SOMO LA
JUMAPILI TAREHE 10 MAY, 2015 NYOKA WA KICHAWI: SNP PAUL JOSHUA_UFUFUO NA UZIMA KIGOMA
ZAB 23:1-6 Bwana ndiye mchungaji wangu
sitapungukiwa na kitu, katika malisho ya majani mabichi hunilaza kando ya maji
ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia za haki
kwaajili ya jina lake, naam nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti sitaogopa
mabaya. Kwa maana wewe upo pamoja name, gongo lako na fimbo yako vyanifariji ,
wanaandaa meza mbele yangu , machoni pa watesi wangu umenipaka mafuta kichwani
pangu na kikombec hangu kinafurika hakika wema na fadhiri zitanifuata. Siku
zote za maisha yangu name nitakaa nyumbani mwa bwana milele.
UFUNUO 12:7 Kulikuwa na vita mbinguni Michael
na malaika zake wakapigana na Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika
zake . nao hawakushinda hata mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa Yule mkumbwa nyoka wa
zamani aitwaye ibiisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata
nchi na malaika zake wakatupwa pamoja naye, nikasikaia sauti kuu mbinguni
ikisema sasa kumekuwa wokovu na nguvu na ufalme wa mungu wetu na mamlaka ya
kristo wake kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu yeye awashitakiye
mbele za mungu wetu mchana na usiku.
Kiumbe wa
kwanza aliyejenga uadui na mungu ni nyoka, kiumbe ni kiumbe aliyekuwa wa kwanza
kulaaniwa hana miguu anatembelea kwa tumbo,ni kiumbe aliye mjanja kuliko
wanyama wote, kwa ujanja wake ameshaingia kwenye ndoa yako, kwa ujanja wake
ameshaingia kwenye kazi yako. Ndiye kiumbe wa kwanza kutumiwa na shetani kwa
kuvaa sura yake, kiumbe ambaye anameza bila kutafuna, Yule uliyedhani kuwa ni
nyoka kumbe ni shangazi au bibi yako anavaa sura ya nyoka, Yule yule aliyefanya
vita na Michael ndiye anafanya vita na ndoa yako, maisha yako, lakini huyu joka
hakuweza kushinda hata wewe hawataweza
kukushinda wala mahali pao hapakuonekana kumbe ana sehemu yake hata kwako
anaweza akawa ana sehemu, joka anaweza kufanya vita na maisha yako,
Kwenye ngazi za malaika kuna malaika maselafi
na makerubi, shetani alikuwa ni rusifa hata alipoasi aliondoka na kundi la
malaika wengi anaweza akaingia kwako akaondoka na familia yako, kazi, ndoa yako
lakini leo lazima tumkate kichwa kwa jina la yesu kristo. Lakini leo
tunamtangazia hataondoka na mtu atatoka peke yake. Shetani alifanya vita
mbinguni akapigana kwa baba yetu mbinguni leo hii ndio maana shetani huwezi
kumtoa kirahisi lazima ujifunze kupigana vita vya rohoni anaweza kushindana na
familia yako au na kanisa. Jina lingune la shetani ni mshitaki wetu anawashitaki
watu wa mungu ufalme wa giza unafanya kazi pamoja naye ukiona mchawi amevaa
sura ya paka au fisi huyo ni mchawi mdogo, ukiona sura ya nyoka ujue shetani
mwenyewe ameizunguka nyumba yako ili kukuangamiza. Shetani mwanzo alikuwa
kwenye kitengo cha kusifu na kuabudu akaona kwanini awe anamsifu mungu akaamua
ajiinu hata akafanya vita na kuasi mbele za mungu, hata mtoto wako anaweza
kuamua kujiinua na kuamua awe yeye ndo mkubwa anaweza kukwambia ungechelewa
kunizaa ningekuzaa mimi.
Anayefanikiwa kumkimbia nyoka huyu ndiye anafanikiwa
katika maisha katika kazi, joka huyu ni mkumbwa ambaye anaishi ziwa Tanganyika
akiona mtu anafanikiwa anakwenda kumuondolea amani kwenye familia yake. Leo
tunasema na Yule joka aachilie ndoa kazi aiachilie kwa jina la yesu, kuna
nyoka, nyoka akizingira familia mmekwisha, nyoka akimzingira binti hata ajipake
wanja haolewi, akazingira nchi hakuna kufanikiwa maana yake kuna joka
amezingira nchi yetu ili iendelee kuwa maskini.
