SOMO LA LEO_ TAREHE 22/3/2015_MADHABAHU YA UKOO/FAMILIA: SNP
PAUL JOSHUA
ZABURI 30:11 uligeuza
matanga yangu kuwa matanga yangu kuwa machezo; ulinivua gunia ukanivika furaha. Kumbe kuna kuvikwa gunia, inawezekena ikawa
gunia la mikosi, laana,umaskini na magonjwa lakini leo yesu anakwenda kukuvua
gunia hilo.
ZABURI 27:1-14
shetani alichofanikiwa kabala ya injili kuja ni kuingiza
roho zake ndani ya watu, hivo akili za watu zikajengwa kuwa ili ufanikiwe
lazima upitie kwa waganga wakienyeji au wazee.
Waamuzi 6:1 wana wa Israel walianza kuonewa, nao wakamuitia
Mungu na kumueleza juu ya kilio chao,Mungu akawaambia amewaacha kwakuwa
wametumikia miungu, ukitenda dhambi yoyote ile unarudi nyuma na unampa shetani
uhalali wa kukushambulia.
Waamuzi 6:25- Mungu alimwambia Gideoni aiangushe madhabahu
ya baba yake na kuyakata maashera, kumbe unaweza ukapata shida lakini shida imezanzia
katika ukoo wako na inawezekana akawa ni baba, bibi au mjomba au shangazi
anamadhabahu ambayo yanatesa ukoo.hivo kufanikiwa kwako ni lazima uangushe
madhabahu hiyo kama alivyofanya gideoni.
Mwanzo 4:8 Matatizo
mengi ya watu yameanzia kule walikozaliwa, na hii inatokana na kuoneana
wivu.wivu unafanya watu wauane hasa ndugu, hakuna adui mkubwa kama ndugu,
Kainia alimuua nduguye Habili kwakumuonea
wivu baada ya kukubaliwa na Mungu.
Kuna mtu amekaa kwa namna ya shangazi au bibi au mjomba ndio anayetesa ukoo wenu. Kuna mtu katika ukoo
anayetunza madhabahu na madhabahu hii
ndio inayosumbua familia yenu au ukoo wako. Na kila ukoo unaye mkubwa au msemaji
wa ukoo anayetunza madhabahu kwaajili yakuangusha
Matatizo yanatokea katika sehemu kuu zifuatazo:-
1.
Kutoka katika ukoo au familia, kama kwenye ukoo
wenu kuna mchawi hiyo ni hatari sana
Na kila mwaka wachawi wana kafara kila
unashangaa kila mwaka kuna mtu anakufa kumbe yupo mtu anayewamaliza na anawatoa
kafala ili kuimarisha madhabahu yake. Na kama kuna mchawi kwenye ukoo ni ngumu sana
kuinuka kwani lazima atakuwa amejenga madhabahu
na jina lako lipo ndani ya madhabahu hiyo. Ogopa sana wakala wa shetani
akiwa ndani ya ukoo maana anawamaliza na
kuwatesa , bahati mbaya sana kama wako wengi na ukitaka ufanikiwe kaa mbali na
nyumbani kwenu maana adui kwanza ni yule wanyumbani kwako.
2.
Shida zinatokea kule uliko olewa, ukoo
mwingine ni tata. Unaolewa na mme ambaye
ukoo wake wote ni wachawi . angalia shida ya nyumbani kwenu inatokea wapi, kuna
mtu katika ukoo wenu anayewaliza
Tunaomba juu ya maeneo makuu mawili yafuatayo:-
1.
Kuvunja madhabahu za ukoo
2.
Kama kwenye ukoo kuna mganga wa kienyeji au
mchawi, mfyeke na kushambulia madhabahu
yake.