JUMAPILI TAR 15/5/2016
SOMO: KESHO ILIYOPINDISHWA
SNP: PAUL JOSHUA
Mungu anapomuumba mtu anampa mwanzo
wake na mwisho wake. Anampa aanzie maisha ya chini lakini hatima yake iwe
maisha mazuri anaweza akaanza na nyumba ya udongo hatima yake akamiliki
gorofani, anaweza akaanzia kwenye magonjwa lakini kesho yake ni uzima, anaweza
akawa masikini lakini hatima yake ni kumiliki utajili. Lakini shetani huwa
anaweza kuiona kesho au hatima ya mtu na aakamua kuipindisha ili kesho yake
ambayo anatakiwa amiliki isitimie, lakini lleo tunawatangazia wachawi wote
tunawashinda kwa damu ya mwana kondoo.
WARUMI 8:29-30 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana
wake ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi; na wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita na wale aliowaita akawahesabia haki na
hao aliowahesabia haki akawatukuza.
Mungu alikuchagua tangu mbinguni
uwe mtu fulani, uwe mchungaji, uwe tajiri, uwe na ndoa nzuri uwe na maisha
mazuri; Mungu alikuchagua tangu asili, lakini shetani anapambana na kile
ambacho Mungu alikipanga juu ya maisha yako. Shetani anaangalia mtu huyu
amezaliwa lakini miaka hamsini au thelasini ijayo mbele atakuwa mtu Fulani; ni kweli amezaliwa kijijini lakini mwisho wake
ni kuishi marekani hakikisheni mnapindisha maisha yake aishie kwenye magonjwa.
Wanasoma nyota yako na kujua Mungu amekupangia nini ni kweli ana kasi ya
kumtumikia Mungu, hakikisheni mnamfunga; Lakini leo tunawatangazia wachawi wote
kwamba tumepewa nguvu ya kushinda kwa jina la Yesu. Tunaye Yesu ambaye
alishinda kifo na mauti, yawezekana ulianza kwa huzuni lakini utamaliza kwa
kucheka hata Yesu alizaliwa kwenye nyumba ya fundi selemara lakini akaishia
kuwa mfalme wa wafalme. Mungu huwa anaiandaa kesho ya mtu, na anapokuokoa lengo
la kwanza la Mungu ni kumpeleka kwenye hatima ya maisha mazuri, hata kama
ameanza vibaya lakini atamaliza vizuri kwa jina la Yesu.
AYUBU 8:5-7 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, na kumsihi huyo mwenyezi ukiwa wewe u
safi na mwelekevu; hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako na kufanya makazi
ya haki yako kufanikiwa. Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini
mwisho wako ungeongezeka sana.
Hata kama umeanza vibaya mwanzo
wako umekuwa sio mzuri lakini BWANA anakuja kufanya makazi kufanikisha haki
yako na hatima yako inaongezwa, kesho yako inakwenda kufanikiwa ule uchawi
ulifanywa ju yako ili kupindisha kesho yako ili wakuingize kwenye huzuni
tunaubomoa kwa jina la Yesu.
MATHAYO 2:1-2 Yesu alipozaliwa katika Bethlelehemu ya uyahudi, zamani za mfalme Herode
tazama mamajusi wa mashariki walifika yerusalemu wakisema. Yuko wapi yeye
aliyezaliwa mfalme wa wayahudi? Kwa maana tuliona nyota yake mashariki nasi
tumekuja kumsujudia.
Mamajusi hawakupigiwa simu bali
waliiona nyota ya Yesu wakajua kuwa huyu ni mfalme amezaliwa; wakaenda
kumsujudia akiwa bado mchanga fedha zikaanza kuja, dhahabu zikaanza kuja,
zawadi zikaanza kuja kumbe nyota iking’aa fedha zinakuja, zawadi zinakuja,
dhahabu zinakuja nyota yako ing’ae leo kwa jina la Yesu.
Nyota ya Yesu ikaonekana akiwa
mchanga, ingawa alizaliwa kwenye holi la ng’ombe lakini hatima yake akaishia
kuwa mfalme; hata wewe usikate tama kwenye maisha yako nyota yako inangaa tena
haijalishi umepitia nini kwenye maisha yako ingawa ulisoma shule bila hata
viatu, au hata shule hujasoma lakini Mungu anakuinua tena kwa jina la Yesu.
Tunawatangazia adui zako ipo njia
nyingine hata kama ulifeli mtihani, ipo njia nyingine hata kama hujasoma sana
ipo njia nyingene ambayo haihitaji uwe umesoma sana bali inamhitaji roho
mtakatifu. Yesu yupo kwaajili yako usivunjike moyo mwambie Yesu akuonyeshe njia
ya kupita; yawezekana mchumba wako ulimsubili kwa muda wa miaka mingi lakini
sasa amekwambia amepata mwingine, usiwe na wasiwasi mtazame Yesu. kila jambo
lina kusudi la Mungu hata kama unapitia mateso ingawa Ayubu alipitia mateso
lakini hakupenda apitie mateso, ndani ya mateso ya Ayubu kulikuwa na kusudi la Mungu.
Heri wewe unayekula ugali kwa
tembele kila siku lakini nyumba yako ina amani kuliko nyumba ambayo wanakula
pilau na kuku kila siku siku lakini nyumbani ni ngumi kila siku.
Kuna watu wengine wamepindishwa
kona, wanajikuta wanafanya kazi ambayo siyo ya kwao mtu anajikuta alipanga awe
Rubani lakini anaishia kuwa mama wa nyumbani, alitakiwa awe mbunge lakini
anaishia kuwa mpiga bodaboda na shetani
amepindisha maisha ya watu kwa sababu aliona nyota zao. Wachawi wapo wanaweza
kumloga mtu asisome shule, asizae watoto, asipate kazi wanapindisha kesho ya
mtu na anajikuta anaishia kufanya kazi ambayo haipendi.
Kuna watu wengine kesho yao
ilipindishwa kwa namna ya kupewa uchawi wakiwa wadogo au wakubwa, wengine
wamejikuta wanaitwa wachawi ingawa hawalogi, wengine kuna kitu ambacho walipewa
nyumbani kwenu yawezekana madawa, mahirizi yamebaki yanakutesa kwenye masha yako
na mwisho wake yatakumaliza mwenyewe; kesho inakuwa imepindishwa hauwezi
kufikia malengo ambayo Mungu aliyapanga kwenye maisha yako. Watoto wengine
hatima ya maisha yao imepindishwa walitakiwa wawe shule lakini wanaishia
kuloga, wengine walitakiwa wasonge mbele kwenye maisha yao yakini wanaishia
kuloga.
Kuna mwingine alitakiwa awe
muimbaji lakini kesho yake imepindishe, mwinginge alitakiwa afanye biashara
kesho yake imepindishwa anajikuta anapitia maisha magumu ni kwa sababu wachawi
waliona kesho yako, waliona hatima ya maisha yake wakaamua kuipindisha, lakini
leo tunaangusha falme zao kwa jina la Yesu.