Tumechanganyikana kati ya wana wa mungu
na ibilisi na malaika zake lakini mungu anasema walio wake anawajua kumbe wapo
ambao sio ni wa mungu wanaimba lakini sio wa mungu wanaomba lakini sio wa
mungu, unaweza ukaimba sana lakini wewe ni wa shimoni, imeandika na uzao wa
mwanamke utakuponda kiwa lazima tukuponde kichwa pale mahali alipo kwenye
familia yangu kwenye kazi yangu nakuponda kichwa. Joka huyu ana uzao ndio maana
kuna uzao wa nyoka mtu unamuona kavaa vizuri lakini asili yake ni wa kuzimu
anakuja kanisani ananena kwa lugha sio kila anaye nena ni wa mbinguni maana
shetani naye hujigeuza ili afanane na
malaika watakatifu.
Nyoka huyu anapona mtu amesimama kiroho lazima
amdanganye anapomuona binti amesimama katika imani anakuja kama hendsome
anasema amefunuliwa ameonyeshwa na mungu ameona anatembea na wewe umevaa shela
ni muongo lazima nyoka aliyetumwa ameze maisha yako, mtaji wako,au kanisa leo
lazima tumwangamize kwa jina la yesu, mungu alisema nitaweka uadui kati yenu na
nyoka, mungu leo anaachilia mzigo wa mawe yatakwenda kwenye familia yako
yatakwenda ujiji,ziwa Tanganyika na Tanzania yote kila aliyekufunga ajiandaye
kupondwa kwa jina la yesu. Imeandikwa vita si yetu ni ya bwana, anayekugusa
wewe anagusa mboni ya jicho la mungu leo majeshi ya mungu yanasambalatisha
kabisa.
Wakati
mwingine ni ndugu yako anakuja kwa sura ya nyoka siyo nyoka huyo ni mchawi
anakuja kwa sura ya nyoka, Ufufuo na uzima tumeitwa kusema usiku na mchana juu
ya yeyote anayevaa sura na kujigeuza kuwa nyoka tunasema na Tanzania hatutanyamaza
hadi tuone ufalme wa Tanzania umegeuzwa na kuwa ufalme wa mwanakondoo,
ukichezea bomba likipasuka linakulowanisha shetani amegusa ufufuo na uzima na
tunasema usishindane na aliyetumwa lazima tutashinda na mahali pako
hapataonekana tena, kuna mtu anakutesa lakini ni wa shimoni anasema huwezi
kumjua kwakuwa amvaa sura na amejigeuza ni joka huyo anasema bwana asifiwe kama
wengine anaimba kama wengine, lakini roho hazifanani pamoja unasema utukuru
pamoja unasema bwana asifiwe, pamoja unanena lakini wewe si mwenzetu ni wa
kwenye shimoni ukijifanya roho amekushuhudia lazima tukujue tu kwa jina la
yesu.
LIKA 10:19 Nilimuona shetani akianguka kutoka
mbinguni kama umeme, Tazama nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu
zote za Yule adui wala hakuna kutu kitaweza kutudhuru.Leo tuna kazi moja tunakanyaga nyoka na nge
mahali alipo anawasiwasi kwamba tunamrudisha kuzimu,saa zingine huyu joka uko
naye kwenye nyumba kama binti wa kazi au ni mchumba wako akajenga urafiki wa
siku chache tu anakuwa kashajua mambo yako yote kwa lengo la kukuchota na
akishakuchota amekumaliza, Mfano Samsoni aliweza kupiga wafilisti elfu mbili,
akachukua mbweha akawafunga mikia akawasha moto wakaingia kwenye mashamba ya
wafilisti.
