TESTIMONIES













Mr. & Mrs Emmanuel Haraka wakimshukuru Mungu leo katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma kwa kuwapa mtoto,
Kipindi cha ujauzito wake Mrs Haraka alipata misukosuko mingi; tangu ujauzito ukiwa na miezi 3 alianza kusikia machungu ya kujifungua, ujauzito ulipofikia kipindi cha miezi 5 alipimwa ikaonekaana kuwa kondo limetangulia mbele badala ya mtoto, hali hiyo iliendelea mpaka kipindi cha miezi 8 cha ujauzito wake.
Majeshi ya Bwana Ufufuo na Uzima yaliingilia kati baada ya kuona hali si shwari mpaka kondo likampisha mtoto na akazaliwa salama.









"ALIISHI NA GLOVES TUMBONI KWA MUDA WA MIEZI 3"
Anaitwa ESTA, anadai kuwa baada ya kujifungua na kuruhusiwa kurudi nyumbani, alianza kuona mabadiliko mwilini mwake, harufu mbaya ikautawala mwili na mazingira yote alipo kuwa. Ikawa kero kwa majirani na kwa kila mtu aliye pita karibu naye. Ndipo ESTA akarudi hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kujua nini chanzo cha harufu hiyo. KUMBE! Gloves ilisahaulika tumboni wakati ma nesi wakimzalisha.
Jambo ambalo lilishangaza wauguzi wa pale na kusema Mungu wako unaemwabudu ndiye Mungu wa kweli kwani kwa hali ya kawaida usingepona.
 "UFUFUO NA UZIMA KIGOMA"




Pastor Paul Joshua _ Akili Iliyobiwa



Pstor Paul Joshua_ Mtego wa Mwindaji





Bibi huyu amshukuru Mungu kwa kumponya moyo ambao ulikuwa umejaa maji. Ni katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma.





Moto umewaka, tumbo la kuzimu linashindwa kuvumilia maumivu, nalo nianawatapika watu wa Mungu kwenye uzima wao.
Dada huyu arudi kutoka shimoni baada ya maombi ya kumtapisha ALIYEMEZA.














Mama Mrko akimshukuru Mungu katika madhabahu ya BWANA Ufufuo na Uzima Kigoma. Mama huyu anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kujifungua salama kwani wakati wa ujauzito, mtoto  alipotea tumboni hali iliyomfanya akose amani. Aliamua kuja kuombewa katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma na mtoto akarejea tena tumboni na kuzaliwa salama.





Jesca akiwa amesimama kumshukuru Mungu katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma baada ya kutendewa muujiza wa kuponywa ugonjwa wangozi uliopelekea ngozi yake kugeuka na kuwa kama ngozi ya kenge.














NI MIAKA 4 SASA BAADA YA DADA HUYU (GRACE) KUPONYWA KIFAFA KILICHOKUWA KINAMSUMBUA TANGU  AKIWA MTOTO MCHANGA. DADA GRACE AMEPONA UGONJWA HUO BAADA YA KUJA KUOMBEWA KANISANI UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.





















“FUMBO LA ROHONI”
JOYCE HENRY (17) MKAZI WA NGURUKA KIGOMA;
Ni binti ambaye alipewa sufuria, kikombe, bakuli, shanga na sarafu mbili kama tuzo; Alikabiddhiwa  na bibi yake akiwa na umri wa miaka 3, tuzo hii ilikuwa maalum akisha olewa ndipo angeweza kuitumia. Kwakuwa  Joyce alikuwa mtoto mdogo, hivyo aliteuliwa mtu (baba mzazi wa Joyce) kuisimamia /kuilinda tuzo hiyo mpaka atakapokuwa mkubwa.
Mpaka sasa Joyce ana umri wa miaka 17. Joyce amekuwa mtu wa kuumwa muda wote hivyo kaamua kukimbilia kanisani Ufufuo na Uzima Kigoma nakusalimisha tuzo ambayo aliachiwa na bibi yake.
Jambo ambalo limeshangaza jamii ni kuwa vyombo hivyo viligeuka kuwa vizito sana hata visibebeke pale Joyce alipotaka kuvisalimisha kanisani. Baadhi ya watu walipigwa mionzi na kuanguka chini pale tu walipotaka kumsaidia Joyce aweze kuvifikisha kanisani.
Mama Joyce aliomba msaada wa makonda wa daladala wamtwishe kichwani, mama Joyce hali ilikuwa ngumu kwake mpaka anafikisha kanisani shingoilikuwa imepinda.
Bwana Yesu asiyeshindwa na lolote, kwa kumtumia mpakwa mafuta wake aliyemtuma Kigoma Mchungaji kiongozi Paul Joshua,  kwa maombezi makubwa kanisani Ufufuo na Uzima Kigoma, Joyce ni mzima sasa.








