IBADA YA LEO
TAREHE 24 MAY, 2015: SOMO -SAUTI YA BARAGUMU-RP MKAMA
Ni sauti
inayotangaza watu kufunguliwa na kuwa huru kutoka kwenye vifungo vya ibilisi
sauti iliyosikiwa na manabii kwenye kisiwa cha patimo leo ni lazima tuyaambie mapepo
yaliyotumwa ili kutuzuia katika maisha yetu, tunayaambia kwa sauti ya Baragumu;
wana Israel walipiga kelele ya Baragumu hadi ukuta wa yeriko ukaanguka na waliopo
kwenye mashimo watakwenda kusikia sauti.
UFUNUO 11:15 Malaika wa saba akapiga Baragumu,
pakawa na sauti kuu katika mbingu zikisema ufalme wa BWANA wetu na wa kristo
wake naye atamiliki hata milele.
Leo ipo
sauti ya Baragumu ili ule ugonjwa uliokusumbua uuambie kwa yatosha tunakwenda
kuyaambia nyamaza tunasonga mbele, hata ulete majambazi au polisi hatutanyamaza
maana wamewekwa watu wa Mungu ili waseme
kwa sauti ya Baragumu tuko kwenye kipindi cha malaika anayepiga Baragumu.
UFUNUO 11:13 Na katika saa ile palikuwa na
tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka wanadamu elfu saba
wakauawa katika tetemeko lile na waliosalia wakaingiwa na hofu wakamtukuza Mungu
wa mbinguni
Sehem ya
kumi ya mji wa kigoma ya mji wa kasulu tunaikomboa na kuilejesha, sehem ya kumi
ya maisha yetu lazima itoke kwenye shimo la kuzimu, wengine wanaweza wakawa
unaingia nao kanisani unasema nao BWANA Yesu asifiwe au utukufu lakini hao hao
ndio wameshikilia sehemu yako ya mafanikio, sehemu ya kwanza hadi ya kumi
iliyokufunga lazima iangamie kwa jina la Yesu.
YONA 2:5-7 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu, vilindi vilinizunguka mwani
ulikizinga kichwa changu nalishuka hata pande za chini za milima hiyo chini na
mapingo yake yalinifunga hata milele, lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka
shimoni, Ee BWANA Mungu wangu.
Wale
wanaoishi katika dunia ndio wanaoweza kukufunga wakaao katika dunia ambao
upande wao wameutegemeza kwa shetani lakini leo tunawaambia waachie kwa jina la
Yesu leo kwa sauti ya Baragumu lazima
wachawi waachie sehemu yetu maana Yesu alisema yeye ni samba wa kabila la yuda.
Ile vita iliyopiganwa mbinguni aliyepigana na joka alikuwa ni Yesu na ndiye aliyemtuma malaike apige Baragumu watu
wafunguliwe, jehanamu ni hasira ya Mungu maana ndiye anampiga shetani,
unapotaka kuuona ufalme wa Yesu wewe endelea kusonga mbele hata wakwambie sisi
ni freemason usikate tamaa maana sisi siyo wakwanza hata yasu walimwambia
anatoa pepo kwa beli-zebubu. Nabii YONA alisema amefungwa na nguvu za dunia
ambazo wanaokaa ndani ya dunia ndio wanaweza kumfunga mtu kutokufikia mafanikio
yake wanaipeleka sehemu yake ya mafanikio kwenye shimo la kuzimu.
