JUMAPILI TAREHE 3.4.2016
SOMO: MAHALI PA JUU
SNP: PAUL JOSHUA
Kila mtu ana mahali pake pa juu,
ambapo akifanikiwa kupanda maisha yake yanafanikiwa lakini kuna waliokaa mahali
pa juu kwa kutumia nguvu za giza na wanganga wa kienyeji; wengine wametoa
sadaka mahali pa juu pa shetani ili waendelee kukaa juu. Mungu naye anakaa
mahali pa juu ni wakati wa kila mtu kumwambia Mungu napanda mahali pa juu pa
maisha yangu na kumshusha kila aliyekaa mahali pako pa juu pa maisha yako.
2WAFALME 16:1-4 “Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Ramalia Ahazi mwana wa
Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza
kutawala; akatawala miaka kuni na sita katika Yerusalamu wala hakufanya mema
machoni pa BWANA Mungu wake kama Daudi babaye. Lakini aliiendea njia ya wafalme
wa Israeli hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na mchukizo ya mataifa BWANA
aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli. Kasha akatoa sadaka za kufukiza uvumba
katika mahali pa juu na juu ya vilima na kila mti mbichi”
Akatoa watoto wake sadaka na
akaanza kutoa sadaka mahali pa juu, maana yake shetani anataka kutolewa sadaka
mahali pa juu kila eneo kuna aliyekaa juu na unapotaka kupanda juu ni lazima umshushe
aliye juu huwezi kupanda wakati unapotaka uende pana mtu amekaa kwenye kiti
chako, ni lazima upambane ufunge na kuomba ili uhakikishe kila aliyekaa juu kwa
kutumia uganga na uchawi umshushe kwa jina la Yesu.
HESABU 33:50-52 “kisha BWANA akanena na Musa hapo katika
nchi tambarare za Moabu karibu na Yordani hapo Yerko na kumwambia. Nena na wana
wa Israeli uwaambie, mtakapovuka mto Yordani na kuingia nchi ya kaanani, ndipo
mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe
yao yote yenye kuchorwa sanamu na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu,
kuvunja-vunja mahali popote palipoinuka”
Na leo tunakwenda kupiga mahali pa
juu pa shetani, kila eneo katika ulimwengu wa roho kuna mahali pa shetani pameinuka. Mchana wa
leo tunamfuata aliyekaa mahali pa juu palipoinuka pa maisha yako. Kila mganga
wa kienyeji ana mahali pa juu palipoinuka, kila anayekutesa ana mahali pa juu
anapochukua msaada ili akutesa. Mwambie Mungu akupe nguvu uangushe mahali pa
juu pa shetani. Kila mtaa una mahali pa juu na Mungu naye ameketi mahali pa juu
patakatifu. Kuna watu wengine wamekaa
mahali pa juu ofisini kwako wewe umekaa chini leo tunageuza wakae chini kwa
jina la Yesu maana Mungu anasema anatuinua kutoka mavumbini na kutuketisha
pamoja na wakuu.
2WAFALME 12:3 “Ila mahali pa juu hapakuondolewa watu wakaendelea kutoa sadaka na
kufukiza uvumba mahali pa juu”
Kila aliyefanikiwa kuna mamlaka Fulani imemfanya awe juu kuna
wengine wametoa sadaka na kufukiza uvumba kwa shetani. Shetani hawezi kuruhusu
mtu apande juu kirahisi shetani anachokifanya anawashusha watu wa Mungu na
kuwapandisha watu wake mahali pa juu, Kama mganga anaweza akamfanya mtu akapata
Dola kutoka kuzimu, au mtu anafungua akaunti kuzimu, je yuko wapi Mungu wetu.
1SAMWELI 2:8 “Humwinua
mnyonge kutoka mavumbini, humpandisha mhitaji kutoka njaani ili awaketishe
pamoja na wakuu wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu”
“Kila mtu aliyeokoka ana mahali pa juu pa maisha yake” Kanuni
ya Mungu ni kumtoa mtu chini na kumpandisha juu ili kuketi pamoja na wakuu, Mungu
humtoa mtu kwenye dhiki kwenye shinda na matatizo, kwenye umaskini, kwenye
njaa, kwenye kukataliwa na kusengenywa lengo la Mungu ni kumpeleka mahali pa juu pa maisha
yako. Na ukiwa mahail pa juu utaweza
kuwashika ndugu zako mkono na kuwapandisha mahali pa juu, unaweza kuwashika
watoto wako na kuwapandisha mahali pa juu; Mchungaji yupo ili kukushika mkono
na kukupandisha mahali pa juu pa maisha yako.
2SAMWEL 22:37-37 “Nawe
umenipa ngao ya wokovu wako, na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia
nafasi hatua zangu wala miguu yangu haikuteleza”
Kuna wengine wamekuwekea utelezi kula ukitaka kupanda
unateleza na kurudi ulikotoka unatamani usome shule, uanze biashara, utoke
kwenye umasikini lakini kila ukitaka kupanda kwenye mafanikio kuna watu
wamekuwekea utelezi unajikuta unateleza na kurudi ulikotoka kurudi kwenye
umaskini, kurudi kwenye shida ya ndoa, kurudi kwenye magonjwa.
ZABURI 69:4 “Wanaonichukia
bure ni wengu kuliko nywele za kichwa chngu, watakao kunikatilia mbali wamekuwa
hodari. Adui zangu kwa sababu isiyo kweli, hata mimi nalilipishwa kwa nguvu
vitu nisivyovichukua:
ZABURI 40:2 “Akanipandisha
toka shimo la uharibifu, toka udongo wa utelezi akanisimamisha miguu yangu
mwambani akaziimarisha hatua zangu.”
Katika maisha kuna watu wapo kwenye ofisi Fulani lakini
wanatumia wanganga wa kienyeji, wana waganga ambao ndio wanawategemea na
unapokuwa unahitaji kupanda mahali pa juu unakuwa unapambana na mganga
unapoomba na kufunga unamshusha mtu anaetumia uchawi kukaa katika ofisi Fulani.
Watu wengi Mungu anapowapandisha na kuwaketisha mahali pa juu
huwa wanasahau walikotoka na wanajikuta wanashushwa chini na adui zao na
wanajikuta wanarudi kwenye shida mbali mbali.