AKUTANA NA FAMILIA YAKE ILIYOTEKETEA   (Marehemu ndugu zake)
Baada ya maombezi makubwa katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Kigoma,yamrudisha Lewina Yohana na kueleza aliyoyaona kule alikokuwa.
Asema kuwa alichukuliwa msukule na kukutana na ndugu zake waliokufa zamani. Akutana nao katika chumba cha kuhifadhia misukule ambacho kina milikiwa na babu yake mzaa baba yake, dada huyu alishangaa kumuona shangazi yake akiwa hai, baba yake akiwa hai na wengine hata hakuweza kuwafahamu kulingana na hali yao ilikuwa ya tofauti sana kwani nywele zao zilikuwa ndefu tena chafu sana, kucha zao hata ngozi zao zimechakaa sana
Dada huyu aliumwa sana asiweze kujitambua ndipo ndugu zake wakapoteza tumaini kuwa haponi tena kwan alikuwa hapumui wala hatikisiki mkavu sana kama mti uliokauka; Baada ya dada huyu kurudishwa, alisema kuwa yeye alikuwa haumwi ila tu alikuwa kwa babu yake mzaa baba yake katika chumba cha kuhifadhia misukule na kudai kwamba amefanikiwa kuutoka kule sababu hapaukuwa na mtu wa kumsogelea na kuweza kumpaka dawa.
 







Yasinta Martin
Arudishwa na majeshi ya ufufuo na uzima Kigoma, asema kuwa mama yake mdogo ndiye aliyehusika kumchukua (msukule) dada huyu tangu akiwa mdogo kisha akampeleka sokoni kuuza ndizi, dagaa na vitu vingine. Anasema kuwa chakula chake kilikuwa ni ndizi.
Jinsi alivyorudi; alisikia sauti ikmwita “Yasinta njoo kwa Jina la Yesu” kisha akahisi kama kitu kinamsukuma na kuweza kutoka mahali alipokuwa amesimama na kuweza kukimbia.
 




USHUHUDA  JUU YA KUPATA MTOTO BAADA YA KUTESEKA KWA MUDA MREFU.
Dada huyu anatoa ushuhuda wa mambo mema aliyo tendewa na Mungu baada ya kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, alikaa miaka sita akisimangwa nakutukanwa na watu japo mmewe alimtia nguvu na kumfariji. Walipewa muda na Mungu wakutukanwa lakini muda waushindi ulikuwa umeandaliwa ili Mungu ajitukuze.kama ilivyokuwa wa kwa Israel juu ya Goliath, aliachiwa muda wakulitukana jeshi la Bwana wa majeshi lkini muda waushindi uliwadia akakatwa kichwa.

THE TESTIMONY ON GETTING A CHILD AFTER BEEN SUFFERED FOR A LONG TIME
This lady is giving her testimony on the great thing which God has made to her after been suffered for a long time without getting a child, she stayed for six years while been offended by people though her husband strengthened her in that situation and comforted. Enemies were given time by God to insult her but the time of salvation were prepared by God in order to glorify himself. Goliath was given time by God to offend Israelites but the time of salvation come where he was killed.






USHUHUDA  JUU YA KUPATA MTOTO BAADA YA KUTESEKA KWA MUDA MREFU.
dada huyu anatoa ushuhuda wa mambo mema aliyo tendewa na Mungu baada ya kukaa muda mrefu bila kupata mtoto,alikaa miaka mitatu bila kupata mtoto lakini Bwana amempa mtoto wa kiume.


THE TESTIMONY ON GETTING A CHILD AFTER BEEN SUFFERED FOR A LONG TIME
This lady is giving her testimony on the great thing which God has made to her after been suffered for a long time without getting a child. She stayed for  three years without getting a child, but God has given her a baby boy. 


