SOMO LA LEO_TAREHE 17/5/2015_KUVUNJA NA KUKATAA MAGONJWA
YANAYOTOKEA KWA WAKATI MAALUMU: RP MKAMA_UFUFUO NA UZIMA KIGOMA
Kuna watu wanaugua kwa wakati maalumu, yaani ikifika jioni
anaugua, huo ni wakati maalamu uliopangwa ili ukifika augue,Lakini kuna mtu
mwingine mwisho wa mwezi ukifika (mshahara) magonjwa yanatokea, kuna mapepo
yamejiiandaa kusababisha magonjwa kwa wakati huo ili atumie mshahara wake
kutibia magonjwa na sio kufanya mabo ya maana; mwingine akitaka tu kwenda shule
anaugua , hii ni kwasababu wachawi wameweka wakati huu kuwa maalumu kwa ajiili
ya mtu ili augue,
Wachawi wanatumia photocopy kutoka kwa Mungu, Mungu hasahau akiamua
kufanya kitu kwa wakati Fulani lazima akifanye, alimuahidi SARA kupata mtoto
kwa wakati Fulani na wakati huo ulipofika SARA alipata mtoto, mapepo pia
hayasahau, kama watu wanakaa vikao na kuweka wakati maalumu kwa kutumia miungu,
jua, mwezi ili muda Fulani ukifika augue
ama wanaweza kupanga baada ya miaka kumi na tano augue, muda huo ukifika
unaugua maana mapepo hayasahau. Au wanaweza kuyatuma mapepo baada ya kuanza
masomo asifauru, basi muda huo ukifika hatafauru.
Kuna mwingine
akichukua jembe kwenda kulima anaugua,
au akipanga kwenda kazini anaugua,leo
tunakwenda kuvunja na kukataa magonjwa yaliyowekwa kwaajili ya wakati maaalum.
Kumbukumbu 4:15-19
Wachawi wanapanga muda maalumu wakumtesa mtu, mwingine saa 2
ni muda wake maalumu wa kuugua kwakuwa kuna watu walikaa vikao nakuuweka wakati
huo. Kuna dua ikisomwa mchana kila ifikapo mchana unauguua. Na hapo watu
hudhani ni magonjwa ya vipindi kumbe ni mapepo yamewekwa ili kuleta magonjwa
wakati huo.
Kuna dua zingine hasomwa siku saba, kuna zingine
haziruhusiwi kufanya ukiwa umekaa. Na anapofanya haya anayafanya kwa wakati
maalumu.Anaweza kuchukua yai lililooza kwamujibu wa madhabahu yake, nakusema
kwamba yai hili linavyochukiwa na biashara yake ichukiwe namna hii. Kwakuwa
amekwenda kusujudu kwenye miungu na ikampa nguvu yakuachilia balaa na mikosi,
sasa hapo bila Damu ya Yesu huwezi kutoka salama.
Yeremia 8:2
Kuna wakati ukipata hela unaugua na hela zikiisha tu unapona.
Hii ni kwasababu wataalamu wamekusoma kwa kupitia nyota,mwezi na majeshi ya
mbinguni. Kumbe kuna magonjwa yanayotusumbua leo na kutuhangaisha leo kwakuwa
kuna watu walipanga katika madhabahu zao ili muda Fulani ukifika uhangaike.
Kuna wengine magonjwa au matatizo ni ya sehemu maalumu,
utakapoingia ofisi yoyote kufanya kazi uugue kwakuwa kuna pepo ambao
wameachiliwa ili ufikapo mahali Fulani unaugua, na kwakuthibitisha hili
ukijaribu kuhama sehemu ya kazi unafanikiwa. Je ni eneo gani ambalo ukikaa
matatizo au magonjwa yanakupata. Ukiona hivo ujue pepo wamewekwa ili ukienda
mahali Fulani usifanikiwe.Wakati mwingine eneo/sehemu maalumu inaweza kuwekwa
kwaajili ya kukutesa.
2 wafalme 17:16
Unaweza kusema unaumwa, hakuna maagano ambayo yanaweza
kutolewa bila sadaka kuwepo mahali hapo
Kutoka 13:5__Mungu anawapangia waisrael kuwa muda huu wataushika utumishi
huu. Hivo hivo na upande washetani wanatumia photocopy kutoka kwa Mungu. Muda
Fulani wanauweka maalumu kwaajili yakufanya kitu au jambo
Kutoka 13:1 __Mungu aliwaambia wamtakasiye yeye wazao wa
kwanza wote, wa watu na wawanyama, hivyohivyo hata shetani anawataka wazaliwa
wa kwanza ili kupitisha mambo yake.utashangaa wazaliwa wakwanza walio wengi
hawana muelekeo au wanauguaugua.
Kutoka 20:4