GLORY OF CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA UZIMA KIGOMA
SOMO: MTU WA NDANI_MCHUNGAJI PAUL JOSHUA
TAREHE: 03/12/2017
1Wakorinto 15:40; Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ya duniani ni mbali.
 kuna mtu ambaye asili yake ni duniani na kuna mtu ambaye asili yake ni mbinguni; Kuna mwili wa asili ambao ni udongo/mavumbi na kuna mwili wa roho ambao asili ni mbinguni; Kumbe roho inamwili. Mungu ni roho lakini ana macho, ana kinywa, ana masikio, ana miguu; unavyoona jinsi mwili wa nyama ulivyo na vingo ndivyo na mwili wa roho ulivyo. Wachawi wanapotaka kumshambulia mtu hawaangalii mwili wako wa nje ila huangalia ndani, wewe ninani. Sasa mtu wa ndani anatakiwa afanye kazi, ashinde maana ndiye ana kila kitu chako. Mungu anaweka baraka kwenye kiungo cha mtu. Kuna mtu akiongea tu ni kama mtu aliye soma sana wakati elimu yake ni darasa la saba; ni kwakuwa baraka zake ziko kinywani.
Maskio; mtu aliye barikiwa masikio ya rohoni atasikia kila kitu hata kama hayupo eneo husika (anapata raarifa zote za rohoni). Kuna watu ni viziwi wa rohoni, hawawezi kusikia chochote hata kama atazungumziwa hali na yeye yupo. Wachawi wakijua unasikia wakiwa wanafanya vikao vyao (kwa sababu una masikio ya rohoni) wataanza kukuwinda ili kufanya vita na wewe. Ukiwa muombaji halafu unamasikio, una macho na unakinywa, unauwa wachawi wote. Masikio ya rohoni yakichukuliwa unakuwa kiziwi wa rohoni.
Sura; Ni kumpa mtu kibali mbele za watu. Kuna mtu anaweza kuwa wa kawaida tu lakini sura yake ya ndani ikawa imebarikwa; hivyo utaona anapata kibali sehemu  nzuri usiyo dhania. Kuna soko la kimataifa la kuuza nyota za viungo vya binadamu, Viungo vya mwili mmoja vinaweza kugawanywa kwa watu hata zaidi ya kumi; Utakuta akili anauziwa mtu mwingine, nywele, kucha, macho, masikio, miguu, mikono, na vinginevyo vingi.  Ufunuo 18:11 Hawa ni wafanya biashara wa nchi/dunia, ni biashara ambayo wanauza viungo vya miili na roho za binadamu. Mtu unapoenda kwa mganaga wa kienyeji kutafuta kibali au nyota ya maisha, ukweli  ni kwamba, mganga wa kienyeji yeye kama yeye hana kitu chochote cha kukupa wewe bali huchukuwa viungo vya rohoni kutoka  kwa mtu/ watu tofauti tofauti na kukupachikia wewe.
Kinywa;(Kinywa cha rohoni) Mungu aweza kuweka Baraka kwenye kinywa cha mtu. Mutu ataweza kuongea na mtu yeyote. Kuna  mtu alikuwa anatumiwa kuongea sehemu mbali mbali hata kwa kukodiwa ili aongee kwa niaba ya wahusika kwani maneno yake yalikubalika  kila alipoongea; na hivi leo  mtu huyo anaonekana pumba aongeapo kwani kinywa chake cha rohoni hakipo tena, kimeshachukuliwa na wafanya biashara wa viungo vya miili na roho za binadamu kuuzia watu wengine. Utakuta mtu mwingine anaongea matusi, kusengenya wengine tangu asubuhi mpaka jioni kwasababu hana mdomo wa kuonelea na si kwamba anapenda la, anatamani sana kuongea mazuri ila kinywa chake hana, kinatumika na mtu mwingine na huyo mtu anaye tumia kinywa cha mtu huyo utaona hata akiimba au akiongea neno lisilo maana yoyote, atakupalika sana kwani kinywa anachotumia ni kinywa chenye kibali. Pia kuna kinywa chenye nguvu; Mtu mwenye kinywa chenye nguvu akitamka jambo lolote kuwa leo  litatokea, na inakuwa hivyo kwa sababu kinywa chake ni chenye nguvu na mamlka. Kinywa kinaweza kufungwa au kuchukuliwa na wachawi, utakuta mtu anabiashara ila anashindwa/hawezi kuongea na mteja kumshawishi anunue.  Kinywa kina ambatana na ujasiri. Kuna siri kwenye kinywa, kama huna ujasiri huwezi kuongea na mtu yeyote hata kama yeye anahitaji aongee na wewe; na watu wengi wamechukuliwa kinywa. Wachawi/waganga wanaweza kuchukua kinywa. Ukiwa na kinywa cha rohoni:- Unaweza kuongea na mtu yeyote, Unaweza kuomba chochote kwasabau unanguvu na mamlaka kwenye kinywa.
Tumbo: Kuna matumbo ya kiroho; Mungu anaweza kubariki tumbo lako, Utakuta Mungu alikuchagua akaribariki tumbo lako kuzaa viongozi wa nchi, wachungaji, watoto wazuri; Lakini wachawi wakaliona hilo tumbo mapema hivyo wakalichukuwa na hivi leo analitumia mwingine na wewe huku unazaa watoto wa ajabu au hakuna kabisa kwani hauna tumbo la uzazi. Wewe uliyepata neema ya kuyafahamu haya, chukua hatua mapema kurudisha kila kiungo cha mwili wako kilichochukuliwa na wafanya biashara wa viungo vya miili ya wanadamu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Amen!