 Hatimaye aliyekuwa kichaa afunguka!
Esta ni dada ambaye alikuwa na tatizo la akili (kuchanganyikiwa)
Leo katika madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma akimshukuru Mungu kwa mambo makuu aliyomtendea kwa kumponya ukichaa huo na kumpa mtoto wa kiume.
Alijifungua kanisani wakati majeshi Ufufuo na Uzima Kigoma yakifungua akili za dada huyu.

 

Now the one who was crazy has been delivered!

Ester is the lady who has mental problem(crazy)

to day Ester is giving thanks at the temple of Ufufuo na Uzima Kigoma to the Almighty God for delivering and healing her and for giving her a child (baby boy)

she gave birth when the Ufufuo and Uzima solders(solders of Christ) delivering her mind (brain of this lady).

 

 Aliyetumwa na Mungu, huwezi kumzuia.
Japo kuwa shetani alijaribu kuficha na kufunika kusudi la Mungu juu ya matumishi wake, kwa kumfanya MKUU WA MAFIA huko Japan, Leo hii ni MCHUNGAJI KIONGOZI UFUFUO NA UZIMA JAPANI.
Hapa pichani ni alama ambzo alichorwa kipindi cha nyuma kabla hajaokoka zikiashiria kuwa yeye ndo mkuu wa mafia.

MCHAWI ANASWA_UFUFUO NA UZIMA KIGOMA 

  Ilikuwa jana majira ya saa kumi jioni katika kanisa la Ufufuo na Uzima -Kigoma, lilitokea tukio ambalo liliwashangaza watu ambao mpaka sasa hawaani uchawa (wakimaanisha hakuna uchawi)

Mama mmoja alinaswa na nguvu za Mungu kanisani Ufufuo na Uzima akiwa na vifaa/vitendea kazi katika kazi zake za kichawi.

Akutwa akiwa na kucha za watu, vipande vya sabuni vilivyotumika, nguo ya mtoto mchanga, kisu, sindano, nyembe, nyama iliyokaushwa pamoja navitu vingine vingi ambavyo  sikuweza kuvitambua angalau hata kwa jina.

BINTI APONYWA MACHO
Regina Josias mwenye umri wa miaka 15, mwanafunzi wa kidato cha 2 katika shule ya sekondari ya Bushabani.
Ni binti amabaye anajitahidi sana katika masomo hali kwamba anaongoza kila jaribio au mitihani ya ndani na nje  ya mkoa yaani kufeli kwake yeye anakuwa mtu wa pili.
Ililikuwa mwezi wanne mwaka jana 2013 binti huyu akiwa anajiandaa na vipindi vya darasani asubuhi  siku ya jumatano, alishikwa  ghafla na ugonjwa wa macho hali ambayo ilisababisha hata asiweze kusoma
Lakini ugonjwa wa binti huyu ulinishangaza kidogo kwani aliweza kusoma vitbu vya katuni na magazeti  ambapo ukimpa daftari au kitabu ya darasa au chochote kinachohusiana na shule, hakuweza kuona kabisa.
Siku moja aliona nyoka darasani wakati wanafanya mitihani ya mock mwaka huu, ndipo hali ilizidi kuwa mbaya na kurudishwa nyumbani kwa wazazi wake; Nao wazazi wake walidai kwenda kwa mganga lakini Regina alikataa na kusema siwezi kwenda huko ila npelekeni kanisani, akaendelea kusema nasikia kuna kanisa lipo Msanga linaponya watu wenye matatizo mabalimbali.
Ndipo wazazi wa Regina waliamua kumleta katika kanisa ambalo linaponya watu wenye magonjwa na shida mbalimbali linaloitwa UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.
Baada ya kuombewa, Regina kawa mzima kabisa, anaweza kusoma vizuri.
Sasa kawa manajeshi wa UFUFUO NA UZIMA, anarudi shule kusoma  kwa nguvu mpya mpaka ndoto yake itimie.     
 

 

 

Ushuhuda wa  Jesca aliyekuwa kichaa
Jesca alikuwa na tatizo la kuchanganyikiwa akili,  lakini cha kushangaza zaidi kichaa huyu aliwataka ndugu zake wamlete katika kanisa la (Glory) Ufufuo na Uzima Kigoma.
Baada ya Jesca kufikishwa katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma, kaombewa na sasa ni mzima kabisa.
        

