JUMAPILI TAREHE: 14/06/2015
SOMO:ALIYEMEZA
MP. MORIS
UFUFUO NA KIGOMA
Ufunuo 12:1-5 Haya ni maono ya mtume Yohana. Yohana anaona
maono, anamuona mwanamke amewekewa jua na mwezi chini ya miguu yake na juu ya
kichwa chake “nyota” kumi na mbili. Nyota
inaweza kumfanya mtu kutajirika. Kama nyota yako imefungwa rohoni , maisha yako
yatakuwa ni giza.
Yohana aliendelea kuona maono, ishara nyingine ikaonekana
mbinguni , joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Na juu ya
vichwa vyake vilemba saba na mkia wake wakokota theluthi za nyota mbinguni na
kuziangusha katika nchi.
“Na Yule joka akasimama mbele ya mwanamke aliyetayari kuzaa,
ili azaapo, amle mtoto wake”.
Kumbe shetani anavizia maisha yako , anawinda kazi yako ,
anawinda elimu yako, ili upate kumeza mafanikio yako.
Mwanzo 41:24 Na hayo
masuke dhaifu yakameza masuke saba mema.
Nyakati za kuinuliwa kwako zinaweza kumezwa. Yamkini una kazi nzuri na kipato kizuri, ila kila
upatapo mshahara au wakati wako wa mavuno ukiwadia, utajikuta magonjwa
yanainuka, ajali na mambo mengine yanayo fanana na hayo, ili usiweze kufaidi
matunda yako; yanainuliwa hayo ili
yameze mafanikio yako.
Kutoka7:11
Sasa tumelitambua hilo, “fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao”
Walete waletavyo, hawatatuweza kwamaana
leo tunayo fimbo imezayo fimbo zao zote.
Utakuwa wa kutoa mshahara na si kupokea tena! Utakuwa wa
kuajiri na si kuajiriwa tena! Utakuwa wa kukopesha na si kukopa tena
haleluya!!!
Ayubu 20:15 “Amemeza mali, naya atayatapika tena
Mungu atayatoa tumboni mwake”.
Una maduka makubwa
lakini yamemezwa, hayaonekani.
Tumbo linalozungumziwa hapa ni kuzimu . Yaani anameza mali
na kuzihifadhi tumboni mwake.
Hata mtu anaweza kumezwa, ndipo utakuwa mdhaifu kila wakati
kwani umo katika tumbo la kuzimu.
Yona 2:2-10
Yona aliomba akiwa ndani yatumbo la kuzimu, watu pia
wanaweza kumezwa.
Moyo wa bahari ndo kuzimu yenyewe
Mtu ukitupwa ndani ya shimo, hauna raha ya kuishi tena.
Afya yako imemezwa, mali zako zimemezwa, umekuwa mtu wa
mawazo tu, umekata tama wala huna tumaini. Leo nakutangazia, hakuna atakaye kaa
chini tena, anakuinua leo anakutoa leo kwenye
shimo la magonjwa, shimo la umasikini, shimo la utasa, BWANA Yesu
ameshuka mwenyewe kukuto leo haleluya!
“BWANA akasema na samaki, naye akamtapika Yona pwani”
Leo BWANA anasema na ugonwa huo unaukutesa, anasema na shida
zako, nazo zitakutapika wewe kwenye uzima na Baraka zako.
Isaya 42:22 “ Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa;
wote wamenaswa na kutekwa; wamefichwa aktika magereza; wamekuwa mawindo wala
hapana aokoaye; wamekuwa mateka wala hapana asemaye, Rudisha”
Magereza yapo katika ulimwengu wa roho , kuna magereza ya ndoa, biashara, kazi
,elimu na nagereza nayo yamefichwa katika ulimwengu wa roho; Na Yesu yupo hapa sasa, yupo katikati
yetu ili kuwaweka watu huru.