MAJI MATAMU
NDANI YA MWAMBA MGUMU _na Mchungaji kiongozi Paul Joshua.
Maji ni ya muhiumu sana katika maisha ya watu, wakati wa
Israeli wanasafiri walipofika jangwani na kukosa maji walimlilia Musa. Mungu
akamwanbia Musa auambie mwamba utoe maji.
HESABU 20:1-8
Kuna kitu kinaonekana kama mwamba katika kmaisha yako, Mungu
huwavuta watu mpaka jangwani ambapo hakuna tumaini, ili mwamba utakapotoa maji
atukuzwe katikati yao, nakipindi ambacho Mungu anawapeleka watu wake jangwani
wao hulalamika nakuona Mungu anawatesa nakutamani bora angewaacha kulekule walipokuwa.
Leo lazima mwamba wa maisha yako utoe maji kwa jina la Yesu,
inawezekana biashara yako ni mwamba, ndoa yako ni mwamba pengine hata huduma
yako ni mwamba, LEO UTOE MAJI KWA JINA LA YESU. Amina.
Sehemu ambapo unaona huwezi hapo ndipo inapowezekana, ndani ya mwamba kuna maji na ndani ya mzoga kuna asali.
Inawezekana kila sehemu unaona haiwezekani lakini hapo tayari Mungu kaachilia
jibu lako, usiogope kuona mwamba kwani ndani yake kuna maji matamu, usiogope
kuona magumu kwani ndani yake kuna mafanikio.
Usitegemee kupata mafanikio katika mambo malaini, lazima
ukubali kuupiga mwamba ili maji yatoke katika maisha yako, unywe maji matamu,
kubali kupita jangwani maana huko ndiko kuna mwamba wa maisha yako, usiogope
kupita jangwani.
KITU CHA KWANZA Mungu anakuokoa halafu anakupeleka
jangwani,hata Yesu alizaliwa akakua, naalichukuliwa na roho mpaka jangwani kwa
siku 40, yawezekana Mungu kakuweka jangwani, watu wote amabao Mungu aliwainua,
aliwainua katika wakati mgumu, kuna kipindi ambacho unapitia unaona jangwa,
unafunga lakini upo jangwani, ndugu hata Yesu alifunga na kuomba lakini
aliingia jangwani.
Mungu akamwambia Musa, auambie mwamba utoe maji, mwamba
ulisikia, mwamba wowote uliopo unasikia wewe uambie nao utatii, ndoa yako
inasikia, biashara yako inasikia, magonjwa yanasikia, wewe sema neno nayo
yatatii.
Mwanzo16:1
Unaweza ukapita katika magunu nakuona kama Mungu kakuacha, Sara alimwambia Ibrahimu apate
mtoto kwa Hajiri maana aliona Mungu kamsahau, lakini Mungu alikuwa
ameshawaahidi kuwapa mtoto. lakini baada ya Mungu kukawia akaona Mungu
kamsahau.
Mungu si mtu hata aseme uongo na tena habadilikibadiliki,
hivyo; tujifunze kumngoja Mungu.
Brikiwa