 Dondandugu lanyaushwa leo na damu ya Yesu; Ufufuo na Uzima-Kigoma
Bibi huyu alikuwa akiteswa na kidonda ambacho kilikuwa katika sehemu ya mguu wake kwa muda wa miaka 10 bila kupata nafuu yoyote, leo afanyiwa muujiza(uponyaji) na Bwana Yesu katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Kigoma.

 


Atanas apata kuona tena!
Ni mwanafunzi [darasa la nne]; Alirudi nyumbani kutoka shule akidai kuwa macho yanamuuma sana hatimae akashindwa kabisa kuona kwa nuda wa miezi 2.
Baada ya kufika kanisani Ufufuo na Uzima Kigoma, ameweza kuona tena {amepona kabisa}.



Mama Atanas akiwa na mtoto wake Atanas akimshukuru Mungu kwa muujiza mkubwa alioufanya kwa mwanae. (uponyaji wa macho). Ufufuo na Uzima Kigoma.

 

 

ESTA ARUDISHWA!
 ALIKUWA KWENYE CHUMBA CHA KAKA MMOJA [MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU] AKIMFANYIA MITIHANI. YAANI KUTUMIA AKILI ZA DADA HUYU (ESTA), KAKA YULE HUWA AKIFANYA VIZURI KATIKA MASOMA YAKE.


REHEMA
 ARUDISHWA KUTOKA MLEBA BUKOBA. ALIKUWA KAFUNGWA KWENYE MGOMBA NA MAMA MKUBWA.
   [ALIKUWA ANASINZIA DARASANI KILA MWALIMU ALIPOINGIA].

  

 MRS.ELIAS (KATIKATI) AKISHUHUDIA JINSI ALIVYOKUWA AKITESWA NA UGONJWA WA TUMBO KUJAA MAJI, KUVIMBA MIGUU NA VYURA WATANO (5) WALIOKUWA WAKIRUKARUKA KATIKA TUMBO LAKE, TANGU MWAKA 2000-2013; ALIJAZA NDOO YA MAJI PINDI WATAALAM WA AFYA WALIPOJARIBU KUTOA MAJI YALIYOKUWA TUMBONI MWAKE.

HAKUWEZA KUFANYA SHUGHULI ZA NYUMBANI KWAKE KWA MUDA WA MIAKA 12, HUKU MUME WAKE (MZEE ELIAS/KUSHOTO) AKIFANYA KAZI ZOTE ZA NYUMBANI. 

BAADA YA MAMA HUYU KUPONA;

 KUNA BAADHI YA WTU WALIOMSHUHUDIA KIPINDI ANAUMWA,  NAO WAMEAMUA KUOKOKA. [UFUFUO NA UZIMA KIGOMA]


 
MZEE ROBERT

 ALIKUWA NA TATIZO LA KUTAPIKA DAMU KWA MUDA MREFU HALI AMBAYO ILISABABISHA ASIJITAMBUE KABISA; BAADA YA KUFIKA KATIKA KANISA LAUFUFUO NAUZIMA KIGOMA NA KUOMBEWA, MZEE HUYU MPAKA SASA ANAJITAMBUA WALA HATAPIKI DAMU TENA, YAANI NI MZIMA KABISA.


MAMA IDIRISA (ASIA EMMANUEL) 

AKIMSHUKURU MUNGU [UFUFUO NA UZIMA KIGOMA]

BAADA YA KUPONYWA UGONJWA WA MGUU ULIOMSUMBUA KWA MUDA WA MIAKA 15.

 

DADA HUYU (ANNA NANSO),  ALIKUWA KAOLEWA NA JINI HALI AMBYO ILISABABISHA AACHANE NA MUME WAKE.

APATA TARAKA YAKE BAADA YA JINI HUYO KUONA MOTO WA MAJESHI YA UFUFUO NA UZIMA UMEKUWA MKALI KUPITA MAELEZO.





MAMA HUYU ALIKUWA AMEPOOZA UPANDE MMOJA WA KUSHOTO, APONYWA UGONJWA HUO BAADA YA MAOMBEZI MAKUBWA YA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.

