Regina Josias mwenye umri wa miaka 15, mwanafunzi wa kidato
cha 2 katika shule ya sekondari ya Bushabani.
Ni binti amabaye anajitahidi sana katika masomo hali kwamba
anaongoza kila jaribio au mitihani ya ndani na nje ya mkoa yaani kufeli kwake yeye anakuwa mtu
wa pili.
Ililikuwa mwezi wanne mwaka jana 2013 binti huyu akiwa
anajiandaa na vipindi vya darasani asubuhi
siku ya jumatano, alishikwa
ghafla na ugonjwa wa macho hali ambayo ilisababisha hata asiweze kusoma
Lakini ugonjwa wa binti huyu ulinishangaza kidogo kwani aliweza
kusoma vitbu vya katuni na magazeti ambapo
ukimpa daftari au kitabu ya darasa au chochote kinachohusiana na shule,
hakuweza kuona kabisa.
Siku moja aliona nyoka darasani wakati wanafanya mitihani ya
mock mwaka huu, ndipo hali ilizidi kuwa mbaya na kurudishwa nyumbani kwa wazazi
wake; Nao wazazi wake walidai kwenda kwa mganga lakini Regina alikataa na
kusema siwezi kwenda huko ila npelekeni kanisani, akaendelea kusema nasikia
kuna kanisa lipo Msanga linaponya watu wenye matatizo mabalimbali.
Ndipo wazazi wa Regina waliamua kumleta katika kanisa ambalo
linaponya watu wenye magonjwa na shida mbalimbali linaloitwa UFUFUO NA UZIMA
KIGOMA.
Baada ya kuombewa, Regina kawa mzima kabisa, anaweza kusoma
vizuri.
Sasa kawa manajeshi wa UFUFUO NA UZIMA, anarudi shule kusoma kwa nguvu mpya mpaka ndoto yake itimie.