KUTOKA 15:14-17 Kabila za watu wamesikia
wanatetemeka wakaao ufilisti utungu umewashika.ndipo wajumbe wa dedomu
wakashangaa watu wa moabu wenye nguvu tetemeko limewapata watu wote wakaao
kanaani wameyeyuka. Hofu na wofa umewaangukia kwa uweza wa mkono wako wanakaa
kimya kama jiwe hata watakapovuma watu wako Ee BWANA hata watakapovuma watu
wako uliowanunua.utawaingiza na kuwapanda katika mlima wa urithi wako mahali
pale ulipojifanyia Ee BWANA ili upakae pale patakatifu ulipopaweka imara BWANA
wa mikono yako
Mungu
anaponyoosha mkono wake juu ya watesi na maadui zetu upande wa manefili upande
wa wafilisiti maandiko yanasema utungu
unawashika maana BWANA anatangaza kwa sauti ya Baragumu, Asimamaye mbele yako
kukuzuia au nyuma yako kukushika mwambie sikuogopi maana BWANA yukopamoja nami,
wale wachawi wanaokutesa utungu unawashika maana BWANA ananyoosha mkono wake
juu ya mfilisti anayejiinua. Leo wachawi wanaposikia tunapita tunaelekea kwenye
Baraka zutu tunaamuru tetemeko liwashika wanatuma majambazi wanapeleka sumu
lakini BWANA alitujua tangu tumboni mwa mama
zetu na ametuweka juu ya mataifa aliyetuwekea sanda katika ulimwengu wa
roho tunaivua kwa jina la Yesu. Kila aliye kinyume na mimi akaye kama jiwe na
hofu imshike kwa jina la Yesu ili maadui wajue ipo sauti ya Baragumu inayonena
ili kufungua watu.
ZABURI 59:12-13 Kwa dhambi ya kinywa chao na kwa
neno la midomo yao wanaswe kwa diburi chao kwa ajili ya kulaani na uongo
wasemao, uwakomeshe kwa hasira uwakomeshe watoweke wajue ya kuwa Mungu atawala
katika yakobo na hata miisho ya dunia,
Unaweza
ukachukua maneno yale yale wanayonuiza juu yako ukamwambia Mungu waingie
wenyewe, maana wachawi wanaposhidwa mipango yao ya rohoni wanaweza wakakujia
mwilini lakini tumepewa mamlaka juu ya pepo wabaya, mamlaka ya kukanyaga nge
na nyoka wala madhara hayatatupata hata
ukute wamepasua vyungu wewe kemea kwa jina la Yesu. Maandiko yanasema hakuna
jaribu ambalo halina mlango wa kutokea na hakuna jaribu linalokuja zaidi ya
kiwango chako cha imani labda Mungu awe anahitaji kufanya kitu cha tofauti juu
ya maisha yako. Adui wanatakiwa wajue anayetawala ndani yako yupo mpaka miisho
ya dunia wajue anayekulinda yupo pamoja na wewe, anayetawala ndani yako akisema
neno linakwenda kutendeka kama ulivyosema na kiasi cha imani ulicho nacho
kinaweza kusaidia uwaambie wanaokuzuia wakae kimya kiwango cha imani kikiwa
kama punje ya haradani unao uwezo wa kuuambia mlima huu ng’oka ukatupwe
baharini ni lazima tuwasimamishe wachawi wawe kama mawe nasi tupite katikati
yao sauti ya Mungu imekwisha kutamka waanguke mbele yako, uliyekwisha
kuokoka umetangaza vita na anayepigana
siyo wewe yuko pembeni yako anakutuma maana wakuu wa dunia wamekwisha kuanguka
YONA 4:5-7 Ndipo YONA akatoka mjini akaketi
upande wa mashariki wa mji akajifanyia kibanda huko akakaa chini yake uvulini
hata aone mji ule utakuwaje, na BWANA Mungu aliweka tayari mtango akaufanya
ukue juu ya YONA ili uwe kivuli juu ya kichwa chake na kumponya katika hali
yake mbaya basi YONA akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango lakini siku ya
pili kulipopambazuka Mungu akaweka tayari buu nalo likautafuna ule mtango
ukakatika.
Watesi wetu
wanapokuwa wametengeneza mambo yao wanakaa pembeni ili kuangalia yanayotokea,
Mungu analitazama kanisa wachawi wanakutazama wewe ili waona waliyokufunga nayo
wanakuangamiza lakini maandiko yanasema iko huruma ya Mungu ambayo anahurumia
hadi wanyama. Wachawi wameketi pembeni ili waone tunavyoangamia kama YONA
alivyokaa pembeni ili kuona kitakachotokea kwenye mji wa ninawi, mwambie Mungu
wamekaa pembeni yangu ili wayaone waliyonifanyia.