 IJUMAA 17.01.2014


UJAUZITO ULIOKUWA UMEPOTEA MIAKA SITA ILIYOPITA, SASA UMEONEKANA TENA!!!
Ni baada ya mama huyu kufika katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma akiwa na shida kwamba amechoshwa na maisha hivyo alikuja kuombewa afanikiwe katika maisha yake lakini kulingana na jina la kanisa hili "UFUFUO NA UZIMA" Kanisa linalofufua na kurudisha vilivyopotea, mama huyu alijikuta tumbo lake linazidi kukua/kuongezeka, hivyo aliona ni vyema aende kupima ili kujua tatizo lakini cha ajabu na cha kushangaza alionekana kuwa anaujauzito wa miezi minne na nusu!
Baada ya kuhijowa na Mchungaji kiongozi Paul Joshua kwamba amepataje ujauzito huo ambapo anasema mume wake alifariki mwaka 2008?
Mama huyu alidai kuwa mume wake alimuacha akiwa na ujauzito wa miezi miwili lakini baadae ulitoweka na hakujua umepteaje. 


AKIMSHUKURU MUNGU KWA MUUJIZA MKUBWA ALIOMTENDEA, BAADA YA UJAUZITO WAKE KURUDI/KUONEKANA TENA.








MARIA  JOHN BINTI MWENYE UMRI WA MIAKA 16 NI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI KITWE KIGOMA MAKISHUHUDIA JINSI ALIVYOCHUKULIWA NA KUFUNGWA MINYORORO CHINI YA MAJI KATIKA ZIWA TANGANYIKA.
ANASEMA ALIANZA KUHISI KIZUNGUZUNGU AKIWA DARASANI PALEPALE AKAWA AMEPOTEZA FAHAMU, TENA ANAENDELEA KUSEMA BAADA YA KUFIKA KULE ALIFUNGWA MINYORORO MIGUUNI NA MIKONONI MARA AKAANZA KUSIKIA SAUTI INAITA "MARIA  NJOOOOOO!" PALEPALE MINYORORO ILIKATIKA NA KUSHTUKA YUPO KANISANI UFUFO NA UZIMA KIGOMA.
"SIFA NA UTUKUFU APEWE BWANA YESU"


MAMA MARIA JOHN AKIMSHUKURU MUNGU KWA MUUJIZA MKUBWA ALIOUFANYA KWA MWANAYE KUMTOA KATIKA MINYORORO ALIYOKUWA AMEFUNGWA NA SHETANI CHINI YA MAJI KATIKA ZIWA TANGANYIKA.





MZEE HUYU ALIYEKUWA MGANGA WA KIENYEJI TANGU MWAKA 1972 LEO AMEOKOKA,  AOMBEWA NA KUPONYWA MISHALE ILIYIKUWA IKIMSUMBUA KATIKA KIFUA CHAKE.  HAPA AKIWA NA MKE WAKE KWENYE MADHABAHU YAUFUFO NA UZIMA KIGOMA  03.11.2013.


 MZEE HUYU ANASWA NA MAJESHI YA UFUFUO NA UZIMA!
MZEE HUYU AMEKUWA AKISUMBUA FAMILIA YAKE KWA MUDA  MREFU AKISADIKIKA KUWA NI MCHAWI, AMESHAHARIBU WATOTO WAKE WATATU {3} KWA KUWAFANYA VICHAA!


  
 

 ASHURA  SAID AOKOKA!
Aja na ushuhuda mkubwa kuhusu kazi za wachawi alizokuwa akitumikishwa na shetani; aliwahi kuhudhuria kikao katika bunge la wachawi Dodoma. Viti walivyokuwa wakikalia wakuu wa kikao ilikuwa ni migongo ya watu  wanainama halafu wakuu wa kikao wanakalia kama viti.



Dada huyu akimshukuru Mungu kwa muujiza aliomtendea; Alikuwa hawezi kugeuza shingo kwa muda wa miezi sita lakini  baada ya kuombewa katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma sasa ni mzima kabisa.




 HAPO PICHANI, NI SNP  PAULO  JOSHUA WA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA AKIMHOJI MAMA  HUYU (MLEMAVU WA MACHO) AMBAYE ALIKUWA DUKANI KWA MTU AKIMUUZIA VITENGE. 



