GROLY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA - KIGOMA,
SOMO: DAMU JUU YA SHERIA,
AP: MORIS
TAREHE 12/11/2017.
WAEBRANIA 9:22 Hii ni damu ya agano mlioamuriwa na Mungu,na ile hema nayo na
vyombo vyote vya Ibada alivinyunyuzia damu vivyo hivyo,na katika Torati karibu
vitu vyote husafishwa kwa damu na pasipo damu kumwagwa hakuna ondoleo, mtume
Paulo anazungumza na waebrania kwamba waitumie damu ya Yesu kwenye maisha yao
kama agano waliloamuriwa na Mungu na kupitia hii damu inasamehe dhambi, inaponya
magonjwa na kuwa upatanisho kati ya Mungu na Mwanadamu.
Damu ya Yesu ni daraja kati ya Mungu na Mwanadamu, unapoitumia
damu ya Yesu magonjwa yanatoweka. Damu ya Yesu kuna wakati inaitwa damu ya
mwana kondoo ndio maana tunajifunza kwamba tunaweza kuwashinda mashujaa wa dunia
kwa Damu ya Yesu na kwa neno la ushuhuda, sdamu hii inaweka upatanisho na
kuwaweka pamoja na Mungu na mwanadamu, ndio mana kama mkristo unahitaji
kuitumia sana hii damu ya Yesu kristo maana inatenda kazi jana leo na hata
milele.
Shetani nae hutumia damu ili kuyaharibu maisha ya watu, kupitia
mawakala wake kama waganga, wachawi, na wasoma nyota; wanaweza kutumia damu ili
kuchafua maisha ya mtu. Maisha ya mtu yanaweza kuchafuka kwa ama kusafishwa kwa
damu, wachawi wanaweza kuitumia damu na wakafanikiwa katika mambo yao kwa
sababu ni sheria ya rohoni. damu ni uhai, kuna vitu ambavyo damu imevibeb;
Imeandikwa, kushindana kwetu si juu ya damu na nyama, kumbe damu inaunganisha
mwili na Roho na kutenda kazi na kuyatimiza makusudi yake.
Damu inatakasa, inapatanisha, inatetea, inalinda, ni daraja
kati ya Mungu na mwanadamu ndio mana tunaitumia damu ya Yesu kunyamanzisha kila
damu inayoongea mabaya kwenye maisha yetu; kama ni damu ya mwanadamu, damu ya
kuku, damu ya kondoo ama ya ngombe tunanyamanzisha kila damu kwa damu ya Yesu kristo.
Ili maisha yako yafanikiwe na yainuliwe yanahitaji damu ya
Yesu, huwezi kushinda pasipo damu ya Yesu na kwa damu hii tunabatilisha kila
damu za waganga na za wachawi waliofunga maisha yetu kwa damu ya Yesu. Amina.