. Amina.
Marko 11:12 Ilifika
mahali Yesu akasikia njaa, akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili
aone kitu juu yake; na alipofika hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa
tini. Akajibu akaumbia , Tangu leo hata milele mtu asile matunda juu yako.
Na asubuhi walipokuwa wakipita, waliuona mti ule umenyauka
toka shinani.
Kumbe mtu anaweza kukutamkia neno, likatenda kazi sawasawa
na alivyokutamkia.
Waganga, wachawi ( Mashetani) hutoa sadaka za damu eidha ya
kuku, mbuzi, ng’ombe, njiwa, n.k kwa mapepo na kunuiza maneno juu ya maisha ya
watu , waharibikiwe.
Lakini leo tunageuza laana kuwa Baraka juu ya maisha ya yetu
na kila aina laana walioandaa juu ya maisha yetu iwarudie wenyewe kwa jina la
Yesu.
Yoshua 24:10
Hesabu 23:11
Kumbe watu wanaweza kukodi mtu (mganga) wanampa fedha ili aje
amlaanie mtu Fulani achanganyikiwe, akimbie ndoa yake au aache shule.
Sisi kama majeshi ya Bwana, tunasimama kinyuma kabisa na
laana yao, mganga waliye mkodisha kukulaani wewe, tunateka ulimi wake badala ya
kutamka laana, atamke Baraka juu ya maisha yako . Kilichobarikiwa na Mungu,
mwanadamu hawezi kulaani, haleluya.
Laana inanyausha, tumeona Yesu aliulaani mtini ule nao
ukanyauka hata usitoe matunda tena (usizae)
Laana inanyausha biashara: Utashangaa kuona biashara yako
inayumba, kuna watu wamekaa kulaani biashara yako iharibike.
Laana yaweza kumfanya mtu kuwa maskini, laana yaweza kuondoa
mtu kazini; utajikuta unaona kazi uliyonayo haikufai, ni mbaya , au huipendi.
Kumbe kuna damu imemwagwa inalilia ardhini kukulaani wewe uache kazi.
Pengine kabla huja zaliwa wewe , mzazi wako baba/mama
alitamkiwa maneno kwamba utazaa lakini watoto wako hawatafanikiwa. Leo
umezaliwa wewe unaona mambo yako hayaendi, kumbe ni ile laana inafanya kazi.
Mithali 26:2 Kama shomoro katika kuanga-tanga kwake, na
mbayu wayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu.
Hesbu 23:1
Laana hii kabla ya maneno kutamkwa, kwanza madhabahu
ilijengwa, sadaka zikatolewa na ndipo maneno yakatamkwa kukulaani wewe, lakini
laana hii haiwezi kukupata wewe kama haina sababu.
Watalaani uchanganyikiwe lakini bado watakuona unazidi
kupendeza tu ndani ya Yesu, Watalaani usizae
lakini ndo kwanza watakuona unajifungua
dabble dabble (mapacha )
Vitu vya msingi vya kusambaratisha katika ulimwengu wa roho,
ni kuvunja madhabahu na kusambaratisha sadaka zilizotolewa juu ya madhabahu
hiyo.
Wachawi hawawezi kumlaani mtu bila kumwaga damu au kutoa
sadaka. Kila mtaa, una madhabahu ambazo
huzitumia kulaani watu na kuchukua damu za watu kama sadaka.
Shetani yupo siku zote kutafuta amani yako aimeze, kutafuka
kazi yako aimeze kukutafuta wewe akumeze. Laana ikiingia katika familia,
hunyauka.
Kuna watu hawapendi kuona wenzao wakifanikiwa, mioyo yao
hunung’unika wakisema kwanini yeye, kwanini yeye, kwanini ajenge, kwanini
asome, kwanini aolewe, kwa nini aoe, kwanini ajenge ; kumbe hata bila kutamka neno, moyo unaweza
kulaani.
Huna kazi kwa sababu laana ina nafasi kwenye maisha yako, ipo katika biashara yako,
haufaulu kwasababu ulitamkiwa usisome.
Leo kila familia iliyo laaniwa, ibarikiwe kwa jina la Yesu.
Na istawi katikati ya maadui, hiyo
inawezekana kabisa, wataishia kulaani tu huku wewe unazidi kubarikiwa.
Usiogope kukaa mtaa mmoja na wachawi, usiogope kufanya
biashara sehemu moja na wachawi, Mungu atakusaidia, wewe kaa tu, unapokaa na
watu kama hao ndipo utamwona Mungu, kwani yeye huonekana katika magumu kujitwalia
utukufu. Unaweza kustawi katikati ya hao hao adui zako, ndiyo ni wengi lakini
mkono wa Bwana ni mkuu, waache walaani;
Barahamu badala ya kulaani, akaanza kbariki.
Ni saa ya kustawi, kanisa listawi, Kigoma istawi, Tanzania
istawi. Walilaani sana, sasa laana zimegeuka na kuwa Baraka.
Kila madhabahu zote katika ulimwengu wa roho zinavunjika kwa
jina la Yesu.
BARIKIWA.