 NI MUUJIZA!
 MUUJIZA MKUBWA ULIOFANYIKA KWA DADA HUYU, WAKATI WA UJAUZITO WAKE UKIWA NA MIEZI  8, MTOTO ALIACHA KUCHEZA TUMBONI, MADAKTARI NA MATABIBU  WALIPIMA NA KUONA MTOTO AMEKUFA.
LAKINI ALIPOFIKA KWENYE KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA  ALIOMBEWA NA  AMEJIFUNGUA SALAMA MTOTO WA KIUME






BINTI MCHAWI ANASWA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA
SNP  PAULO  JOSHUA WA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA TANZANIA AKIWA NA BINTI AMBAYE ALIKUWA MCHAWI  (MKAZI WA MAGU MWANZA) NA KAZI YAKE KUBWA ILKUWA  NI KUINGIA HOSPITALINI  KUCHUKUA WATOTO KISHA NA KUWAACHIA MIDORI.
NA HAPO PICHANI ANAONYESHA JINSI ALVYOKUWA AKISAFIRI KUTUMIA FUVU LA MTOTO MCHANGA.



 


MISUKULE WANARUDI!!!
 Anaitwa Betrice {Mama Paschal} akishuhudia jinsi alivyoishi maisha ya usukuleni yaliyojaa mateso makubwa!
Mama huyu alichukuliwa kichawi {msukule} miezi miwili ilyopita, alisikia sauti za watu asiowajua zikimuita  huku mume wake aliachiwa mwanamke {pepo lililovaa sura ya mke wake}.
Alipofika kule alikabidhiwa kulinda shimo kubwa la misukule wasitoroke, alikuwa akikija usiku kuwatembelea mume wake na mtoto wake Paschal bila wao kumuona hata kazini kwa mume wake aliweza kuingia na kula, kunywa maji bila mume wake kujua wala kuona chochote.
Lakini baada ya maombi makubwa ya kurdisha waliochukuliwa mateka/misukule yanyofanyika katika kanisa la ufufuo na uzima kigoma 
alisikia sauti za watumishi wa Mungu zikiita NJOOOO KWA JINA LA YESU ndipo wahusika waliokuwa wamemchukua walishindwa kupinga sauti ya Mungu wakaamua kumuachia na hivi sasa yupo huru.  






Bitrice {mama Paschal} akiwa na mume wake {baba Paschal} kwenye madhabahu ya ufufuo na uzima Kigoma



Binti huyu akilia kwa uchungu baada ya kurudi kwenye halisi ya mwili wake baada ya kurudishwa; Anasema alikuwa Musoma akiuza bidhaa sokoni kwa muda wa miaka sita.







Maajabu Kigoma
Dada huyu amkana mtoto wake baada ya kurudishwa, anadai kuwa mtoto wake kamuacha msukuleni na siyo huyu aliyenaye sasa.





Anusurika kung'olewa jicho.
 Mganizi akimshukuru Mungu katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma  baada ya kuponywa jicho lililokuwa na nyama za ndani zimetoka nje sasa ni mzima kwa jina la Yesu.




Mama huyu kutoka Bukoba mkoani Kagera akimshukuru Mungu katika madhabahu ya ufufuo na uzima kigoma baada ya mtoto wake kuponywa ugongwa wa ajabu
Mtoto huyu alikuwa anakula kinyesi chake akisha maliza kujisaidia  pia alikuwa  akilia sana na kukwaruza makucha yake  kama mnyama mwilini kwa mtu yeyote aliyejitokeza kumshika.
Mama huyu alihangaika sana kwa kutafuta tiba ya mtoto wake kwa muda wa miezi mitano bila mafanikio yoyote, lakini baada ya kusikia kanisa la ufufuo na uzima kuwa lina Mungu asiyeshindwa na lolote ndipo aliamua kukimbilia kwenye kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma   akafanyiwa maombezi makubwa  chini ya kiongozi SNP  PAULO   JOSHUA na sasa ni mzima kabisa





SNP  PAULO JOSHUA WA KANISA LA UFUFUO NAUZIMA KIGOMA AKIMHOJI BIBI HUYU BAADA YA KURUDISHWA; 
BIBI HUYU ANASEMA ALIKUWA KAHIFADHIWA DUKANI KWA MTU.


