SOMO LA LEO 15/10/2017,
SNP:PAUL JOSHUA,
KIFUNGO CHA MAUTI.
Mauti ni kifo,
ZBURI 102:20. Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, na kuwafungua walioandikiwa kufa. Mungu huwafungua waliondikiwa kufa, kuna watu wengine wameandikiwa kufa. Mtu anaugua lakini unakuta ameandikiwa kufa, ugonjwa huo ni ugonjwa kwaajili ya kuleta mauti. Unaona mtu anaugua malaria isiyo isha lakini mwisho wake ni kifo, ama typhoid lakini mwisho wake ni kifo, lakini zaidi yoyote adui anaweza kukufunga kwenye magonjwa, unajiona unamagonjwa na unatumia pesa zote kutibu magonjwa hayo na mwisho ya yote unakupeleka kwenye mauti. Kuna ufungwa wa rohoni kama ilivyo kwa wafungwa wa gerezani, wamefungwa lakini kila mtu anahukumu yake. Hivyo hivyo mtu amefungwa na matatizo mengi lakini ameandikiwa hukumu na hukumu hiyo inaweza kuwa ya mauti.
Shetani na mawakala wake wanaweza kuifunga familia. Wanaweza kufunga watoto, ndoa, uchumi ama kazi.
MITHALI 24:11 uwaokoe wanaochukuliwa ili wauwawe nao walio tayari kuchinjwa uwaokoe.
Kuna watu waliochukuliwa kama wafungwa lakini mwisho wake ni kuuawa. Unaweza kufungwa na aliyekufunga hujui alimaanisha nini kukufunga. Na mara nyingi tatizo linaanza kidogo, maana shetani huanza kidogo kidogo na baadae anafanya tatizo linakuwa kubwa na hatimae anakumaliza.
ISAYA 42:7 kuyafunua macho ya vipofu, kuwatoa gerezani waliofungwa, kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa.
Ni nyumba ya mtu lakini inatumika kufunga, ni gereza. Kwaniwa wachawi wanafunga maisha yako, wanaona nyota yako na hatima ya maisha yako nao wanakufunga. Unakuta mtu anamaisha magumu, lakini akifunguliwa tu hata maisha yake yanabadilika.
LUKA 13:10-16… na huyu mwanamke aliyeuzao wa Ibrahimu ambaye shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato.
Shetani anaweza kumfunga mtu asifanikiwe, wachawi wanaweza kukufunga usizae au usifanikiwe. Lakini Yesu hatakuacha kwenye vifungo hivyo.
Yusuphu alizingiziwa amembaka mke wa mfalme lakini bado Yusuphu alikuwa amebeba kusudi la Mungu ndani yake,ndio mana hakumwacha waLa kumpungukia hata ndani ya gereza bado Mungu alikuwa pamoja nae,Mungu wetu si Mungu wa hasara Mungu wetu ni Mung wa faida,ni bora aangamize watu lakini kusudi lake libaki limesimama.
Kuna kitu Mungu alikupa ambalo kupitia hicho Mungu atakutoa ndani ya Gereza,Yusuphu amekaa gerezai na wafungwa wenzio badae wakaota ndoto lakini ndoto zikawachanganya,Mungu akamuandaa yusuphu kuwa jibu la ndoto zao zilizowachanganya,akawambia mana ya ndoto zao,badae Mfalme nae akaota ndoto ikamchanganya sana akawaita wachawi,waganga,wasoma nyota wote hawakufanikiwa,badae akaitwa Yusuphu akatafsiri ndoto ya Mfalme badae akatolewa gerezani na kuwa waziri mkuu,Mungu alimuinua yusuphu kwa kile alichompa ndani yake ndicho kilicho mtoa gerezani,na kupita karama hio Mungu aliompa akamuinua.Alianza kama mfungwa lakini akamaliza mwenye heshima,na kuwasidia ndugu zake kupitia kile Mungu alichoweka ndani yake.
Kusudi la Mungu kwenye maisha yako ndilo litakalo kutoa kwenye shida unayopitia leo,lakini shetani anafanya njia ya kukuonesha kwamba huwezi kutoka hapo ulipo lakini nakwambia Mwana wa Mungu kwamba mwenye Mungu mpe mda tu,Mungu atamuinua
MAMBO YA WALAWI 19:26 Msile kitu chochote pamoja na damu yake,wala msifanye kuroga wala kutumia utambuzi,kumbe mtu anaweza kurogwa na wachawi,waganga, wasoma nyota ili usifanikiwe,usiolewe,usizae,wala usifanikiwe kwenye maisha yako,lakini leo mtu wa Mungu unatoka na Mungu akikutoa hapo watu watakushangaa,mana hata kuacha kama ulivyo.
ZABURI 18:4 Kamba za mauti zilinizunguka, mafuliko ya uovu yakanitia hofu,kamba za mauti zilinizunguka na mitego ya mauti ilinikabiri,kuna watu wamefungwa na kamba za Mauti umetumia kaili zako na ngvu zako lakini imeshindikana kwa sababu aliekufunga alimaanisha kukufunga na alitoa sadaka,na mwisho wake alikdhamilia ni kifo,lakini kile ambacho Mungu amepanda ndani yako ndicho kitakacho kuponya ili kusudi la Mungu litimizwe,ni maombi yangu mchana wa leo Mungu kausogeree pale ulipo ili akuponye aiponye ndoa yako,biashara yako,kazi yako na familia yako kwa ujumla.
Wakati mwingine Mungu anaruhusu upitie kwenye hali Fulani ya tatizo ili ujifunze,na badae uwe mwalimu wa wengine,usiogope kwa yale unayopitia leo Mungu anakusaidia leo.