SOMO: VIFO VYA KUTENGENEZA
SNP: PAUL JOSHUA
Ni kweli watu wanakufa na kuna vifo ambavyo ni mpango wa Mungu lakini
kuna asilimia kubwa ya watu ambao wanaokufa; na vifo hivyo vinakuwa ni
vifo vya kutengeneza. Mtu anapozaliwa Mungu anampa miaka mingi ya kuishi
lakini hapa katikati wachawi wanatokea wanatengeneza matukio ili
kufupisha maisha yako. Yawezekana umetengenezewa kifo kwenye ukoo wako
au kwenye familia yako na kabla hakijakupata leo tunaibomoa kwa jina la
Yesu.
MATHAYO 27:1 Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote wa wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu wapate kumwua.
Tunaona kikao cha wazee kinaandaa mauti juu ya Yesu, kumbe watu
wanaweza kukukalia kikao ama usiku ama mchana wakaandaa kifo kwenye
maisha yako. kwa maana kila tukio baya linalokutokea wewe kuna sehemu
limetokea hakuna tukio linakuja kwako kwa bahati mbaya. Matukio yote
mabaya yanatengenezwa kuzimu, na mazuri yanatengenezwa mbinguni; na leo
tunaamuru mbingu itengeneze mambo mazuri kwaajili yako, kwaajili ya
familia yako kwa jina la Yesu.
Wazee wakaona kati ya wanafunza
kumi na mbili wa Yesu kuna mtu ambaye watamtumia ili kumwangamiza Yesu,
Yuda akaitwa akaambiwa unataka shilingi ngapi akasema nataka vipande
ishirini vya fedha.
Kuna kundi la watu wamekaa kikao ili
kutengeneza kifo kwaajili yako lakini leo kabla hujalia wewe watalia
wenyewe. Maana Yuda aliyemsaliti Yesu kabla Yesu hajafa Yuda
akajinyonga, msalaba ambao aliuandaa Hamani ili kumtundika Morkedai
akatundikwa yeye; na leo kila aliyekaa kikao kuandaa kifo juu ya maisha
yako kiwarudie wenyewe; maana imeandikwa anayepolomosha jiwe kwaajili
yako limrudie mwenyewe, anayekuchimbia shimo atatumbukia mwenyewe.
UKiri: Kwa damu ya Yesu ninabomoa kila uchawi uliotumwa kwenye familia
yangu roho za kifo ninazibomoa kwa jina la Yesu, hakuna kifo kwenye
familia yangu, kwenye nyumba yangu, kwenye ndoa yangu, kwa watoto wangu,
ninakataa kwa jina la Yesu.
Adui zako waache waje maana
wanakutengenezea mafaninikio, ili ushindi uje kwenye maisha yako ni
lazima Yuda awepo ili akutengenezee mazingira uinuke. Yule adui yako ni
daraja la ndoa yako, ni daraja la huduma yako, na ukimuona adui yako
mwambie wewe ni daraja langu bila wewe sitaweza kupiti.
Usiogope
kwaajili yao kwa maana wao wanataja magari, wao wanataja farasi, wao
wanataja waganga wa kienyeji, lakini sisi tunalitaja jina la BWANA. Ni
kweli wanashindana nasi lakini hawatashinda maana walio upande wetu ni
wengi sana kuliko walio upande wa adui zako.
Anayeaandaa kikao
kwaajili yako ni daraja la maisha yako bila yeye huwezi kupita, wamekaa
vikao wanajadili utakufa lini? Imeandikwa Sitakufa bali nitaishi hadi
niyasimulie matendo makuu ya BWANA hautakufa kwa damu ya mwana kondoo.
Inawezekana kuna wazee wa mtaa wamekaa sehemu ili kujadili ndoa yako,
kujadili masomo yako, kujadili kazi yako, lakini imeandikwa vita si
vyako bali ni vya BWANA nyamazeni kimya muone BWANA atakavyowapigania
wamisri mnaowaona leo hamtawaona tena maadui zako walioinuka leo
hutawaona tena.
Kifo kinaweza kutengenezwa kwa njia ya ajali; kwa
maana hakuna dereva anayependa kufa, au hakuna bodaboda anayependa kufa
hata kama ni mlevi. Lakini wachawi wanaweza kutengeneza kifo cha ajali;
wanaweza wakaita majini jini makata, jini subiani, wanatoa kafara ya
damu wanayapa majini wanayaambia kaa barabarani ili mtu Fulani anapokuja
umtie kizungu-zungu anguke.
Kifo kinaweza kutengenezwa kwa namna
ya magonjwa. Kuna kiwanda sehemu cha kutengeneza magonjwa, na ukitaka
kutoka kwenye magonjwa tafuta kiwanda cha kutengeneza magonjwa, maana
siyo kila mwenyeugonjwa ni wa kawaida,siyo kila Ukimwi ni wa kawaida,
unaweza kutengenezewa. Unaweza ukaenda kupima ukaambiwa una sukari au
unaambiwa moyo umepanuka kumbe yanakuwa ni magonjwa ya kutengeneza.