 
NI BAADA YA KURUDISHWA  KAKA HUYU {YAMUNGU MLEMAVU WA MIGUU} AKIELEZEA MAISHA ALIYOKUWA AKIISHI MSUKULENI


 ALIKUWA  AKIFANYISHWA  KAZI ZA HOTELI  HUKU  AKIDAI  CHAKULA CHAO KILIKUWA  NI NYAMA  ZA KUOZA


HUYU NDIYE MKEWAKE YAMUNGU {FAMILIA YAKE KUSHOTO}

KUWAOKOA WALIOMEZWA NA SHETANI.

BAADA YA SOMO LA LEO 15.9.2013 LIKIAMBATANA NA MAOMBEZI MAKUBWA YA "KUWAOKOA WALIOMEZWA NA SHETANI" 
MAMA HUYU AKIWA NA MSHANGAO MKUBWA ANAULIZA HAPA AMEFIKAJE HUKU AKIDAI KUWA YEYE SIYO MKRISTO NA ALIKUWA ANAISHI MAKABURINI AKIPALILIA MASHAMBA YA MUME WAKE!

HAPA ANALIA AKITAKA  AWAONE WATOTO WAKE PAMOJA  NA MAMA YAKE MZAZI






BAADHI YA  WAUMINI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MASANGA KIGOMA TANZANIA.





KIJANA HUYU ( KAWAYA) ALIYEKUWA KICHAA 

  ANAMUSHUKURU MUNGU KWA KUMPONYA UKICHAA HUO HIVYO MUNGU WETU WA ISACKA NA YAKOBO NI MUNGU ASIYESINDWA KITU




ANAITWA MGISHA YUNUSLAUS KUTOKA BUKOBA KWA SASA ANAISHI  KIGOMA  ALIKUWA ANAFANYA KAZI YA KUWANYONYA WATU DAMU  YAPATA MIAKA MIWILI (2) AKIWA YUPO KIGOMA LAKINI KAZI HII YA KUNYONYA DAMU ZA WATU ALIKUWA ANAENDA SEHEMU MBALIMBALI NA KAZI HII ALIIFANYA BILA  MTU YEYOTE KUJUA   NA SASA AMEAMUA KUMPOKEA YESU KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE KATIKA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA MASANGA KIGOMA TANZANIA.  Kwa maelezo zaidi unaweza kupitia   ufufuonauzima.kigoma@gmail.com





MAMA HUYU  {ANASTAZIA}   KUTOKA KIJIJI CHA KIDEA  KIGOMA TANZANIA  AKIMSHUKURU MUNGU BAADA YA KUSUMBULIWA NA UGONJWA WA KIFAFA KWA MUDA WA MIAKA MITANO{5}
LAKINI BAADA YA  MAOMBEZI  KATIKA KANISA  LA GLORY{UFUFUO NA UZIMA } KIGOMA ,   SASA  AMEPONA KABISA .  YESU ANAWEZA  AMINA.






 KICHAA APONA 
 Anaitwa Judith  mkazi wa kibirizi Kigoma alikuwa kichaa kwa muda wa miaka mingi lakini baada ya  kufika katika nyumba ya ufufuo na uzima - kigoma ukichaa huo ulitoweka na sasa anamtumikia Mungu   maisha yake  na kupata badaka nyingi sana kutoka kwa SN: PAUL JOSHUA wa kanisa laUFUFUO NA UZIMA KIGOMA TANZANIA




TASA APAKATA MTOTO
Unaemuona hapa juu kapakata mtoto, anaitwa Grace akiwa na mume wake,  alikuwa na tatizo la utasa(kutokushika ujauzito) kwa muda wa miaka mitatu(3), lakini baada  ya kufika katika kanisa la Glory(Ufufuo na Uzima) lililopo Masanga Kigoma Tanzania, nakufanyiwa Maombezi, kampata mtoto. Jamani Mungu anaweza mambo yote.


MOYO KUPANUKA
   Mektrida Issa mkazi wa Katonga Kigoma; alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kupanuka kwa muda wa mwaka mmoja sasa amepona ugonjwa huu baada yakufanyiwa maombezi makubwa katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma. 





