GLORY OF
CHRIST TANZANIA CHURCH
UFUFUO NA
UZIMA KIGOMA
SOMO: MTU
WA NDANI_MCHUNGAJI PAUL JOSHUA
TAREHE: 03/12/2017
1Wakorinto 15:40; Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya
duniani; lakini fahari yake ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ya duniani ni
mbali.
kuna mtu ambaye asili
yake ni duniani na kuna mtu ambaye asili yake ni mbinguni; Kuna mwili wa asili
ambao ni udongo/mavumbi na kuna mwili wa roho ambao asili ni mbinguni; Kumbe
roho inamwili. Mungu ni roho lakini ana macho, ana kinywa, ana masikio, ana
miguu; unavyoona jinsi mwili wa nyama ulivyo na vingo ndivyo na mwili wa roho ulivyo.
Wachawi wanapotaka kumshambulia mtu hawaangalii mwili wako wa nje ila huangalia
ndani, wewe ninani. Sasa mtu wa ndani anatakiwa afanye kazi, ashinde maana
ndiye ana kila kitu chako. Mungu anaweka baraka kwenye kiungo cha mtu. Kuna mtu
akiongea tu ni kama mtu aliye soma sana wakati elimu yake ni darasa la saba; ni
kwakuwa baraka zake ziko kinywani.
Maskio; mtu aliye barikiwa masikio ya rohoni atasikia kila
kitu hata kama hayupo eneo husika (anapata raarifa zote za rohoni). Kuna watu
ni viziwi wa rohoni, hawawezi kusikia chochote hata kama atazungumziwa hali na
yeye yupo. Wachawi wakijua unasikia wakiwa wanafanya vikao vyao (kwa sababu una
masikio ya rohoni) wataanza kukuwinda ili kufanya vita na wewe. Ukiwa muombaji
halafu unamasikio, una macho na unakinywa, unauwa wachawi wote. Masikio ya
rohoni yakichukuliwa unakuwa kiziwi wa rohoni.
Sura; Ni kumpa mtu kibali mbele za watu. Kuna mtu anaweza
kuwa wa kawaida tu lakini sura yake ya ndani ikawa imebarikwa; hivyo utaona
anapata kibali sehemu nzuri usiyo dhania.
Kuna soko la kimataifa la kuuza nyota za viungo vya binadamu, Viungo vya mwili
mmoja vinaweza kugawanywa kwa watu hata zaidi ya kumi; Utakuta akili anauziwa
mtu mwingine, nywele, kucha, macho, masikio, miguu, mikono, na vinginevyo
vingi. Ufunuo 18:11 Hawa ni wafanya
biashara wa nchi/dunia, ni biashara ambayo wanauza viungo vya miili na roho za
binadamu. Mtu unapoenda kwa mganaga wa kienyeji kutafuta kibali au nyota ya
maisha, ukweli ni kwamba, mganga wa
kienyeji yeye kama yeye hana kitu chochote cha kukupa wewe bali huchukuwa
viungo vya rohoni kutoka kwa mtu/ watu
tofauti tofauti na kukupachikia wewe.
Kinywa;(Kinywa cha rohoni) Mungu aweza kuweka Baraka kwenye
kinywa cha mtu. Mutu ataweza kuongea na mtu yeyote. Kuna mtu alikuwa anatumiwa kuongea sehemu mbali
mbali hata kwa kukodiwa ili aongee kwa niaba ya wahusika kwani maneno yake
yalikubalika kila alipoongea; na hivi
leo mtu huyo anaonekana pumba aongeapo kwani
kinywa chake cha rohoni hakipo tena, kimeshachukuliwa na wafanya biashara wa
viungo vya miili na roho za binadamu kuuzia watu wengine. Utakuta mtu mwingine
anaongea matusi, kusengenya wengine tangu asubuhi mpaka jioni kwasababu hana
mdomo wa kuonelea na si kwamba anapenda la, anatamani sana kuongea mazuri ila
kinywa chake hana, kinatumika na mtu mwingine na huyo mtu anaye tumia kinywa
cha mtu huyo utaona hata akiimba au akiongea neno lisilo maana yoyote,
atakupalika sana kwani kinywa anachotumia ni kinywa chenye kibali. Pia kuna kinywa
chenye nguvu; Mtu mwenye kinywa chenye nguvu akitamka jambo lolote kuwa leo litatokea, na inakuwa hivyo kwa sababu kinywa
chake ni chenye nguvu na mamlka. Kinywa kinaweza kufungwa au kuchukuliwa na wachawi,
utakuta mtu anabiashara ila anashindwa/hawezi kuongea na mteja kumshawishi
anunue. Kinywa kina ambatana na ujasiri.
Kuna siri kwenye kinywa, kama huna ujasiri huwezi kuongea na mtu yeyote hata
kama yeye anahitaji aongee na wewe; na watu wengi wamechukuliwa kinywa.
Wachawi/waganga wanaweza kuchukua kinywa. Ukiwa na kinywa cha rohoni:- Unaweza
kuongea na mtu yeyote, Unaweza kuomba chochote kwasabau unanguvu na mamlaka
kwenye kinywa.
Tumbo: Kuna matumbo ya kiroho; Mungu anaweza kubariki tumbo
lako, Utakuta Mungu alikuchagua akaribariki tumbo lako kuzaa viongozi wa nchi,
wachungaji, watoto wazuri; Lakini wachawi wakaliona hilo tumbo mapema hivyo
wakalichukuwa na hivi leo analitumia mwingine na wewe huku unazaa watoto wa
ajabu au hakuna kabisa kwani hauna tumbo la uzazi. Wewe uliyepata neema ya
kuyafahamu haya, chukua hatua mapema kurudisha kila kiungo cha mwili wako
kilichochukuliwa na wafanya biashara wa viungo vya miili ya wanadamu katika Jina
la Bwana wetu Yesu Kristo. Amen!