Shetani ukimsumbua sana anaunda tume ya
upelelezi je anatumia nguvu gani mbona anazidi kufanikiwa hata anasonga mbele
tu lakini wa mbinguni huwa hashidwagi wanaamua wakuchunguze chanzo cha nguvu
zako ni nini, wafilisti wakafikilia samsoni huyu tumfanyenyeje, hata wewe
unawindwa adui zako wanafikilia kuomba unakoomba unawasumbua mtaani kweny wakufanyeje,
Delila alikwenda kwa nia ya kumdanganya samsoni wala siyo nia ya kuolewa
alikuwa ni nyoka huyu kavaa sura ya binadamu maana imeandikwa; Tutawatambua kwa
matendo yao wala usiwe na halaka mchumba anakuja. Kama unaomba sana kwenye ukoo
au familia yako halafu kukawa kuna vigagula unabomoa madhabafu za familia,
kikao kinaundwa nini siri ya nguvu zake nini siri ya upako wake siri ni kuacha
vyote na kuamua kumfuata yesu maana ukimfata yesu atakulinda ndio maana mungu
anasema acheni dhambi lakini kuacha vyote si rahisi maana yesu amesema sikuja
kuleta amani duniani maana inawezekana unaomba kumbe mama ana shamba la
misukule unapiga majeshi unaangamiza unadai nyota yako kumbe kaka yako ndiye
mwizi wa nyota yako, unaweza ukainukiwa na ndugu zako.
Delila
alikuwa symbols ya shetani wakamuuliza tunamshikaje samsoni, wakamwambia wewe
ndio mrembo kuliko wote hapa nchini,
akaambiwa nenda kuna dau hapa umnase samsoni, kuna watumishi wengi wamenaswa na
mtego wa shetani unaolewa na hajaokoka unataka kwenda kwenye mkesha anakwambia
rudi ndani, unashangaa anachukua panga ananoa kila siku halafu anaweka ndani
omba sana ni kwaajili yako wewe, Joka aliyemshika adam na eva ndiye aliye
mshika samsoni maana hakuwatii wazazi wake walimkataza delila hakuwa na nia ya
kuolewa alitaka tu kumpeleleza samsoni kwa sura ya binadam. Usipende kulopoka
kwa watu juu ya maisha yako unatoa siri za nyumbani kwako utalia kuna mtu
anakutesa na kukuliza amejificha kwa namna ya joka, usiende sehem bila kuomba
muulize mungu wenzako walizama Biblia inakataza kuolewa na mtu asiyeokoka
usifuate mali mfuate yesu usifuate nyumba kazi utajiri huwaga zinaisha kuna
kufukuzwa kazi kuna kupata na kukosa olewa na mtu unayemfaham fika wengine ni
majoka wanatumiwa na ibilisi, delila alikuwa amevaa sura ya mrembo tu ili
kumpeleleza samsoni kuna mtu ayameze
maisha yako biashara familia wanao tunawaangamiza kwa jina la yesu.
Usimwangalie mtu kwa macho ya mwilini kuna urafiki wa mwili na wa rohoni eti anakwambia tuchange tuanze biashara
urafiki wa rohoni hauchagui tajiri au masikini yesu kristo hawezi kututenge
maana anatujua sisi ni wake ifike wakati adui zako waiogope familia yako maana
ukiomba vikao vyao wanaharibikiwa wakienda kukujadili vikao haviendi kabla huyu
nyoka hajameza msomo mtaji akili ndoa tunamng’oa kwa jina la yesu mungu ni wa
majira na nyakati unaweza ukalia leo kesho ukacheka mungu anakarenda yake huwa
anaisomo akisema ndio hakuna wa kusema hapana yawezekana tarehe yako ya kupona
ni leo, Mungu alikuwa anawatembelea adam na hawa baada ya jua kupunga na
shetani akamua mungu akitoka tu nayeye anaingia leo tunamng’oa unapotaka kufanikiwa ndipo vita inainuka,
hapo mwanzo kulikuwako neno naye neno
alikuwako kwa mungu naye neno akafanyika mwili akaja akakaa kwetu uliye kuja
tasa jiandae kupokea neno tena imeandikwa kwa kupigwa kwake sisi tumepona hili
neno laweza kuwa chakula mkake, fedha, afya nyumba mtaji hili neno laweza
kubadilika uliyeteseka kwa miaka mingi jiandae kupokea neno. Petro alipokuwa
ameenda kuvua samaki usiku mzima akakosa lakini yesu alipokuja akamwambia
chukua nyavu zako utavua samaki maana yake hata biashara yako unayoifanya huoni
mtu anaulizia usibadilishe biashara bwana atatenda kupitia hiyohiyo.Tunalituma neno
la mungu kwenda kila mahali halipotei bure linapotumwa sehemu linaponya magonjwa
tunatuma mshale wa bwana unaenda mtaa kwa mtaa kata kwa kata nyumba kwa nyumba utanyooka
kumtafuta adui yako huwezi kulizuia neno ni lazima litapenya tu kwa wale wanaokutesa.