Hata kwenye familia mnaweza kutengenezewa magonjwa unakuta kila mwaka
lazima afe mtu, wengine unakuta kwenye familia kuna ugonjwa wa presha,
ugonjwa wa moyo, sasa leo kile kifo ambacho kimetengenezwa kikupate,
wewe au familia yako au watoto wako tunakibomoa kwa jina la Yesu.
DANIEL 6:1-7 Ilimpendeza Dario kuweka juu ya ufalme maliwali mia na
ishirini, wawe juu ya ufalme wote na juu yao akaweka wakubwa watatu, na
Danieli alikuwa mmoja wao, ili maliwalo hao watoe hesabu kwao mfalme
asipate hasara. Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na
maliwali, kwakuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu
kumweka juu ya ufalme wote. Basi mawaziri wakatafuta sana kupata sababu
za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme lakini hawakuweza
kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu wala hakuonekana
kosa wala hatia ndani yake. Ndipo wale watu wakasema hatutapata sababu
ya kumshitaki Danieli huyo tusipoipata katika sheria ya mambo ya Mungu
wake. Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya
mfalme wakamwambia hivi mfalme Dario uishi milele. Mawaziri wote wa
ufalme na manaibu na maamiri na madiwani na maliwali wamefanya shauri
pamoja ili kuweka amri ya kifalme na kupiga marufuku ya kwamba mtu
yeyote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote au kwa mtu awaye yote katika
muda wa siku thelasini ila kwako Ee mfalme atatupwa katika tundu la
simba.
Tunawaona hawa walifanya shauri kwaajili ya Danieli ili
kuandaa kifo kwaajili yake, muda mwingine inawezekana Mungu amekuinua
mahali pako pa kazi adui zako wanaamua kufanya shauri ni jinsi gani
wakuangamize. Lakini usiogope Mungu yuko pamoja nawe hakuna jambo
lisilowezekana kwake, watafanya sana mashauri lakini hayatafanikiwa kwa
jina la Yesu.
Usiogope adui zako wewe songa mbele utafanikiwa mbele
ya macho yao; adui yako ni daraja lako na ukitaka upite tafuta adui,
ukimuona adui amekuja kwako ujue kuna hatua nyingine kwenye maisha yako.
Hao wamisri unaowaona leo hautawaona tena maana BWANA atakupigania
f-Farasi na mpanda Farasi BWANA amewatosa baharini, leo adui zako
tunawatosa ziwa Tanganyika kwa jina la Yesu.
Unapoona jambo
limekutokea iwe kwenye ndoa ama kwenye huduma kuna sehemu kikao
kimekaliwa, tafuta kikao kilipokaliwa usihangaike na magonjwa tafuta
kiwanda cha magonjwa tunazifuata kwenye ulimwengu wa roho na kukipasua
kwa jina la Yesu.
Kunapokuwa na watu wanakutafuta lazima Yuda
awepo, mtu anayekujua vizuri ni lazima awepo ili kuwaambia latiba zako
huwa zinaendaje, anakuwa anakujua unatoka saa ngapi na unarudi saa ngapi
na unapita njia ipi, lakini leo tunatuma malaika kwenye kila hatua zako
wakutangulie unapopanda gari na kila unapokanyaga nyayo za miguu yako.
Wanatega mitego mauti ikupate popote ulipo siyo wewe tu hata wanao
lakini kwakuwa umeokoka neema yako yatosha kuwafunika ndugu zako na
watoto wako hata kama hawajaokoka.
Dalili za kujua kama kuna roho ya kifo au mauti imetumwa kwako, au kwenye familia yako.
1. Kuota ndoto za msiba; tambua kuna jambo baya ambalo limetumwa lije kwenye maisha yako au kwenye familia yako.
2. Kuota unalia; tambua kuja jambo baya limepangwa lije likulize.
3. Kukosa amani; yaani siku nzima hauna amani, unalala usingizi unaota
ndoto mabaya, unashangaa mbona sina amani leo hiyo ni ishara kuna roho
ya kofo ama kwenye familia.
4. Moyo kushituka-shituka. Unatembea unawaza kifo, Ndio maana mtu aliyeokoka mmoja anaweza kuzuia mauti kwenye familia nzima.
Ukiri: kwa damu ya Yesu roho ya kifo iliyotumwa kwangu au kwenye
familia yangu ninaivunja kwa jina la Yesu, nakataa kifo kwenye maisha
yangu kwa jina la Yesu, nakataa kifo kwenye familia yangu, kwenye ukoo
naibomoa roho ya kifo kwa jina la yesu.