SOMO LA LEO_TAREHE 26 / 7 / 2015_KUBOMOA KITI CHA ENZI: SNP
PAUL JOSHUA_UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.
Kila anayeongoza watu kuna kiti chake ambacho anakalia.
Ukienda sehemu yoyote… kila mtawala wa mwilini na mtawala wa rohoni anakiti
chake cha katika utawala wake. Hata Mungu wetu amekaa katika kiti chake cha
enzi
Ufunuo 7: 9-12
Baada ya hapo tutaona kuwa kuna watu wamekalia viti vya
enzi na wanatawala eneo hilo. Tukifanya
kwa mapenzi yetu tutashangaa mtawala huyo atatutawala mpaka nyumba na mifugo
wetu.
2 Samweli 3:9
Huwezi kufanikiwa sehemu mpaka umpige anayetawala eneo hilo.
Huwezi kufanya biashara sehemu mpaka umpige mtawala wa eneo hilo.
Kiti ni maisha kitikinakupa utawala wa eneo hilo pamoja na
kila kitu na mali. Mtawala akisema hakuna mnakuwa hamna ujanja.
Familia zote zaweza kulia njaa,elimu mbaya, madawa hayatoshi
lakini mtawala hana tatizo hilo wala shida hiyo.
Zaburi 11: 4
Kumbe Mungu naye anakopoe, ana macho. Tena anakiti na
anatawala. Ukitaka kutawala wewe pasua kiti cha utawala, ukipasua atakaa chini
na akikaa chini maana yake mtawala.
Ufunuo 2:13
Unaweza kukaa sehume yoyote kwaamani na furaha kama utafanikiwa kumpiga mtawala. Ndio maana kila
sehemu zinatofautiana maana watawala wanatofautiana. Mambo ya kigoma
yanatofautiana na mambo ya mwanza maana sehemu hizi zina viti vya enzi tofauti
katika ulimwengu wa roho
Maeneo ambayo shetani ameweka kiti chake cha enzi
1)
Anga , angani kuna kiti cha enzi cha shetani,
anatawala lakini pia elewa kuwa shetani anaitwa mfalme wa anga.
Unajua sio kwamba watu hawaombi ila
wanaomba kwa kukosa maarifa ya vita vya rohoni
Daniel, Mungu anasema kila aombaye hupewa
lakini mbona hatupati? Je Mungu ni muongo? Mungu amekwaisha kujibu bali yupo
mkuu wa anga azuiae.
Kuna mbingu ya kwanza ya pili nay a
tatu,ili maombi yako yapenye ni lazima uwe rohoni sana
2)
Kiti cha enzi cha baharini
3)
Kiti cha enzi katika nchi
Matendo16:16
Anayetawala nchi ana utawala wake
anaouongoza
Kiti cha enzi ndicho kinachochagua upate
pesa au mafanikio, huwezi kumiliki bila kumpiga mkuu wa anga
Paul alihubiri sana lakini alikuwa hajagusa
kiti cha enzi cha shetani, unaweza ukaomba sana hujajibiwa, kuna sehemu moja tu
ukigusa ambayo ndiyo kiti cha enzi, ukigusa tu , unafanikiwa. Unapoomba
hakikisha unaomba mpaka uhuse kiti cha enzi.
Sio kila kitu ni cha kutii na sio mamlaka ni
yakutii lakini maana anaweza akasema mkubwa au mwenye mamlaka maana unaweza kujikuta unatii yasiyo mapenzi ya Mungu, kwani shetani
anaweza kumtumia mtu yeyote katika ukoo au nchi au familia ili kupitisha mawazo
yake au matakwa yake. Hivyo sio kila mamlaka ni yak utii , chunguza kwanza ni
kiti kipi cha enzi kinachoongoza ndani ya mamlaka.