APONA UKIMWI
   Anna Malgesi Mkazi wa Burega-Kigoma, anamshukuru sana Mungu kwa mambo makubwa aliyomtendea. Kwa mujibu wa wataalam wa afya inasemekana kwamba UKIMWI ni ugojwa usiotibika lakini kwa mujibu wa neno la Mungu nikwamba; Hakuna jambo linalomshinda Mungu. Alikuwa mgonjwa wa UKIMWI kwa muda wa miaka 10, baada ya kufika katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma, aliombewa akapona UKIMWI nasasa ni mzima kabisa!


                                 
UVIMBE WA MIAKA KUMI WAYEYUKA!
Dada huyu  "RACHIEL"  akiwa na SNP:Paul Joshua kwenye madhabahu ya Kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma; kwa furaha kubwa amesimama madhabahuni hapo kushuhudia muujiza ambao Bwana kamtendea kumponya ubavu uliomsubua kwa muda miaka kumi.




 Binti huyu akiwa amesimama na Mchungaji kiongozi Paul Joshua katika madhabahu ya kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma baada yakutembea! 
 Kutokana ugonjwa wa miguu uliomsumbua "Biti Mlela" alikuwa akitembelea fimbo kwa muda wa miezi mitatu lakini sasa ameiacha fimbo hiyo baada ya kuombewa na kuponywa ugonjwa huo katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma.

 
JACKSON  NOAH AKIWA AMESIMAMA KWENYE KABURI LAKE KIJIJINI KWAO BUBANGO KIGOMA










 RP Esta Paul wa kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma akiwa amesimama kwenye kaburi la Jackson Noah kijijini Bubango




 Mtoto Dickson Dismas akiwa amekufa


 Wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma wakimfufua mtoto Dickson aliyekuwa amekufa siku ya Alhamisi tarehe 18.04.2013 Jioni.


 Mama Dickson {Happyness Joseph mkazi wa Majengo Kigoma}
  akishuhudia matendo makubwa ya Mungu kwenye madhabahu ya Ufufuo na Uzima Kigoma aliyoyafanya kumfufua mtoto wake



 Mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma akiwa amembeba mtoto Dickson aliyekuwa amekufa





  Jenipha Joshua
 Aliugua ugonjwa wa kisukari kwa muda wa miaka kumi. Kwa sasa anamshukuru Mungu kwani baada ya kufika katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma, aliombewa na akapona; sasa  ni mzima kabisa.





                                                               Asante Yesu
 Yusta Robart aliyekuwa mwathirika wa UKIMWI kwa muda wa miaka mitatu, apona ugonjwa huo katika kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma.






Yusta Robart akiwa amesimama kwenye madhabahu ya kanisa la Ufufuo na Uzima
Akimshukuru Mungu  kumponya UKIMWI




Magreth Smail
Mkazi wa Manyovu Kigoma, niliugua kifafa kwa muda mrefu 
lakini baada ya kufika katika nyumba ya Ufufuo na Uzima Kigoma aliombewa akapona kifafa na sasa ni mzima.



 Kijana Yusuph amesimama madhabahuni {UFUFUO NA UZIMA KIGOMA}, Kujisalimisha na kazi za shetani alizokuwa akizifanya ikiwemo UCHAWI naWIZI!





SNP Paul Joshua akimuongoza sala ya toba kijana Yusuph aliyekuwa mwizi na mchawi siku ya Alhamis tarehe 25.04.2013 jioni
{Mama Yusuph "Christina" akiwa amesimama upande wa kushoto}




Bitrice {mama Paschal} akimshukuru Mungu kwa kujifungua salama baada ya kukaa na ujauzito kwa miezi 11.
Pembeni ni mume wake {baba Paschal} akiwa amebeba mtoto wake kwa furaha


SNP Paul Joshua wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Kigoma akiwa na "Bestha Mdaila" binti mwenye umri wa miaka 12 aliyekuwa mchawi kwa muda wa miaka mitatu   

 
Betha Mdaila akielezea jinsi alivyokuwa anafanya kazi za kichawi ikiwemo "kuchukuwa watu misukule"
alianza kazi ya uchawi mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka tisa.



KANISA LA UFUFUO NA UZIMA KIGOMA MWAKA 2007