JUMATATU TARAHE 12 OCTOBA, 2015
SNP: PAUL JOSHUA
SOMO: MAOMBI YA REHEMA
2Mambo ya Nyakati 7:14 “Ikiwa watu wangu walioitiwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuomba na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mabaya basi nitasikia toka mbinguni na kuiponya nchi yao”.
Kukiwa na dhambi hakuna jambo ambalo Munguatalifanya kwako ni lazima ujinyenyekeshe na kuomba mbele za BWANA na kuutafuta uso wa BWANA ili kuomba rehema mbele za Munguanasema katika neno lake atasikia maombi na kukuponya.
Yoshua 7:2 “Kisha Yoshua akatuma watu kutoka yeriko mpaka mji wa Ai. Ulio karibu na bethaveni upande wa mshariki wa betheli akawaamia akisema pandeni juu wakaupeleleze nchi, Basi wakapanda juu wakapeleleza Ai”.
1Samwel 15:19 “Mbona basi hukuitii sauti ya BWANA bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA”.
Kuna watu wengine Mungualiwaacha kwa sababu ya kutokutii sauti ya BWANA, unapaswa kuwa unatii kila kitu ambacho Munguanakwambia ukifanya maana unaweza ukajikuta Munguanakuacha kwa sababu ya kutokuwa mtii. Tunamuona Sauli ambaye Mungualimwacha kwa sababu hakuitii sauti ya BWANA bali akafanya yaliyo maovu mbele za BWANA matokeo yake Munguakamwacha.
Kila mtu ana neema Fulani au kipawa ambacho Munguamempa ili amtumikie, lakini kuna wakati tumejikuta Munguametuacha kwa sababu hatukutii sauti yake kwa kuyatenda yote aliyotuamuru. Munguanaweza kughairi mazuri yote ambayo ameahidi kumfanyia mwanadamu. Kutembea na Munguni gharama tena siyo kitu cha mchezo
1Samwel 2:29 “Kwanini basi mnapiga teke dhahabu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika masikani yangu ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israel zilizo njema”.
Dhambi inamfanya mtu asiende mbele kiroho na kijikuta hata hatua aliyokuwa anayo inatoweka, inakupasa kumwendea Munguili akusaidie
Mithali 5:22” Maovu yake yeye yatampata mdhalimu naye atashikwa kwa kamba za dhambi zake”.
Huwezi kufanikiwa ndani ya dhambi unaweza ukaombewa mara nyingi lakini huponi shida inakuwa ipo kwenye dhambi, kwa kiwango ambacho unamsikiliza Munguna kukifanya anachokitaka maisha yako hayatabaki kama yalivyo ni lazima Munguatakusaidia na kukuvusha. Kumbuka bidii yako ya kwanza kanisani mbona huombi kama zamani uko wapi upendo wa kwanza wa mungu, umepata ndio maana umesahau kidogo hicho umekipata ndio maana umemsahau Munguungekuwa bado hujapata ni lazima ungemtafuta mungu. Ulikuwa ukiomba tu Munguanajibu lakini sasaivi inajikuta unaomba sana lakini hakuna mabadiliko kuna kitu umepoteza. Unajijua mwenyewe ni wapi ambapo ulianguka na kukosea Munguwetu amejaa rehema na huruma atakusamehe na kutozikumbuka tena dhambi zako.